Arusha: Yaliyojiri mapokezi ya Godbless Lema, Adai VICOBA ni umasikini, Mama lishe ni utumwa, Samia asitukanwe, Mbowe ampa kazi ya Katiba Mpya

Kauli za Lema za Bodaboda ni kazi ya laana na Vicoba ni kudumisha umasikini ni kauli thabiti kwa watu wanaotaka kutibu tatizo permanently.

Tujiulize katika bodaboda 100 ni wangapi ufanya maisha bora kwa familia zao kama ambavyo tumeahidiwa kwenye kampeni za tangu 2010.

Kwa nini bodaboda huweI kukata bima kubwa, kwa maana endapo changamoto yoyote ikitokea itaweza kuku-cover?

Pia kwenye suala la VICOBA dhima kubwa ni kukopeshana na kudhaminiana. Endapo tungekuwa na uchumi mzuri basi mifumo yetu ya kifedha ingekuwa inafikika kirahisi, riba zingekuwa hata ni single digit.

Lakini kwa kuwa umasikini umekithiri nchini ndio sababu Mpesa inaonekana kama bank acvount, na vicoba vinarahisishwa kwani ndio njia pekee ya wao kula kirahisi.

Kuna wakati watawala wanaamua kuwapa uhuru, mkajihisi nyie ni pamoja nao ili msiwape shida kula keki ya taifa.

Tusimame kwenye kutatua matatizo kiujumla na tupate suluhu yenye kurithiwa na kizazi kijacho.
 
Unaposema boda boda ni kazi ya laana, kusajili laini ni kazi ya kipuuzi hutaki mwanao umuone anaifanya utamfukuza kwako, vikoba ni laana sijui hutaki mkeo ajihusishe navyo kabisa.

From a standing point wewe ni mkimbizi wa kisiasa umebebwa huko Canada for over a year. Umepata PR na familia yako na privileges nyingi huko. Umeyaona maisha kwa utofauti hilo hatukatai. Najua kwa sasa wewe watoto wako wanaweza wakaishi huko Canada for whatever reasons, huko ada hazilipwi ni serikali kila kitu. Mzazi kazi yako ni kulipa kodi ya nyumba na utilities tu.

Viwanda na Private companies ziko kibao kiasi kwamba ishu ya kupata cha kufanya wakimaliza vyuo ni wao kuamua tu kukaa kwenye corporate sphere, kwenda kuuza migahawa, kukwangua mabarafu na kutawaza wazee.Maybe sio kazi za hovyo atleast kwa uchumi wa Canada maana hata wazungu wenyewe wa huko hawazitaki.

That being said, wewe unapata wapi guts za kusema kuwa Watanzania wanafanya kazi za laana esp. Boda boda, wasajili line na wauza mboga wanaocheza vikoba? Okay, hizo kazi ni za laana atleast kwa fikra zako lakini ushajiuliza kuna ugumu kiasi gani kwa hapa Tanzania when it comes to making ends meet?

Sidhani kama una idea kwamba graduate aliyemaliza chuo anaetoka familia hohehae anapitia ugumu kiasi gani na fedhea ilioje pale anapokosa ajira na hana mtaji! Usicheze na maisha ya watu kabisa, huna ajira una mke na mtoto huna chanzo cha pesa unafikiria kitakachofuata nini?

Utakaa chini unaangalia familia iangamie? Boda boda ndio quick fix ya maisha yetu ya dhiki walau familia zile na maisha yaende, vikoba ndio quick fix ya mikopo ya benki bila masharti magumu.

Toa solution watu wafanye nini baada ya kuachana na hizo kazi za laana. Sio unaropoka hovyo tu bila kuwa na substance. Tanzania sio Canada watu wanakolipwa dollar 15-20 kwa kazi ya saa 1. Huku unapigishwa mzigo masaa 12 unalipwa elfu 4 na hamna kitu utaongea.
 
Biashara ya magari ila sijui kama imesajiliwa. Anaingiza mamilioni ya pesa ndio maana anadharau bodaboda.
 
Lazima kama Nchi tuhakikishe vijana wanapata ajira za viwandani au mashambani , kule Kyela siku za nyuma kidogo kulikuwa na vijana waliokuwa wakifanya biashara ya kusafirisha mizigo mizito kwa baiskeli , walijulikana kwa jina la NJEMUKE ( kwa kiswahili ni kama kuchemka au kutobweteka )

Hawa walitumia baiskeli ya Phoenex , sijui ilitengenezwa wapi , walibeba mizigo mizito sana huku wakiendesha baiskeli hizi , lakini baadaye wakaanza kupukutika kwa maradhi ya kifua hadi tukaaanza kuwapa elimu kwamba ni bora waingie kwenye kilimo .

