Arusha: Yaliyojiri mapokezi ya Godbless Lema, Adai VICOBA ni umasikini, Mama lishe ni utumwa, Samia asitukanwe, Mbowe ampa kazi ya Katiba Mpya

Kutengeneza ajira ni process, it takes a lot. Kuanzia resources za fedha na watu makini, sera nzuri na miundombinu ya kutosha.

Serikali ya CCM kwa bahati mbaya kwa miaka 60+ wameshindwa kufanya hayo, yoyote atakayepata nafasi hiyo, atakuwa na mda mfupi sana wa kutokomeza ajira za namna hiyo, sio bidaboda tu, hata kupanga nyanya na karoti kando ya mabarabara ni umasikini mkubwa sana, ni basi tu tumeshakuwa taifa lililolaanika.
 
Godbless Lema amewatukana vijana Waliojiajiri kwa kuwaambia wanafanya kazi za laana, hii suala limeacha simanzi kwa vijana wengi sana.

Jana nilikua Arusha nimezunguka sehemu mbalimbali kuona wamepokeaje kauli hii yenye dharau kubwa sana. Hakika walio wengi wanajuta kwa Nini walienda Kumpokea Lema.

Serikali inapambana usiku na mchana ili vijana wapate ajira na wajiajiri alafu leo lema anakuja kuwatukana?

Lema anapaswa kuomba radhi kwa kauli hii. Yeye kwa kuwa anakula na kulala bure kule canada basi anataka watu wote waishi hivyo kitu ambacho hakiwezekani. Imeandikwa kwenye vitabu takatifu kuwa mwanaume atakula kwa jasho, wewe inakuaje unakula bure alafu unaleta dharau kwa wanaokula kwa jasho?

Lema anapaswa kuomba radhi mara moja kwa kauli hii.
 
Watanzania wengi wakiambiwa ukweli wanaona wanatukanwa.

Unaweza kuwakuta watu wapo karibu na choo, pananuka mavi, ukawaambia hapa mlipokaa pananuka mavi.

Wengi wao (sio wote) badala ya kuchukua maneno yako na kuyafanyia kazi, watalalamika umewatukana.
 
Kwani cha ajabu ni nini hapo??
 
Lema yeye anafanya kazi gani huko Canada? Angeeleza kazi yake kwanza ndio azungumzie za wengine. Sio wote wanapenda kulelewa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…