Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Klabu ya Arusha Saccos imemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kumteua Mhe. Paul Christian Makonda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, wakisema amekuwa chachu ya maendeleo ya Mkoa huo hasa katika masuala ya kiuchumi na ustawi wa mwananchi mmoja mmoja.
Mwenyekiti wa Arusha Club Saccos ndugu Ludovick Mbasha ametoa kauli hiyo kwaniaba ya klabu hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya miaka 20 ya kuundwa kwa Klabu hiyo, akimshukuru pia Mhe. Makonda kwa kuridhia kwake kuwa Mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo yaliyifanyika Februari 28, 2025 yakiambatana na siku ya Familia kwa wanachama wao.
Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Mbasha ameeleza kuwa katika sherehe hizo za miaka 20 ya Klabu ya Arusha Saccos, Mhe. Makonda alifanikisha klabu hiyo kupata zaidi ya Shilingi Milioni 400 ambazo zilitokana na Klabu hiyo kupata wanachama wapya baada ya kuhamasishwa na Mhe. Makonda.
Klabu hiyo pia imemshukuru Mhe. Makonda kwa kujiunga na Klabu hiyo, akiungana na Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Mhe. Maximilian Iranghe ambaye amekuwa Mwanachama wa Klabu hiyo kabla hata ya kuchaguliwa kuongoza Baraza la madiwani Jiji la Arusha, wito pia ukitolewa kwa wananchi wengine kuweza kujiunga na klabu hiyo ili kunufaika na fursa mbalimbali.