Arusha: Yaliyojiri mapokezi ya Godbless Lema, Adai VICOBA ni umasikini, Mama lishe ni utumwa, Samia asitukanwe, Mbowe ampa kazi ya Katiba Mpya

Usijali hata yeye ataondoka soon kama tundu lisu, wote wawili wanamtumikia Bwana moja na wamekuja/letwa kwa mission maalumu akimaliza atasepa zake kwani unamsikia tundu lisu tena? Si na yeye alikuwa hivyo hivyo alivyoletwa kukejeli watu ambao wanataabika kila siku kwa gharama za maisha kupanda, watoto wanamaliza Shule wanafeli wote wazazi hawajui wafanye nini no one is held accountable for anything, watu wanataabika na hawajui waangalie wapi, uhalifu kila mahali panya road wanavamia watu, lkn lema na tundu lisu wanaleta kejeli anyway labda wao ni Superhuman, time will tell.

Pure evil!
 
Baada ya lema kurudi ametoa matamko mengi kuhusu makundi mbalimbali yakiwemo ya wajasiriamali. Alianza na bodaboda, akaja watumishi wa Mungu, akaja kwa wamama wa vicoba na Sasa amewafikia mama lishe.

Lema anasema mama lishe ni kazi ya kitumwa, huwezi kuwa mama lishe ukatoboa maisha Wala kusomesha kwa kazi hiyo. Sijui hadi Sasa lengo la lema kushambulia hawa watu ni nini. Wapo mama lishe wengi tu wamesomesha Watoto wao hadi vyuo vikuu.

Lema anafikiri kwa kuwa yeye ameweza kuishi bure Canada basi kila mtu anaweza hivyo. Lema amekuwa na kiburi na dharau kubwa sana kwa hawa wajasiriamali wadogo.

Mama lishe poleni, endeleeni na kupambana kesho yenu ni nzuri. Dharau na majivuno ya lema yana mwisho wake.

 
Asilimia 80% ya mafanikio kwenye biashara humtegemea mjasiriamali na hiyo 20% ni yanayomzunguka lakini hili linahitaji mjadala wa kitaifa kwasababu hii aslimia ishiirini inanguvu sana hata kuua biashara endapo jamii itaendelea kukaa kimya Lema anajaribu kuwaamsha ubongo (The entrepreneur and his environments well define as business environmental factors, whereas the major environmental factors are: political decisions, National economy and social development strategies of an existing government, social factors and Technology advancement) we have to include uncertainty and the unexpected around us
 
Lema:haya matamko yako mbona yamezidi sasa umeanza kuwatukana na wapiga kura wako tena,
Unatakiwa utulize kichwa sasa kama hauna shida na kura za watu wa Arusha unarudi kutafuta nini?
Lema kasema mwenyewe hana shida na kura zenu watu wa arusha maana hata msipomchagua anarudi Arusha iliko familia yake kuendelea kusimamia biashara zake huko.
Lema kasema hata asipochaguliwa kamwe hawezi kuona shida maana anajiweza sana kuliko mburula wote wa Arusha,
 
Maisha sio siasa mzee, hio serikali unayotegemea kulumbana nayo haitatoa majibu within two or three days. How would you survive kutegemea kui pressure serikali isiojali maslahi ya raia? For how long after all hatuna vision za kitaifa kila mwanasiasa atakayepewa uongozi anajifanyia anavyoona yeye ni sawa kwake.
 
Nimemsikiliza Lema tokea ile siku ameridi. Ukweli ni kuwa amekuwa akisema ukweli mchungu kwa raia kwakuwa sisi raia hatujielewi, ndio maana alituita sisi ni maskini (ni kweli).

Huwa inakera mtu kijaribu kuwafungua watu akili lakini watu wenyewe wapo tu kama kondoo waliopigwa jua kali vichwa chini mda wote.

So lazima atuchane kweli ili akili zikae sawa. Unafikiri yeye ana chakupoteza asipochaguliwa kuwa mbunge? Unafikiri maisha yake yatakuwa yamefika mwisho?

Tuwe tunaelewa kuwa mtu anaeamua kuwapigania watu na kuona anaowapigania wanakuwa mazuzu lazima awaambie ukweli.

Siku zote ukweli unauma ila ndio hivyo. Lema yupo sahihi.
 
Akikaa hyo kumi atasema hata wazazi waliomzaa wame fake tu lakn yy anashea baba na mama mmoja na Drake au j.bieber
 
Limbukeni la Canada linachafua chama...
Licha ya Mbowe kuwa tajiri mara kumi au ishirini ya Lema hawezi tukana wananchi masikini namna hii...

Yaani huko Canada kumemfanya atukane kila kitu Tanzania
Halafu atakuja omba Kura Kwa bodaboda na Wana vicoba??
 

Kabisa wana arusha wamepewa ukweli wao
 
Vikoba vinaleteleza wake za watu KUBANDULIWA VIZIBO VYA KISAMVU ili kilipa marejesho.
 
Nikweli tumefika hapa tulipo kwasababu ya wanasiasa hatuna vision za kitaifa zenye muelekeo chanya ambazo hazitakiwi zechezewe na wanasiasa , (visionary set not to be tempered by any political leader)
 
Mimi ni mfanyabiashara wa Bodaboda na kiukweli naungana na lema,hii si biashara bali ni laana,ninaifanya tu kwasababu sina cha kufanya ila ningekuwa nina uhakika wa kazi wala nisingehangaika na hii laana
 
Vikoba vinaleteleza wake za watu KUBANDULIWA VIZIBO VYA KISAMVU ili kilipa marejesho.
Hahahahah nilimwambia bibie hio biashara ya kufanya vikoba kipindi hajapata kazi ya maana nikamwambia siitaki!

Alikuwa ananisumbua sana na hayo marejesho. Maana mostly alikuwa hana hela. Nikamwambia iwe mwanzo na mwisho
 
KATIBU MKUU CCM akiwa ziarani SINGIDA Amesema Wote wenye DEGREE na hawana AJIRA waende VETA Vipi hapo unasemaje AMEWASIFU?
 
Mimi ni mfanyabiashara wa Bodaboda na kiukweli naungana na lema,hii si biashara bali ni laana,ninaifanya tu kwasababu sina cha kufanya ila ningekuwa nina uhakika wa kazi wala nisingehangaika na hii laana
Lema anawaambia mnafukuza upepo, miaka 50 hamtoboi. Eti mnakusanywa boda 100 mpewe mtaji wa million 5 wenye figusu na masharti kibao.

Huu ujinga unatakiwa uishe.
 
Nilimsikia ''johnthe baptist'
' akidai kuwa mwanasiasa anaongea jambo lolote,mahali popote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…