Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Mtuhumiwa mmoja pekee, Kanael Akyoo (50), ametiwa mbaroni na kikosi maalum cha kupambana na dawa za kulevya, akidaiwa kukutwa na magunia matatu na viroba tisa vya bangi nyumbani kwake.
Julai 6 mwaka huu, Rais John Magufuli aliagiza kuondolewa kazini na kushushwa vyeo kwa aliyekuwa Mkuu wa Polisi Wilaya ya Arumeru (OCD), Ofisa Usalama wa Wilaya hiyo (DSO), Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya hiyo (OC CID) na maofisa wengine wa vyombo vya ulinzi na usalama wanaohusika, baada ya kushindwa kudhibiti dawa hizo hadi Kaimu Kamishna wa Tume ya Kudhibiti Dawa za Kulevya alipokwenda wilayani huko kufanya operesheni.
Jana, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini katika Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Florence Khambi, alisema bangi hiyo ilikamatwa katika Kitongoji cha Karafia kilichoko eneo la Kisimiri Chini wilayani Arumeru.
Kwa mujibu wa Khambi, operesheni hiyo iliongozwa na Kamishna Jenerali wa DCEA, James Kaji, kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi mkoani Arusha.
Alisema kuwa katika ukaguzi wa awali kwenye maeneo ya mashamba ya kitongoji hicho walifanikiwa kukamata magunia 116 ya bangi.
Alisema pamoja hayo, pia walikamata viroba tisa vya bangi, gunia 1 la mbegu na misokoto 714 ya bangi.
Alisema kuwa katika operesheni hiyo, pia walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa mmoja Kanael Akyoo (50), mwanamke mkazi wa Karafia Kisimiri Chini akiwa na magunia matatu na viroba 9 vya bangi vikiwa vimehifadhiwa ndani ya nyumba yake.
“Juhudi za intelijensia ya taasisi hizo zilifanikisha kumkamta mtuhumiwa huyo na kwa kweli ni jambo jema, maana unapokamata kitu bila mtu inafikirisha," alisema.
Alibainisha kuwa magunia mengine 113 yalikamatwa katika nyumba zaidi ya 20 za wakazi wa eneo hilo ambapo watuhumiwa waliokuwa wakiyamiliki, walikimbia makazi yao.
Alisema kuwa mtuhumiwa Akyoo anatarajiwa kufikishwa mahakamani hivi karibuni baada ya mchakato wa upelelezi kukamilika.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro, akizungumza na Nipashe jana kuhusiana na tukio hilo, alisema kuwa kwa kushirikiana na vyombo mbalimbali vya udhibiti wa dawa za kulevya, wameendelea kupambana na biashara hiyo haramu wilayani huko na hivi karibuni walifanikiwa kukamata watu watano wakituhumiwa kujihusisha na biashara hiyo na tayari wameshafikishwa mahakamani.
Alisema kuwa jana walipanga kufanya ziara ya kikazi katika maeneo ya Kitongoji cha Karafia na vijiji vingine wilayani humo ili kutoa elimu na kubadili fikra za wananchi kuhusu kilimo cha bangi ambacho alidai wananchi wa huko wanaona ndiyo kipato cha kuendeshea maisha yao.
“Tutaambatana na wataalamu wa elimu za kilimo biashara, tuna programu ya kuelimisha kilimo cha pareto ambacho hustawi sehemu za baridi ambacho kina kipato zaidi ya kilimo na biashara haramu dawa za kulevya aina ya bangi. Kilo moja ya pareto ni Sh. 1,600 hadi 2,000.
Kwa hiyo, kwenye gunia moja ni pesa nzuri kabisa na watabadilisha maisha yao na kuepuka bangi ambayo kila siku inawakutanisha na mkono wa dola," alisema Muro.
Chanzo: Nipashe