Arusha: Yaliyojiri mapokezi ya Godbless Lema, Adai VICOBA ni umasikini, Mama lishe ni utumwa, Samia asitukanwe, Mbowe ampa kazi ya Katiba Mpya

Watanzania wengi ni wepesi kutafuta matusi na kejeli kuliko kuchangia hoja yenyewe. Kama Tanzania ingekuwa inatumia viwango vya takwimu na kutoa takwimu halisi za idadi ya ajali, vilema na idadi ya vifo vilivyosababishwa na bodaboda tangu usafiri wa bodaboda kurasmishwa kuwa biashara bila kujali kuwa polisi wana uwezo kuwasimamia kutii sheria za barabarani, ungeelewa kwa nini nchi zenye uongozi unaojitambua zimepiga marufuku biashara hii! Tunatumia hisia za kisiasa na kipato kipya bila madhara yake halisi katika jamii. Vizazi vijavyo kama vitakuwa vimezindukana kwenye usingizi pono wa kizazi hiki, watataka kufukua makaburi kupima wastani wa uzito au ukubwa wa ubongo wetu kama ulikuwa pungufu au ulikuwa na mapungufu gani hasa kuweza kuruhusu ghasia ya aina hii! Vipeperushi kwenye nchi zingine vimeandikwa kuwa na hadhari ya bodaboda, siyo simba kwenye mbuga za wanyama, ukitembelea Tanzania.
 
China wanatengeneza bodaboda lakini hakuna bodaboda, bodaboda sio Kazi ni kupoteza nguvu Kazi ya taifa.
Niambie bodaboda mwenye nyumba au gari
 
Na watoto wake wakikuwa wakawa na tabia chafu Canada watakuja kumlaani kwa kuwapeleka Ukimbizini
Karma mbaya sana

Tumuombe Mungu sana

Yeye kachagua kuwalipua wanae na mke wake na yeye kama mkimbizi ila sisi hatusemi kuwa ni laana bali ni maisha aliyochagua

Hakuna anaejua kesho tuishi kwa adabu kwenye huu mgongo wa ardhi
 
Laana ya mama yake, kuna mtu ninamfahamu anasomesha na kulea familia kwa usafiri huo huo, ajali nyingi ni wendawazimu wa wahusika.. padri akibaka hatufungi kanisa… hana adabu na ni limbukeni wa maisha, miaka miwili tu Canada anajufanya amesahau bodaboda…RIP Mr. ebbo
 
Wazee wa nyomi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…