Arusha: Yaliyojiri mapokezi ya Godbless Lema, Adai VICOBA ni umasikini, Mama lishe ni utumwa, Samia asitukanwe, Mbowe ampa kazi ya Katiba Mpya

Arusha: Yaliyojiri mapokezi ya Godbless Lema, Adai VICOBA ni umasikini, Mama lishe ni utumwa, Samia asitukanwe, Mbowe ampa kazi ya Katiba Mpya

Lema anazungumza ukweli kwenye jamii ambayo ukweli huo ni dhihaka na kejeli. Je ana suluhisho la kweli kwa anaosema wako kwenye shughuli za kimasikini? Ukweli wa Lema ndio mtazamo wa halisi wa watu wote wenye madaraka, utajiri au vipato vya kuridhisha, lakini uhalisia ni kinyume chake kabisa.
Kuvaa baibui unaizungumziaje? Maana amesema Amewahi kuvaa baibui
Au ndio mambo ya lgbt
 
Kabisa mkuu; Inaonekana yupo out of touch na reality on the ground. Akalishwe chini akumbushwe hii ni Tanzania siyo Canada.

CHADEMA wakicheka naye wataumia. Anatafuta ugomvi na kila mtu mara Geo Davis mara Gambo mara Watu wa mererani...ya nini yote hayo?

Kuna jinsi ya kuwakilisha maoni bila kukwaruzana na watu. Lema inaonekana amesahau hilo
johnthebaptist
Yoda
 
nchi ambayo haina Sera yapamoja kila anaeingia madarakani anafanya la kwake ningumu mno,mnoo,mnooo,mnoooo nasema Tena mnooooooooooo kwawananchi wake kufanikiwa.

nchi ingekuwa nachama kimoja tuu tukakaa tunaongea lugha moja😕😕yani ingekuwa nisuala la miaka 10-20 tuko sehemu nyingine kabisa

coz hatutakuwa na mivutano mikubwa ya kisiasa tunaenda na mikataba tuu.ukizingua unatolewa anawekwa mwingine.

sisi tunaendekeza ujinga wa vyama vingi hatujui kuwa ndio mchawi wetu wa maendeleo
 
Sasa Lema anataka tuwe majambazi kama yeye?Atupe basi kazi mbadala,si anatuambia mama lishe kazi ya kitumwa na hatupi wazo la njia mbadala. Anafikiri tumependa kuwa mama lishe ?
 
Vikoba havina msaada,

Ni hela yako inakatwa sijui, akiba sijui nini, wa kufaidi ni wachache.

Vikoba lazima mgombane mpaka mtishiane kurogana.

Kosa la Lema anasema ila hatoi option B, bila vikoba au bodaboda watu wapateje hela?
Akili kubwaz
 
Amekuja na staili tofauti na ya Lissu
Huyu hamtukani Marehemu direct bali anapiga aliokuwa anawatetea kila siku na kuwasema kuwa hawa ndio wapiga kura wangu


Lema waache kama inakuuma waseme na waliokuwa wanapiga deki barabara kuwa nao walikuwa matahira
Hizi kauli za kisomi na zilizofanyiwa tafiti sana za Chadema na viongozi wake zimesaidia sana ma mbumbumbu mnaibuka Kwa Kasi mkidhani mnawamaliza kina Lema kumbe ndio mnawapa nafasi waeleweke viziri zaidi.
 
Uyu ni wakupigwa Shaba
Mpige Shaba mama yako kama hilo ni jambo zuri.
CCM imeozesha brain [emoji3447] zenu kiasi mkiambiwa la kweli mnaona matusi, ila wakiwaremba remba kuwa hizo ni ajira mnaona hao ndio watu wakati kumbe wanawadharau.
Kisha wanajifanya kujumuika nanyi Kim chongo kicheko kama yote.View attachment 2536773
JamiiForums520026435.jpg
 
Sasa Lema anataka tuwe majambazi kama yeye?Atupe basi kazi mbadala,si anatuambia mama lishe kazi ya kitumwa na hatupi wazo la njia mbadala. Anafikiri tumependa kuwa mama lishe ?
Umemsikiliza mpaka mwisho au unafuata hayo ya mihemko ya kuchukua sentensi moja na kuisambaza?
Ufafanuzi ni mwingi sana basi watu sio wafuatiliaji.
Halafu sio vizuri kumuita mtu jambazi wakati huna ushahidi bali ni maneno ya vijiwe vya CCM ndio vinavyo tunga maneno.
Ukiona mtu anakuenezea kuwa wewe ni kahaba wakati sio kweli how will you feel?
Uungwana ni jambo la heri, tunamjua Lema vizuri na tusiwatukane watu wa Arusha wanaomwamini kuwa wanachagua jambazi.
 
Back
Top Bottom