Arusha: Wanafunzi Chuo cha Uhasibu kurudi chuoni kwa huruma za Wakuu wa Wilaya...


4. Mwanafunzi awe amekamilisha malipo ya ada iliyobaki wakati anatuma maombi yake 5. Mwisho wa maombi ni tarehe 16 Mei 2013. sasa kodi yako anayotumia ni ipi
 
Hapa kinachotakiwa ni kutafuta kiini cha mzozo uliopo kati ya wanafunzi wa chuo cha uhasibu na wananchi bila hivyo
watakuwa wanauwana kila kukicha.kwa mkuu wa wilaya kuna nn?ili iweje?
 
In a country led by weak leaders-everything is politicised for protection &

The political system with full of less compitent people will always use force to silence the citizen.

BUT- let patient hold as "there is no parmanent situtaion".
 
If we wont learn how to chose good leader, then we'l still experience the same surcumstance, ourself, our sons/doughers and grundsons and doughers.
 
Mulongo Magessa anazidi kukifukia kaburini chama chake cha ccm hapa arusha.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Hapa kinachotakiwa ni kutafuta kiini cha mzozo uliopo kati ya wanafunzi wa chuo cha uhasibu na wananchi bila hivyo
watakuwa wanauwana kila kukicha.kwa mkuu wa wilaya kuna nn?ili iweje?

Mkuu pia hakuna uhasama wowote kati ya wananchi na wanachuo, tukio lilotokea la mwanafunzi kuuliwa na vibaka ni tukio la ualifu kama ualifu mwingine tu ambao ungeweza kumtokea hata mwanakijiji anayepita maeneo husika kwa miguu usiku uwo.

Hichi chuo kimefungwa kwa sababu mkuu wa mkoa Mulongo Magesa amezomewa na wanachuo baada ya kushindwa ku-maintain hadhira ya maelfu ya wanachuo wenye hasira na uzuni kubwa baada ya kufiwa na mwanachuo kwa tukio la ualifu lililotokea njiro maeneo jirani ya chuo.
Ukitazama video ya tukio zima la uhasibu utaona ni jinsi gani hisia binafsi za mkuu wa mkoa zinavyozidi kuzamisha jahazi la CCM.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Mkuu wa mkoa alizomewa kanisani siku ya mabomu je amewachukulia hatua gani waumini, alizomewa pia hospitali ya mt Meru siku hiyo hiyo je amewachukulia hatua gani au hao hawatibiwi kwa pesa zako, je wanaotakiwa kuandika barua ni wanafunzi wanao lipiwa na seriakali au unawashwa na masaburi tu..huo uhuni wa ccm una mwisho na mnajijengea chuki zaidi kwa vijana na hii ni shangwe kwa chadema na vyama vingine makini vya upinzani...
 

Mpuuz mwingine huyu
 
Last edited by a moderator:
Katika Gazeti la Mwananchi la leo kuna Tangazo linalowahusu wale wanafunzi waliofukuzwa kutoka Chuo Cha Uhasibu Arusha kutokana na zengwe la Mkuu wa Mkoa huo, Magesa Mulongo. Tangazo hilo linasomeka hivi:

Kutokana na Chuo kufungwa, Baraza la Uongozi wa Chuo katika kikao chake cha dharula cha tarehe 03 Mei 2013 kimeagiza wanafunzi wote kuanzia ngazi ya Cheti mpaka Stashahada ya Uzamili kuzingatia yafuatayo:

1. Kila mwanafunzi anatakiwa kutuma maombi mapya ya kujiunga na Chuo
2. Barua ya maombi hayo ipitishwe kwa Mkuu wa Wilaya anapoishi mwanafunzi. Kwa mwanafunzi wa Stashahada ya Uzamili ya Uhasibu barua yake ya maombi ipitie kwa Mhasibu Mkuu wa Serikali
3. Katika maombi hayo mwanafunzi anaagizwa kueleza namna alivyoshiriki katika vurugu za tarehe 24 Aprili 2013
4. Mwanafunzi awe amekamilisha malipo ya ada iliyobaki wakati anatuma maombi yake
5. Mwisho wa maombi ni tarehe 16 Mei 2013

Swali: Je, utaratibu huo umewekwa kulenga mtu au watu wowote hapo Chuoni? Sababu ilisababisha vurugu iko wazi, ambayo ni Serikali kutojali kilio cha wanafunzi na kupelekea mwanachuo mwenzao kuuawa kwa kuchomwa kisu. Sababu ya pili ni kiburi cha Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo.
 

Kiongozi!

naona unazidi kujifurahisha kwa hoja zako zisizo na mashiko. Simezunguka sana duniani lakini sijawahi ona mahali popote ambapo upo mfungamano wa Learning Institutions na wakuu wa Mikoa au ukipenda Governors.

Learning Institutions are an INDEPENDENT organs. Ambazo zinakuwa na Directors wao ambao ndio wenye kutoa maamuzi kuhusiana na masuala yanayo zihusu taasisis zao. Labda nikuulize kama umewahi kuona mTanzania yeyote anaomba kujiunga na Overseas Learning Institution na katika application form zake ukakuta kipengele ambacho kinamuelekeza kupitishia form yake kwa Governor huko anako taka kusoma?

Tatizo ni kwamba kila kitu Tanzania kimeingizwa kwenye siasa kwa hofu ya watawala kupokwa ulaji. Mnafikiri kushabikia haya ndio kuta waweka salama kwenye himaya zenu/zao?

Sasa hivi kila siku kasi ya kila kitu kupitia kwa Ma-DC na Ma-RC ndio inaongezeka huku wakijiona ndio miungu watu wa nchi hii. Upende usipende, ni suala la muda tu. Na huwa historia ni mwalimu mzuri. Ngoja tuone.
 
upo mzozo nz kzmz hutaki kuamini rejea mauwaji ya kijana kubaka/mwananchi alieuwawa miaka ya 2009/2010 hapa kuna kulipiza kisasi.kwa nn wasirudi nyuma na kukumbuka tukio hilo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…