Bushmamy
JF-Expert Member
- Aug 18, 2019
- 9,140
- 15,963
Vurugu kubwa zimetokea katika mtaa wa Engosengiu kata ya Sinoni kati ya msimamizi wa uandikishaji wa mtaa huo na wakala wa chadema na baadhi ya wananchi baada ya msimamizi huyo kutaka kumtorosha muandikishaji wa daftari bila ya kuonyesha idadi ya waliojiandikisha wakiwa na lengo la kwenda kuongeza majina feki.
Wakala huyo wa chadema amelalamika kuwa ni kawaida ya msimamizi huyo kuongeza majina mara tu aondokapo na daftari.
Baadhi ya wananchi wamesikitishwa na kitendo hicho kwa madai ya ukiukwaji wa haki za msingi na kusema kuwa ni bora wasipige kura kama hali ndo hivo.
Soma Pia: Njombe: Polisi wakamata wafuasi wa CHADEMA waliomshambulia wakala wa CCM aliyedaiwa kusambaza majina hewa
Wananchi wengi wamelalamika na kukata tamaa ya kupiga kura kwa madai ya serikali kutumia pesa nyingi katika zoezi hilo huku hujuma zikifanyika kwa maelelezo ya kuwa ni maelekezo toka juu.