Arusha shikamoooni, nimekutana na bei ajabu

Hakuna landmark?
 
Daah nenda kwa Ustaadhi hapo kwa Mrangi bara bara inayotoka Stand Ndogo upate Lishe ya maana kwa 3000 tuu Ukitaka kuku wa Kienyeji na Pilau ni 5000 wana kipimo cha kawaida na excess hiyo lumbesa inatakiwa uwe mlaji kweli...Lodge za 20,000 na 25,000 huko maeneo ya Picnic zipo za kumwaga sema mnaingia kimya kimya bila kuuliza wenyeji ndio maana mnaangua sehemu sio...
 
Ungekuwa upo vizuri mfukoni ilikuwa unapiga simu jikoni wanakuandalia Makange yako ya Kuku mzima, elfu 28 tu unapiga na ugali wako safi kabisa.

Then unashushia na Wine yako huku unasoma kitabu chako cha Novel🍷
Wine gani nzuri ndugu? Nataka kuanza kutumia kilevi
 
zipo sehemu za chini huko matejoo ngarenalo na ze like..
salimia watu!
 
Wine gani nzuri ndugu? Nataka kuanza kutumia kilevi
Inategemea unataka soft wine au zile kali kwaajili ya kulewa.

Kwa kuanza upate soft ambazo ukienda supermarket utaulizia kulingana na mfuko wako.
 
Inategemea unataka soft wine au zile kali kwaajili ya kulewa.

Kwa kuanza upate soft ambazo ukienda supermarket utaulizia kulingana na mfuko wako.
Niwekee mapendekezo hapa ndugu (soft & zenye kilevi), huko supermarket watanipiga tu. Nitauziwa zile ambazo hazina soko, hahaa
 
Niwekee mapendekezo hapa ndugu (soft & zenye kilevi), huko supermarket watanipiga tu. Nitauziwa zile ambazo hazina soko, hahaa
Jaribu Altar Wine, Dodoma wine, Imagi sweet wine au Dame Wine.

Dompo wine pia ni nzuri ukitaka kuchangamka.

Nashauri ufanye window shopping kuweza kupata machaguo mengi zaidi
 
Tafuta mume akihudumie kwa malazi na chakula.
 
Mnaongopa,Arusha haipo kama mnavyosema sehemu za bei rahisi kuliko hata mbagala dar zipo... mahali popote ili uokoe gharama ni lazima uwe na wenyeji wanaojua mitaaa.

sio unapata mwenyeji wa Arusha mitaa anayoijua yeye ni njiro na sakina... Nenda ndani huko ukutane na guest hadi za 10k per day (muhimu usingizi)

Acha luxury life ukijijua huna maisha mfukoni, una 50k halafu unatafuta lodge za wenye nazo?

ishi kwa passcode zako utaishi popote.
 
Sawa kaka
 
Arusha ya wapi hiyo, Arusha kuna chakula mpaka cha 1500, vyumba single zipo mpaka za 10,000, self ziko nyingi 15,000 tena mjini tu mitaa ya makao mapya karibu tu na stand kuu. We hata hujafika Arusha. Chakula pale stand ndogo bei 2,000 tu tena wali nyama au ugali nyama. Arusha ni wewe tu, ukijichanganya utaliwa.
 
Nipo tengeru kwenye mishe zangu ,nipo hapa bar ya road kabisa nakula mbuzi choma, inaitwa Sumni bar
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…