Jamal Akbar
JF-Expert Member
- Oct 9, 2014
- 413
- 471
Mkoa wa Arusha unaongoza nchini kwa kupatikana na kuchukuliwa kwa matumizi ya huduma za simu, posta na utangazaji; kwa mujibu wa takwimu za hivi karibuni na matokeo ya utafiti mdogo.
Arusha inaongoza kwenye matumizi ya mfumo wa anwani za makazi na postikodi. Ni mkoa wa i kwa uwiano wa idadi ya laini simu za mkononi zilizosajiliwa idadi ya watu na pia kwenye huduma za utangazaji za kulipia
Jumla ya laini 3,262,398 zimesajiliwa mkoa huo wenye wakazi milioni
1.9; ukilinganisha na Dares Salaam yenye wakazi milioni sita na laini 9,102,203; takwimu za mawasiliano za Juni 2022 zinaonyesha.
Asilimia 10 ya watumiaji wa huduma za utangazaji wa televisheni kwa kulipia Tanzania wako Arusha, kwa mujibu wa takwimu hizo, zilizotolewa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Arusha ya pili baada ya Dar es Salaam kwa wingi wa ving'amuzi vya kawaida vinavyowezesha kupatikana matangzo ya televisheni za mfumo wa ardhini. Kuna ving'amuzi 314,395 Arusha na 1,230,485 Dares Salaam.
Kuenea miongoni mwa watu ni aslimia 15 Arusha na 23 Dar es Salaam. Utafiti uliofanywa na TCRA mwaka 2020 kuhusu matumizi ya anwani za makazi na mfumo wa postiodi ulionyesha kwamba Arusha inaongoza kwa uelewa wa mfumo huo.
Jiji la Arusha ni mwenyeji wa Umoja wa Posta Afrika (PAPU), ambao kwa kushirikiana na TCRA unajenga jengo la ghorofa 19 litakalotumika kwa ofisi, kumbi za mikutano na hoteli ya kimataifa.