Chachu Ombara
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 6,067
- 10,938
Jeshi la Polisi mkoani Arusha linamshikilia mfanyabiashara Abdi Hamis (27) mkazi wa Ngarenaro na Ally Said (25) dereva na mkazi wa Olasiti baada ya kukamatwa wakisafirisha dawa za kulevya aina ya Heroin gramu 70.77 kwa kutumia gari Na. T 949 DQA lenye tela Na. T. 253 CXR.
Kamanda wa Polisi wa mkoa huo Justine Masejo amesema uchunguzi wa awali wa Jeshi la Polisi umebaini kuwa watuhumiwa hao wamekuwa wakijihusisha na biashara hiyo haramu kwa muda mrefu na walikuwa wakifuatiliwa.
Aidha jeshi bado linaendelea kuwashikilia watuhumiwa hao pamoja na gari hilo mpaka upelelezi utakapokamilika.