Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
VIONGOZI wa dini mkoani Arusha,wameridhishwa namna Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi nchini(INEC),inavyoshirikisha makundi mbalimbali kwa kuyaelimisha na kupokea maoni ya uboreshaji wa daftari la kudumu la mpiga kura awamu ya kwanza zoezi litakaloanza Disemba 11 hadi 17 mwaka huu.
Hayo yamesemwa na Msemaji wa Taasisi ya Kidini ya Kiislamu ya Twariqa Qadiriya Razikia Jailania Tanzania,Sheikh Haruna Hussein,wakazi akizungumza na waandishi wa habari jiji Arusha kuhusu zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
Sheikh Haruna,ametumia nafasi hiyo, kuwaomba viongozi wa dini,wanasiasa na viongozi wa mila kuwahamasisha wananchi kwenda kuboresha taarifa zao kwenye daftari hilo, ili wapate fursa ya kuwachagua viongozi wao mwaka 2025 kwenye uchaguzi wa Madiwani,Wabunge na Rais.
Pia kiongozi huyo wa dini,ameiomba INEC kuendelea kutoa elimu hiyo kwa uwazi hasa katika maeneo ya vijijini ambayo yamekuwa hayafikiwi kwa urahisi na wahusika waliopewa jukumu hilo.
PIA SOMA
- LGE2024 - Zoezi la uandikishaji wa wapiga kura (INEC) halijaamasishwa sana, isipokuwa kwa viongozi wa CCM waliwaambia wanachama wao wahakikishe wanatimiza zoezi