Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Kampeni ya Mtu ni Afya tarehe 1 machi 2025 imeendelea kutimua vumbi katika wilaya ya Monduli mkoani Arusha na kutembelea kata ya Makuyuni kujionea hali ilivyo ya utekelezaji wa afua tisa na kutoa elimu kwa wananchi.
Evance Simkoko ni Afisa Afya kutoka Wizara ya Afya taifa amesema jambo hilo haliwezi kuvumilika na ametoa maagizo kwa halmashauri kuona ni kwa namna gani wanajenga choo ndani ya siku saba.
"Kampeni ya mtu ni Afya ina afua tisa ambapo moja ya afua ni ujenzi wa vyoo na kwa masikitiko makubwa hali ya ujenzi wa vyoo katika Wilaya ya Monduli bado ni duni na hii itasababisha taifa zima tuwe na kaya ambazo hazina choo na kama wizara tunatoa maelekezo kwa halmashauri na mkoa usimamie upatikanaji wa choo hapa katika soko la Makuyuni haraka iwezekanavyo", amesema Simkoko.