KERO Arusha: Wananchi Sovoyo walalamikia kukosa maji kwa miezi mitatu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Wananchi wa Kitongoji cha Sovoyo, Kijiji cha Ngorbob, Kata ya Mateves jijini Arusha, wamelalamikia kukosa huduma ya maji kwa zaidi ya miezi mitatu, licha ya mabomba ya maji kuwa yameunganishwa hadi ndani ya nyumba zao.

Wananchi hao wamesema hali hiyo imekuwa changamoto kubwa kwa familia zao, hasa kwa kuwa wana mahitaji mbalimbali ya ndani yanayotegemea huduma ya maji. Wamesema kinachowashangaza zaidi ni kuendelea kupokea bili za maji kila mwezi licha ya kutopata huduma hiyo kwa kipindi hicho.

Soma Pia: Wananchi walalamikia mradi wa maji wa shilingi bilioni 2.5 kutoleta manufaa Losikito, Arusha DC

Baada ya malalamiko hayo, wataalamu kutoka idara ya maji walifika katika eneo hilo na kubaini kuwa kuna bomba lililoharibika ambalo limesababisha huduma kukatika. Wameanza kufanya matengenezo na kueleza kuwa maji yanatarajiwa kurejea leo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…