Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Wananchi kutoka kata za Kisongo, Mateves na Musa wamegomea maelezo ya Mkuu wa Kituo cha Polisi Kisongo kufuatia malalamiko ya kuongezeka kwa vitendo vya uhalifu katika maeneo yao.
Wananchi hao walidai kuwa baadhi ya watuhumiwa wanaokamatwa na kupelekwa katika kituo hicho huachiwa bila maelezo ya kuridhisha, huku wengine wakidaiwa kuachiwa baada ya kutoa rushwa.
Akizungumza katika mkutano huo, Mkuu wa Kituo alijaribu kutoa elimu na ufafanuzi kuhusu utendaji wa jeshi la polisi, lakini wananchi hawakuridhishwa na maelezo hayo.
Kutokana na hali hiyo, baadhi ya wananchi walianza kuondoka eneo la mkutano kabla ya mkutano huo kuvunjika rasmi.