Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
HISTORIA YA MKOA WA ARUSHA
Mkoa wa Arusha ni moja kati ya Mikoa 26 ya Tanzania Bara, wenye ukubwa wa KM za mraba 34,515.5. Kiutawala Mkoa unao Wilaya 6 na Halmashauri 7, Tarafa 23, Kata 33, Vijiji 393, Mitaa 154 na Vitongoji 1471.
Idadi ya watu kwa ongezeko la 2.7% kwa mwaka na inakadiriwa kufikia jumla ya watu wapatao 1,835,787 ambapo wanawake wakiwa sawa na 51.5% na wanaume 48.5%
Mkoa wa Arusha umepakana na Mkoa wa Manyara kwa upande wa Kusini, upande wa Mashariki umepakana na Mkoa wa Kilimanjaro, kwa upande wa Kaskazini umepakana na Nchi ya Kenya na kwa upande wa Magharibi umepakana na Mkoa wa Simiyu na Mara
Pia, soma: Orodha ya Nyuzi za Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
KUELEKEA UCHAGUZI MKUU 2025
Uchaguzi wa mwaka 2025 unatarajiwa kuwa wenye ushindani tofauti na ule uliofanyika mwaka 2020. licha ya matukio kadhaa yanayotishia demokrasia nchini vyama vya siasa vimeendelea kufanya maandalizi kuelekea uchaguzi huo ikiwemo kufanya mikutano ya hadhara katika maeneo mengi.
MAJIMBO YA KIUCHAGUZI
Katika muktadha wa kisiasa, Mkoa wa Arusha umegawanyika katika majimbo saba (7) ya uchaguzi, ambayo yana jukumu muhimu katika kuwakilisha maslahi ya wananchi katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Majimbo haya ni yafuatavyo:
- Arusha Mjini
- Longido
- Karatu
- Ngorongoro
- Arumeru Mashariki
- Arumeru Magharibi
- Monduli
MATOKEO YA UCHAGUZI WA 2020
Wabunge ambao walichaguliwa katika majimbo ya uchaguzi yanayopatikana katika mkoa wa Arusha asilimia 100% walitoka Chama cha Mapinduzi, huku uchaguzi huo ukidaiwa kutokuwa huru na haki kutokana na kukandamizwa kwa vyama vya upinzani.
Haya ni Matokeo ya idadi ya kura walizopata wagombea katika majimbo ya uchaguzi yaliyopo mkoa wa Arusha.
Katika Jimbo la Uchaguzi la Arumeru Magharibi, wagombea walikuwa John Emanuel Kivuyo wa ACT-Wazalendo, aliyepata kura 2,492, Noah Lemburis Saputu Mollel wa CCM, aliyepata kura 72,160, Ole Meiseyeki Gibson Blasius wa CHADEMA, aliyepata kura 22,743, Arafa Mohamedy Muya wa CUF, aliyepata kura 329, Mch. Laizer Loilole Wilson wa NCCR-Mageuzi, aliyepata kura 323, na Tumaini Andrea Akyoo wa UPDP, aliyepata kura 169. Mgombea aliyeshinda ni Noah Lemburis Saputu Mollel wa CCM.
Katika Jimbo la Uchaguzi la Arumeru Mashariki, wagombea walikuwa Dkt. Pallangyo John Danielson wa CCM, aliyepata kura 84,858, na Rebecca Michael Mngodo wa CHADEMA, aliyepata kura 14,688. Mgombea aliyeshinda ni Dkt. Pallangyo John Danielson.
Katika Jimbo la Uchaguzi la Arusha Mjini, wagombea walikuwa Husna Tomasi Kundi wa AAFP, aliyepata kura 831, Shayo Polycarp John wa ACT-Wazalendo, aliyepata kura 384, Zuberi Mwinyi Hamisi wa ADA-TADEA, aliyepata kura 249, Mathayo Richard Membi wa CCK, aliyepata kura 245, Gambo Mrisho Mashaka wa CCM, aliyepata kura 82,480, Lema Godbless Jonathan wa CHADEMA, aliyepata kura 46,489, Magdalena Loonjumuya Shangay wa CUF, aliyepata kura 177, Elisante Michael Mjema wa Demokrasia Makini, aliyepata kura 57, Elizabeth Geofrey Sembuche wa DP, aliyepata kura 33, Mkama Rashid Jaralya wa N.R.A, aliyepata kura 57, Heftsiba Reward Kiwelu wa NCCR-Mageuzi, aliyepata kura 77, Simon Johnson Bayo wa SAU, aliyepata kura 88, Alfred Nicolas Mollel wa UDP, aliyepata kura 66, na Happy Eliasi Sumari wa UPDP, aliyepata kura 80. Mgombea aliyeshinda ni Gambo Mrisho Mashaka wa CCM.
Katika Jimbo la Uchaguzi la Karatu, wagombea walikuwa Constantine Kanso wa ACT-Wazalendo, aliyepata kura 803, Awack Daniel Tlemai wa CCM, aliyepata kura 49,042, Cecilia Daniel Paresso wa CHADEMA, aliyepata kura 31,150, Emmanuel Patrick Qaymo wa CHAUMMA, aliyepata kura 424, Joseph Jacob Paulo wa NCCR-Mageuzi, aliyepata kura 127, na Joseph Cresent Balde wa NLD, aliyepata kura 140. Mgombea aliyeshinda ni Awack Daniel Tlemai wa CCM.
Katika Jimbo la Uchaguzi la Longido, wagombea walikuwa Steven Lemomo wa CCM, aliyepata kura 61,885, Paulina Lukas Laizer wa CHADEMA, aliyepata kura 1,037, Mkadam Kombo Mkadam wa CUF, aliyepata kura 65, na Feruziy Juma Feruziyson wa N.R.A, aliyepata kura 21. Mgombea aliyeshinda ni Steven Lemomo wa CCM.
