Pre GE2025 Arusha: Paul Makonda atoa pikipiki 20 kwa Jeshi La Polisi ili kuimarisha Ulinzi na Usalama

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Wakuu,

Tunaposema kwamba CCM wameanza kampeni kabla ya muda elekezi hii ndio maana yake.

=========================================================

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Christian Makonda, leo Januari 24, 2025, amepokea pikipiki 20 zilizotolewa na Leopard Foundation kwa Jeshi la Polisi Mkoani Arusha ili kusaidia kuimarisha ulinzi na usalama.

Wakati wa hafla hiyo, Makonda amesema juhudi za wafanyabiashara kama Leopard Foundation zina mchango mkubwa katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii kupitia fursa za ajira na misaada wanayotoa kwa jamii.

Leopard Foundation, kupitia Mwenyekiti wake Mustapha Lalji, imesema msaada huo ni sehemu ya jitihada za kuunga mkono juhudi za serikali katika kuimarisha sekta ya usalama na maendeleo ya jamii.

Snapinst.app_474216257_18300732361226150_2982501061484961539_n_1080.jpg

Snapinst.app_474947026_18300732571226150_9005585861883181901_n_1080.jpg
 
CCM na polisi ni Pete na kidole. Ni hatari sana kwa majeshi kujiingiza kwenye siasa
 
jamaa ni kichwa hasa. hapa licha ya hisia zetu kisiasa lakini amelisaidia sana jeshi. ni ubunifu mkubwa sana kwa nafasi yake
 
Wakuu,

Tunaposema kwamba CCM wameanza kampeni kabla ya muda elekezi hii ndio maana yake.

=========================================================

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Christian Makonda, leo Januari 24, 2025, amepokea pikipiki 20 zilizotolewa na Leopard Foundation kwa Jeshi la Polisi Mkoani Arusha ili kusaidia kuimarisha ulinzi na usalama.

Wakati wa hafla hiyo, Makonda amesema juhudi za wafanyabiashara kama Leopard Foundation zina mchango mkubwa katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii kupitia fursa za ajira na misaada wanayotoa kwa jamii.

Leopard Foundation, kupitia Mwenyekiti wake Mustapha Lalji, imesema msaada huo ni sehemu ya jitihada za kuunga mkono juhudi za serikali katika kuimarisha sekta ya usalama na maendeleo ya jamii.

Acha upotoshaji wa kijinga, pikipiki zimetolewa na mfanyabiashara na sio Makonda.
 
Huyo mwenye sare za kijani na cheo cha kijeshi ni mwanachama wa ccm au ni askari Polisi?.
 
Polisi kaamua kabisa kuvaa nguo ya chama Cha mapinduzi na kujifanya kama sare ya jeshi.Hili jeshi linashida sana
 
1737729239194.png

Polisi siku hizi wanavaa uniform za rangi ya chama tawala? Sasa si ndio inawafanya PoliCCM kihalisi?
 
Acha upotoshaji wa kijinga, pikipiki zimetolewa na mfanyabiashara na sio Makonda.
Nilitaka kuuliza hii kitu sijui baadhi ya watanzania akili zao zikoje, pikipiki zimetolewa na mfanyabiashara kisha jitu linasema Makonda ametoa/amegawa pikipiki na wajinga wengine wanaunga mkono. Hovyo kabisa
 
Back
Top Bottom