Jembe Jembe
JF-Expert Member
- Jun 9, 2016
- 753
- 1,812
Wafanyakazi zaidi ya 200 wa hotel za Naura Spring na Impala za jijini Arusha wameandamana katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha wakilalamikia mwenendo mbaya wa mashauri yao ya madai yaliyopo mahakamani unaolenga kuchelewesha haki ya kulipwa Madai yao yanayofikia kiasi cha sh,milioni 700.
Wafanyakazi hao waliokuwa na mabango yenye jumbe mbalimbali walitinga ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Arusha majira ya saa Tisa alasiri wakitokea katika mahakama Kuu Kanda ya Arusha Masijala ndogo ya kazi kusikiliza shauri lao la madai ambapo wakimtuhumu mahakama hiyo kujaa Rushwa na kushindwa kuwatendea haki.
Hata hivyo baada ya kutoridhishwa na mwenendo wa shauri hilo lililopo mbele ya Jaji Mohamed Gwai ambaye aliahiridha Kesi hiyo hadi June 28 na Mei 20 mwaka.huu, wafanyabiashara hao walihamasishana na kuandamana kuelekea ofisi ya mkuu wa Mkoa wa ARUSHA.