Kwahiyo watu waweza kuwa wanafanya jambo linaloonekana linawasaidia lakini kumbe nyuma yake kuna madhara makubwa
 
Kauli za Lema za Bodaboda ni kazi ya laana na Vicoba ni kudumisha umasikini ni kauli thabiti kwa watu wanaotaka kutibu tatizo permanently.

Tujiulize katika bodaboda 100 ni wangapi ufanya maisha bora kwa familia zao kama ambavyo tumeahidiwa kwenye kampeni za tangu 2010.

Kwa nini bodaboda huweI kukata bima kubwa, kwa maana endapo changamoto yoyote ikitokea itaweza kuku-cover?

Pia kwenye suala la VICOBA dhima kubwa ni kukopeshana na kudhaminiana. Endapo tungekuwa na uchumi mzuri basi mifumo yetu ya kifedha ingekuwa inafikika kirahisi, riba zingekuwa hata ni single digit.

Lakini kwa kuwa umasikini umekithiri nchini ndio sababu Mpesa inaonekana kama bank acvount, na vicoba vinarahisishwa kwani ndio njia pekee ya wao kula kirahisi.

Kuna wakati watawala wanaamua kuwapa uhuru, mkajihisi nyie ni pamoja nao ili msiwape shida kula keki ya taifa.

Tusimame kwenye kutatua matatizo kiujumla na tupate suluhu yenye kurithiwa na kizazi z.
 
Unamkuta binti mzuri wa umri kati ya 18 -22. Amepigwa jula kali la mchana kisawasawa! Mida ya saa nane mchana mdomo umemkaukaa kwa kiu na muonekano anaonekana dhahili hajatia kitu tumboni, yupo anakualika usajili laini.
Unamjibu laini unazo tayari umeshasajili, kinyonge anaendelea na safari.

Inaniumizaga sana moyo na kuniumiza kiakili hasa ukizingatia nami nna vijana na binti ambao kuna leo na kesho hata baada ya kuwapa elimu stahiki wanaweza kuishia hukuhuku kuteseka juani.

Mimi naona badala ya mzigo wote kuitupia serikali inabidi na sisi wazazi tujitahidi sana kuwatengenezea watoto wetu ile hali ya kuwawezesha wajimudu kibiashara au kiufundi.

Mfano ni wenzetu wafanyabiashara wa kihindi.

Lakini sometimes wazazi tunakufa mapema kabla vizazi vyetu havijajitegemea unawaacha bila muelekeo nao wanaishia hukuhuku, hapo sasa ndio kuna umuhimu wa serikali kutengeneza mifumo rafiki ya kiajira.


Aaagh! Maisha nowdays yanaumiza sana kichwa! Hasa kwa kuangalia future za watoto wetu
 
Boda boda ni ajira atleast by CCM point of view ila mi naitazama kama temporary solution. Wanaofanya hio kazi kwa mahesabu wanafanikiwa ku venture kwenye vitu vyengine vikubwa.

Ila kwa mtu ambaye anaona kwake ndio maisha basi hafiki popote pale.
 
Namuona mjinga kuishi kwake Canada ule ushamba wake umemjaa sana, ame depreciate badala ya kuongezeka thamani, I think he lack knowledge addition from a wider spectrum and he has had multidisciplinary global and glocal malnutrition knowledge wise.
Watakuwa washamu afandelize, sidhani kama. Marinda yake yako tight
 
Unahoji kitoto sana
 
Kama ana hoja hizo alete na suluhisho pia
Hao vijana wengi hawana elimu ila akili wanazo za kujitafutia ajira hata kama wameangukia sehemu hizo kwa kuona inawapa mlo wa siku ila wengi ni hand to mouth

Mawazo yapo mengi kama kutoa mafunzo ya bure kwa wenye uwezo huko VETA na serikali iwalipie 100%

Na hizo hela serikali itafute sehemu ya kuzipata hata kupandisha road tax kwa magari au kuwe na congestion charges kuingia mjini kabisa kwa magari, ili hela zitazopatikana vijana wakasomee bure na kujifunza taaluma zozote kama ufundi magari, electrician, builders nk

Tukitaka vijana waondokane na haya lazima kutoa mafunzo bure kwa mda na hata vijana milion moja

Hili linawezekana badala ya kuwatukana na kuwasimanga

Yeye kawa mkimbizi Canada na kuna watu wamewaambia watoto wao ukiwa mkimbizi usinijue tena
Je analijua hilo kuwa mkimbizi nayo ni kama laana kwa wengine?
 
Kwa akili za huyu jamaa bora angebakia huko Canada kuliko aibu aliokuja kujitia hii. Ni mshamba kuliko hata Magufuli waliokuwa wanamuogopa na kumkimbia.
 
Unahitaji akili gani kufanya kazi ya bodaboda au kusajili laini??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…