Katika Jimbo la Uchaguzi la Monduli, wagombea walikuwa Khalfan Chogga wa ACT-Wazalendo, aliyepata kura 485, Fredrick Edward Lowassa wa CCM, aliyepata kura 72,502, Cecilain Samson Ndossi wa CHADEMA, aliyepata kura 4,637, na Adam Mohamed Kijuu wa N.R.A, aliyepata kura 145. Mgombea aliyeshinda ni Fredrick Edward Lowassa wa CCM.
Katika Jimbo la Uchaguzi la Ngorongoro, wagombea walikuwa Supeet K. Olepuruko wa ACT-Wazalendo, aliyepata kura 1,080, William Tate Olenasha wa CCM, aliyepata kura 63,536, na Jacqueline Aisaa Swai wa CHADEMA, aliyepata kura 7,983. Mgombea aliyeshinda ni William Tate Olenasha wa CCM.
YANAYOJIRI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU 2025
JANUARY
- Arusha: Wananchi wakasirika wamvaa Mbunge Gambo mkutanoni "Unatuangusha, sisi tunakufa"
- Paul Makonda: Gambo usitake umaarufu, uwe unahudhuria vikao vya maendeleo Mkoa wa Arusha
- Kuelekea 2025 - Mbunge Arumeru Magharibi azomewa msibani, asema wananchi wasitake laana kwa kumzomea kiongozi!
- Ulega katika kikao kizito na Makonda na Mrisho Gambo, akituliza hali baada ya kurushiana maneno
- Sakata la Makonda na Gambo Zitto amchana Gambo kuhudhuria vikao asifikiri kuna kupita bila kupingwa kama 2020
- Diwani Arusha: Mbunge Mrisho Gambo ni matatizo tunayotembea nayo, hafai
- Lema: Sitagombania ubunge Arusha mjini
- Arusha: Paul Makonda atoa pikipiki 20 kwa Jeshi La Polisi ili kuimarisha Ulinzi na Usalama
- Wamasai Monduli wampongeza Rais Samia kupitishwa na Chama, Wapinga madai ya fidia ya eneo la mazoezi ya Kijeshi
FEBRUARY
- Mwenezi CCM mkoa wa Arusha: Arusha tutampa kura za kishindo Rais Samia
- Mrisho Gambo: CHADEMA Wakisusa, sisi twala
- Dkt. Mpango: Nimeamua kukaa kando kwa hiari na kuwaachia wengine waendeleze gurudumu la kumsaidia Rais Samia
- Makonda: Watu waliofanikiwa kwa fedha za ushoga moto wa Mungu utawashukia. Mungu amtunze Trump!
- Mwana FA asema Gambo ana kila sababu za kuendelea kuwa Mbunge wa Arusha
- Makonda: Pesa za mafao ya ubunge tusiwape wajumbe, karibuni kuwekeza Arusha
- Arusha Mjini: Mrisho gambo azungumza na wazee kuhusu uhamasishaji wa kutoa elimu nishati safi
- Mrisho Gambo: CCM tumekaa tumesema sisi 2025 mgombea wetu ni Dkt. Samia, wewe yasiyokuhusu unapiga porojo unapoteza muda
- Wazee wataka uwakilishi Bungeni na ngazi nyingine za kimaamuzi
- Hadi wazee sasa nao wamekuwa chawa, waunga mkono 'mitano tena' kwa Rais Samia
- Mrisho Gambo: Godbless Lema aliniambia mzigo anaoupiga Rais Samia umenifanya hata hamu ya kugombea iniishe
- Ramsey: CCM Arusha Mwiko kusema mitano tena kwa mbunge na diwani
- Wananchi Arumeru Magharibi wasema mbunge wao ni mzigo, ameshindwa kutekeleza ahadi ya ujenzi wa barabara
- Arusha: CHADEMA yakutana na Mashehe na kufanya nao Mazungumzo
- Heche: CCM wanaishi kwa kuviziana hawawezi kufanya uchaguzi kama wa Chadema
- Heche amtembelea muasisi wa Chadema, Mzee Ewdin Mtei
- John Heche: CCM haitaki uchaguzi, Makalla akisema 'hatujajiandaa' aulizwe kwa nini wanaengua wagombea
- Mwenyekiti CHADEMA Kanda ya Kaskazini: Nitawashughulikia wote wasiomkubali Lissu
- Msajili wa Vyama vya Siasa ameupa Siku 7 Uongozi wa TLP kujibu madai ya ukiukwaji wa Katiba, Kanuni za Chama hicho
- Kwa hii collabo ya Meya Max na RC Makonda, Gambo hachomoki
- Mrisho Gambo hauhitajiki tena Arusha, Mwachie Paul Makonda
- Gambo Vs Makonda: Gambo asema anayetaka Ubunge Arusha aje uwanjani aone kama ngoma ya kitoto inakesha
- Gambo ajibu mapigo ya Makonda "mimi nimeenda shule"
- Arusha: Waziri mkuu awasema viongozi wanaojipanga na kugombania vyeo
- Makonda: Dalili mojawapo ya umasikini ni majungu na fitina
- Arusha: RC Makonda aiagiza TAKUKURU kumhoji Mrisho Gambo upotevu wa Tsh. Milioni 400 zilizochangwa na wadau kwa ajili ya kusaidia bodaboda
- CCM Arusha yapinga Madiwani kumpigia Debe Makonda, yatoa Onyo kali
- Polisi wilaya ya Arusha, waaswa kujipanga kusimamia uchaguzi mkuu
MARCH