Arusha: Mfanyabiashara wa madini auawa mlima wa maombi, wauwaji watuma meseji

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Mwili wa Mfanyabiashara wa madini ya ujenzi, David Mollel mkazi wa Kata ya Moivaro, umekutwa ukining’inia kwenye mti juu ya Mlima Oldonyowas, jirani na eneo linalotumika kwa maombi.

Inadaiwa Mollel mwenye umri wa kati ya miaka 50 na 55, aliuawa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia Jumanne, Oktoba Mosi, 2024 kwa kunyongwa na mkanda wa suruali. Mwili wake ulifunikwa kitambaa chekundu usoni.

Taarifa za awali zinaashiria mgogoro wa kugombea eneo la uchimbaji madini ya ujenzi aina ya moramu ni chanzo cha mauaji hayo.

Soma Pia: Njombe: Mfanyabiashara aliyevamiwa na kujeruhiwa afariki dunia

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Justine Masejo amethibitisha tukio hilo akisema uchunguzi umeanza kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usalama.
 
Taarifa za awali zinaashiria mgogoro wa kugombea eneo la uchimbaji madini ya ujenzi aina ya moramu ni chanzo cha mauaji hayo.🥺🥺🥺
Watu siku hizi wanajiulia tuu
 
Hivi ni lini watu watajifunza huwezi kukwepa kesi ya mauaji? Ni ngumu sana.

Sasa kwanini uchukue risk ubaki kuishi kwa mashaka? Sasa hivi hata hilo eneo la machimbo ya moram hawatoweza kulitumia kabla hawajadakwa, hasara kubwa.

Lakini, meseji iliyotumwa na wauwaji iko wapi ndugu mleta mada?
 
How to get away with murder,it's possible.ukiwa bright kichwani hauchi alama yeyote
 
Mke na ndugu wanagombania sehemu ya kuzika.
Mke anasema aliwambiwa ana muewe akifaa azikiwe nyumban anapoishi ndugu wanapeleka huko kwao kimbeembekuanzia kufa mpaka kuzikwa aisee

Naomba Allah wasielekee mahakaman watamchosha jama
 
Back
Top Bottom