Jembe Jembe
JF-Expert Member
- Jun 9, 2016
- 753
- 1,812
Na Joseph Ngilisho
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongela amefungua maonesho ya kimataifa ya kilimo yanayojulikana Kama ‘TANZFOOD Expo’ katika viwanja vya magereza, na kuwataka wadau wa kilimo na wafugaji kuyatumia maonesho hayo kama fursa ya kujifunza na kutangaza bidhaa zao Kimataifa.
Akiongea mara baada ya kufungua maonyesho hayo na kutembelea baadhi ya mabanda ya waoneshaji alisema mpango wa serikali ya mkoa ni kuyafanya maonesho hayo kuwa ya Kimataifa na kuleta mnyonyoro wa thamani katika sekta ya kilimo,uvuvi,uchakataji na wakulima kupata fursa ya kujifunza teknolojia mbalimbali za kisasa.
Mongela pamoja na kuwashukuru waandaaji wa maonesho hayo,alisema mpango wa mkoa Kwa kushirikiana na jumuia ya Afrika Mashariki (EAC)yenye makao yake Jijini hapa,ni kuufanya mkoa wa Arusha kuwa mji wa matukio na hivyo kuwezesha kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo ndani ya mkoa.
Mmoja ya waandaaji wa maonesho hao ambaye pia ni mkurugenzi wa Kilifair promotion,Dominic Shoo alisema lengo la maonesho ni kukuza sekta ya kilimo kwa kutoa fursa Kwa wakulima kujifunza kilimo biashara na kukutana moja Kwa moja na masoko ya Kimataifa.
"Tumeona tuandae maonesho haya mara baada ya kuona Kuna pengo katika nswkta ya kilimo kati ya wakulima na wanunuzi namna ya kuyafikia masoko Kwa faida,hivyo kupitia maonesho haya wakulima watakutana na wanunuzi wa Kimataifa"alisema Shoo.
Aliongeza kuwa katika maonesho ya siku tatu wakulima watanufaika na semina kutoka kwa wataalamu wa kilimo nchini ili kilimo chao kiwe na faida na manufaa wakulima
Naye Mkurugenzi mtendaji wa shirika la TAHA, Jacqueline Mkindi alisema sekta ya kilimo imefunguka kidunia na kutoa rai Kwa wanzania kuwekeza kwenye hiyo kwani bidhaa za Tanzania ikiwemo mbogamboga na matunda zimeonekana kuwa Lulu katika soko la dunia.
Mkindi ambaye pia ni mwenyekiti wa baraza la kilimo nchini,alisema bidhaa za Tanzania zinagombewa kwenye masoko ya Kimataifa hivyo maonyesho kama hayo ni fursa ya kujifunza zaidi ili kuendelea kuleta tija kwenye uzalishaji na usindikaji.
"Naomba niwahakikishie Watanzania hasa sisi tuliopo kwenye sekta ya kilimo fursa ni kubwa sana hasa kwenye mazao ya mbogamboga na matunda, dunia inahitaji matunda, mboga na viungo kutoka Tanzania" alisema.
Alitoa rai kwa Watanzania, taasisi binafsi na wakulima kuwekeza zaidi kwenye kilimo kwani masoko yapo Kwa kiwango cha juu Sana duniani.
Maonesho hayo yanawashirikisha waoneshaji zaidi ya 120 kutoka ndani ya Nchi na Nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki , yatafanyika Kwa siku tatu katika viwanja vya magereza kuanzia Leo Hadi jumapili yatakapofungwa rasimi.