Arusha: Kituo cha daladala Kilombero hakikidhi viwango

Arusha: Kituo cha daladala Kilombero hakikidhi viwango

Bushmamy

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2019
Posts
9,140
Reaction score
15,963
Stand ya magari madogo Kilombero Almaarufu kama stand ya Hiace ambazo daladala zote za mjini huanzia hapo haikidhi kabisa vigezo vya kuitwa stand ya daladala kutokana na sababu zifuatazo.

Hakuna vibao vinavyoonyesha kwamba hapa ndipo yanapopaki magari ya uswahili, Njiro au Usa, bali dereva anapaki popote pale ndani ya kituo hicho.

Sehemu ya kujikinga mvua na jua kwa abiria hakuna, mvua na jua vyote vyao.

Uzio, kituo hicho hakina Uzio unaoonyesha mwanzo na mwisho wa kituo,

Uboreshaji wa kituo chini hamna ni udongo tu hivyo wakati wa mvua ni matope na wakati wa jua ni vumbi tupu.

Uchafu, kituo ni kichafu kutokana na kukosekana kwa mapipa ya kuwekea taka, taka zinatupwa popote pale.
DSC_0854.JPG
DSC_0853.JPG
kituo hichi kipo katikati ya jiji
 
Nenda kule kwenye milango ya kutokea utakuta vibao vipo vinavyoonyesha magari yanapokwenda, hapo ulipo simama ni mlango wa kuingilia kwa gari zote zinazotokea moshono, njiro, uswahilini, murieth na ukanda wote wa chini ya jiji.
 
Yote uliyoandika Ni kweli tupu.Halmashauri ya Jiji Ina kila sababu ya kubeba lawama.Kama Ni mgeni hapo unajikuta umesukumiwa na Wapiga debe kwenye sehemu nyngn kabisa.Na hii ilijitokeza Niliona Kama wiki tu imepita
 
Kituo kichafu sana na Jiji wanachukua hela za ushuru wa hizo Hiace kila siku na gari moja ni zaidi ya 500 na bado fine zao kipindi cha mvua wanadanganya kwa kutupia vifusi kama sita tuu hivi...
 
Nenda kule kwenye milango ya kutokea utakuta vibao vipo vinavyoonyesha magari yanapokwenda, hapo ulipo simama ni mlango wa kuingilia kwa gari zote zinazotokea moshono, njiro, uswahilini, murieth na ukanda wote wa chini ya jiji.
Ila kituo kibaya sana
 
stendi kuwa katikati ndio inayoifanya Arusha iwe imechangamka zaida ya mwanza na iringa ndugu🤣🤣 miji yote mikubwa stendi ipo katikati ya mji mfano nairobi na kampala
 
Back
Top Bottom