JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Washtakiwa 20 wakiwemo raia wanne wa kigeni kutoka mataifa ya Afrika Mashariki wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha jana na kusomewa mashtaka 195 ikihusisha kesi ya kuongoza genge la uhalifu pamoja na uhujumu uchumi, matumizi ya vifaa vya kielektroniki yaani simu box kuingilia mfumo wa mawasiliano.
Katika Kesi ya kwanza Mshtakiwa Onesmo Kamolla (33) na wenzake 10 wamesomewa mashatka 75 na kesi ya pili Mshtakiwa Noel Morijoi (24) na wenzake Tisa wamefikishwa mahakamani hapo na kusomewa mashtaka 120.
Mbele ya Hakimu Mkazi Arusha, Regina Oiyer, na Wakili wa Serikali Nurat Manja amedai katika kesi ya kwanza washtakiwa wametenda kosa hilo Mei 27 hadi Oktoba 2024 eneo la Kisongo C, Longido, Arusha ambapo waliunganisha vifaa vya kielektroniki vya mawasiliano pasi na kuwa na leseni kinyume na Sheria na kusababisha mamlaka ya TCRA kukosa kodi.
Manja alidai washtakiwa hao waliendesha genge la uhalifu na kuisababishia hasara serikali na Mamlaka ya Mawasiliano TCRA ya zaidi ya shilingi milioni 40.
Katika kesi ya pili Manja alidai washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka 120 ikiwa ni pamoja na shtaka la kuongoza genge la uhalifu ambao kumeisabisha hasara serikali zaidi ya shilingi million 150 kupitia mamlaka ya mawasiliano TCRA, ikiwa ni pamoja na utakatishaji fedha zaidi ya milioni 150 za kitanzania.
Aidha Hakimu Mkazi Regina Oiyer amefafanua Mahakama hiyo haina uwezo wa kusikilisha kesi hiyo na kuahirisha shauri hilo hadi Novemba 14, mwaka huu itakapokuja kwa ajili ya kutajwa tena ambapo baadhi ya watuhumiwa walikidhi vigezo vya dhamana, na wengine wakiwemo raia wakigeni wakirejeshwa rumande kutokana na makosa yao kutokuwa na dhamana na upelelezi wa shauri hilo hauja kamilika.