Arusha: Yaliyojiri mapokezi ya Godbless Lema, Adai VICOBA ni umasikini, Mama lishe ni utumwa, Samia asitukanwe, Mbowe ampa kazi ya Katiba Mpya

Baada ya kutua jana akitokea uhamishoni Canada alipokimbilia kwa takribani miaka 2, mwanasiasa machachari na maarufu aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema alipokelewa kwa shangwe kubwa na wafuasi wake na tayari ameibua mijadala ambayo ilikosekana kwa muda mrefu sana.

Mijadala hiyo ni pamoja na uhai wa upinzani kutokana na ukubwa wa umati wa wafuasi wake , mahusiano ya serikali na upinzani ikizingatiwa kufika kwake uwanja wa ndege kuliingiliana na msafara wa Rais bila matatizo yoyote, aina ya hotuba aliyotoa ambayo sasa ameibua mjadala mwingine mkubwa kuhusu aina ya ajira ya bodaboda ambayo kwa masikitiko makubwa imekuwa kimbilio kwa vijana wengi taifa hilo hata wale ambao ni wasomi.

Haya yote ni mambo mazuri sana yaliyokosekana kwa kipindi fulani, yanapaswa kuendelea na kushamiri zaidi kutoka kwa wanasiasa kama tunataka nchi nzuri yenye fursa sawa kwa wote na yenye demokrasia imara. Kufika kwa Lema ni mwamko zaidi na afya kwa taifa letu.
 
Mama anajiwekea Legacy nzuri. Muda wake ukishpita atakuwa anaishi maisha ya amani sana. Hatasemwa vibaya kama mwenzake. Mungu akubariki mama Samia.
 
Kweli kuna wavivu wa kufikiri na kuitafakari. Aliyoyasema Lema si kuwa kazi Ile ni "laana" tu, Bali alitoa na sababu za kazi Ile kuwa laana na kupendekeza njia mbadala. Hebu tuache propaganda za kuwahadaa wenye uelewa mdogo ili waendelee kuteseka kwa manufaa ya werevu wachache wanaowatumia kwa manufaa yao. Tunaangamia kwa kukosa maarifa; tunaelimishwa lakini hatuelimiki!
 
Andiko bora kabisa.....
 
Ulitaka watu wafanye kazi rahisi? Vipi wale wanaobonda kokoto? Wanaovua? Madereva wa masafa marefu? Hizo zote ni kazi ngumu kwa hiyo unataka watu waache?
Lazima kuwa na mawazo ya kimaendeleo. Maendeleo ni mabadiliko kutoka katika hali duni kwenda kwenye bora zaidi. Ili utoke katika hali hiyo ni lazima uelewe ipi ni duni na nyingine bora halafu uchukue hatua kuondoka kuelekea bora zaidi. Sasa, kama hujui na kukubali kuwa upo duni utapata vipi maendeleo?
 
Mbona naniii Tito yupo siku nyingi saana
 
Sasa changia lolote kwenye hili....kama unalo lakini otherwise tulia tusikie maoni ya wengine...hiyo ndio busara
 
Anavuna alichopanda
 
Kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…