Arusha: Kituo cha daladala Kilombero hakikidhi viwango

stendi kuwa katikati ndio inayoifanya Arusha iwe imechangamka zaida ya mwanza na iringa ndugu🤣🤣 miji yote mikubwa stendi ipo katikati ya mji mfano nairobi na kampala
Stendi ya Iringa ilikuwa katikati ya mji kabla ya kupelekwa Ipogolo na kuhamishwa tena.
 
stendi kuwa katikati ndio inayoifanya Arusha iwe imechangamka zaida ya mwanza na iringa ndugu🤣🤣 miji yote mikubwa stendi ipo katikati ya mji mfano nairobi na kampala
Tatizo ni hali ya stendi ilivyo inatia aibu, mimi pia nipo Arusha Sasa nakubaliana na mtoa mada
 
Ila Dar ambayo 80% ya wakazi wake wanaishi kwny squatters yenyewe ilistahili kua jiji?
tatizo ni watu wanaakili za kukurupuka
ukiacha dar hamna mji mwingine unaostahili kuwa jiji tofauti na Arusha mingine yabmchongo tu
 
Tatizo ni hali ya stendi ilivyo inatia aibu, mimi pia nipo Arusha Sasa nakubaliana na mtoa mada
mikakati ipo ya kuihamisha ila kwa sasa bado ipo katikati kama kungekua hakuna mipango ya kuihamisha ningetia neno ila mipango ipo na eneo limeshapatikana there's no need to rush it kwanza hata foleni yenyewe si kubwa kivile ikifika saa moja tu yale mataa ya kuingilia stendi yameshawasha njano😂
na hata ikichelewa kujengwa zaidi sana itatoa fursa kwa kule wanapojenga stendi mpya kwa maana ya bondeni city watu waanze kufanya uwekezaji ikiwemo maduka na mahoteli ilibkusudi itakapohama isiwe tena kero kwa wananchi
 
Tatizo ni hali ya stendi ilivyo inatia aibu, mimi pia nipo Arusha Sasa nakubaliana na mtoa mada
bado mnachanganyana mtoa mada anaongelea stendi ya kilombero ambayo kiukweli inatia aibu sana yani kunawakati nashindwa kuelewa uongozi wa jiji unashindwa hata kuweka paving pale, vibao pamoja na viti vya kusubiria usafiri ambapo naamini kabisa sio hela nyingi jiji linatia aibu mno stendi hata taa za usiku hamna. What a shame😎 ila mimi hoja yangu ilikua ni stendi ya mabasi makubwa
 
Kwa kweli stendi ya Kilombero ni TAKATAKA kabisa, kipindi cha mvua ndio balaa zaidi.
Kuna huu upande wa magari yanayoenda Njiro, Moshono, Uswahilini, Dampo yanapotokea yani hapo napo panakera sana, vigari havikai kwa mpango ni vurugu tupu.

Pia kuna swala la utupaji taka hovyo, panatia aibu sana magari ya mananasi humo humo, sema bora hata saivi vibanda vimeondolewa pamekuwa wazi kidogo lakini uchafu ni kama kawa.
 
ni afadhali hata waifunge tu iwe kama mwanzo lakin kwa hali hii ni aibu kwa jiji letu tena jiji la kitalii
 
Arusha haikupaswa kuwa jiji, ina miondombinu ya umma mibovu sana.
Tangu niijue Arusha for the first time mwaka 2010 hiyo stand iko ivoivo.

Hata ile stand ya mabasi ya mikoani ni finyu sana na imekaa pabaya.

Nilisikia wanaihamisha ila sijui kama wameshaihamisha.
 
Arusha haikupaswa kuwa jiji, ina miondombinu ya umma mibovu sana.
kuwa na miundombinu ya umma sio kigezo cha kuwa jiji mapato ndio kigezo namba moja ila siasa za upinzani zimefanya arusha kutokupewa kipaumbele licha ya hivyo bado Arusha ndio jiji la pili kwa mtandao mkubwa wa barabara za lami boss
 
Mbona Dar es Salaam, Mbeya na Mwanza kumekuwepo na siasa za upinzani ila miondombinu yao ina afadhali?

Mbona sehemu kubwa ya Tanzania haijawahi kuchagua upinzani ila kuna umaskini uliotopea?
kuwa na miundombinu ya umma sio kigezo cha kuwa jiji mapato ndio kigezo namba moja ila siasa za upinzani zimefanya arusha kutokupewa kipaumbele licha ya hivyo bado Arusha ndio jiji la pili kwa mtandao mkubwa wa barabara za lami boss
 
Arusha ina hype sana mitandaoni wakati ni pa kawaida sana

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Moshi imeipita Arusha kwa kitu gani maana kwanza mji wa Moshi jioni unakuwa hauna watu.
Lakini ukiachia hilo kuna kitu gani ambacho we unadhani Moshi imeizidi Arusha.
Kingine kinachonishangazaga inakuwaje mpaka leo Moshi sio jiji wakati imeipita mbali Arusha.
 
Arusha inatakiwa kuwa na lami kila uchochoro,, taa kila sehemu, usafiri mzuri wa umma, usalama wa kutosha nk, nk. Watalii wa leo hawapendi miji michafu. Watatupiaje picha insta na background ni vipanya na mauchafu mengine! Serikali inatakiwa kuiangalia kama mji wa kimkakati.
 
Ni lini uongozi wa jiji utapiga marufuku hivi vifodi kubeba abiria na kuruhusu coster kufanya hizo kazi?
 
Wako nyuma sana hilo jiji.
kuna vifodi vinaendaga sanawari ya juu… aisee ni vituko sana utafikiri vigari vya mkaa kumbe zinabeba abiria, vipigwe marufuku tu wenye coster wanaojielewa wapewe kazi hivi vifodi vipelekwe kwenye ile mikoa ambayo baiskeli ndio usafiki mkuu (jokes)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…