Umeme umekua ukikatika mara kwa mara hivi sasa. Jana (15/06/2024) umeme umekatika saa mbili asubui na kurudi saa moja jioni.
Leo umeme umeshinda siku nzima ila majira ya saa kumi na mbili jioni umekatika (ratiba kama ile ile ya mgao).
Hili linakuja bila taarifa yoyote kutoka Tanesco kuelezea ni nini kinaendelea. Je ndo tumerudi kule kule? Hizi taarifa kwamba tuna umeme wa kutosha ni uzushi?!