As a loving and Life Experienced Parent, Would you.................?

Hivi utakubali binti yako aolewe halafu wewe ndo uwe mlezi wa familia tarajiwa....kwamba wakiumwa waje kwako??? uwape na chakula?? Damn it.....:A S angry::mad2::doh:...povu....

Mapenzi yana macho aisee...
Salama mjukuu??? I think me missing wewe....
 
Ukweli unauma lakini mimi najaribu kuangalia mifano hai niliyonayo katika familia yangu. Nina ndugu wa kiume ambao hata wakati hao mawifi walipokuwa hawajaolewa nilikuwa nawaonea huruma huko wanakojiingiza. Sasa hivi ndio wahangikaji wakubwa kuhakikisha nyumbani kinaeleweka. Waume bado hawana mbele wala nyuma, wadada wanakazana kweli. Pengine ndio yale mambo ya kila shetani na mbuyu wake. I am sure mama zao wanasikitika sana. Mimi kama wifi nasikitika, na kila mara najaribu kuwaeleza wanangu umuhimu wa kuwa na mwelekeo wa maisha uwe wa kike au wa kiume.
 
kama umeolewa, wazazi wako wangekukataklia kuaolewa na unaempenda kisa hana mbele wala nyuma (kama ulivyosema wewe), ungekubaliana nao??

Nachofaham basically watu wantakiwa kuoana chini ya msingi m1 tu wa "love". haya ya mali na elim na future ni kupotoshwa kwa misingi ya mapenzi. ndo sababu wanaooana kwa sababu hizi hua hawadumu na kwa kipindi wanacho exixst mmoja hua anapapta shida sana katika mahusiano.
 

Ninyi wanawake ni pungufu tu kwa asili. asa kwa nini kama hii ndio kesi msifikirie haja ya wakaka kutokuoa wadada wasiokua na mbele wala nyuma??
kwa nini mnadhani kua ni justifiable kwa wakaka kuoa wadada wasiokua na mbele wala nyuma lakini sio justifiable kwa wakaka kutokuoa wadada wasioku na mbele wala nyuma.

kwa taarifa yenu wakaka wamejipanga siku hizi, hakuna mtu anaetaka utegemezi 100%
subirieni mtasubiri sana.
 
Dahhh
Mj1 sante kwa chemsha bongo ..
Kwangu mimi binafsi furaha yamwanangu
ndo nitaipa kipaumbele...

Kama mzazi ningependa mwangu aolewe na mtu mwenye
upendo,hashima, adabu na uti kwa binti yangu..
Na awe na mwelekeo fulani wa maisha
At list awe u na kazi au kipato kitakacho weza kuisaport
familia yake baadaye

Papo hapo natakiwa nijiulize je ndo hiki binti yangu anachotaka...?
maana yeye ndo atakaye ishi na huyo mwanaume...
Si vema kwa mimi ku force my decision kwake
Yeye ni mtu mzama sasa
sana sana utampa ushauri na ni juu yake kuuchukua
au kuiacha..

Cha muhimu mimi kufanya kama mzazi nikumpa mwanangu
Elemu ya kutosha na Mungu akimjalia apate kazi ya maana
ili baada ye asimtegee huyo mwanaume asilimia zote...
 
MJ1,what a lovely post,.very argumentative too.....well,mimi kama mzazi(someday)ningewaelimisha wanangu wote(kike na kiume) juu ya kuwa independent kwanza,kwasababu siku hizi kuna group kubwa la wakaka wanaopenda mteremko!.so ningeanza kwangu kabla sijaanza kuwacriticize watoto wa wengine..pili,Mungu ndo guarantor wa haya maisha hujui leo au kesho itakuaje,so huyo mwanamke au mwanaume ikiwezekana inabidi na yeye apewe a chance kuprove kama anaweza or ndo total failure(which siamini)kila binadamu ana uwezo wake flani..but kuna wale wasiosaidika,hao siezi kukubali..
So MJ1 i will go for IT DEPENDS,maana kuna wenye hela na hawajui zilikotoka,kuna wenye elimu but full usharobaro,kuna wenye kufanya kazi kwa bidii but pesa zote zinaisha due to women na starehe..
Therfore before kusema flani hana hiki na kile,ask youself of what you have na je is that person worth to be challenged?
Love u MJ1.
 
Hivi utakubali binti yako aolewe halafu wewe ndo uwe mlezi wa familia tarajiwa....kwamba wakiumwa waje kwako??? uwape na chakula?? Damn it.....:A S angry::mad2::doh:...povu....

Mapenzi yana macho aisee...
Salama mjukuu??? I think me missing wewe....

babu yaani huwa ninawaza na kuwazua haswa......... nadhani ni sahihi kupenda kwa macho na akili zaidi ya kupenda kwa hisia......na dunia yenyewe ya sasa ambapo ule munkari na mori wa wanaume kuhudumia familia unapungua kwa kasi sasa hukawii kumpata mkwe mwenye aleji na kazi so unaruhusu mwanao anaolewa naye kwa kuwa anampenda! Mh ngumu kuimeza aisee
 
...................Aksante sana Lizzy na kwa bahati mbaya sana ni binadamu wachache sana wenye uwezo wa kujifunza kutokana na experiences. Nadhani kuna umuhimu wa kuachana na fikra za mapenzi ni maua popote huchanua, jamani there was a time nilikuwa ninatathmini kuendelea kuwepo kwa matabaka ya masikini na matajiri na nikaamini kuwa sababu mojawapo ni kuoana kimatabaka mfano mtu mwenye elimu ndogo (na asiye na uwezo) akaoa mwanamke of the same characteristics ni wazi kama ubunifu haupo (na hii ni bahati) hata familia watakayoijenga itakuwa duni yaani ile poverrty circle itakuwa halisi generation hata generation.

Tupende kwa malengo..............
 


Kwa kauli kama hii mtu aseme nini zaidi? Hakuna mtu anaeona ni sahihi kuoa au kuolewa na mtu asiye na mwelekeo. That means tunapaswa kama wazazi kuwasaidia watoto wetu kuwa na malengo katika maisha. Kama wanawake kwa asili ni pungufu au si pungufu hili nafikiri nikuachie ukalijadili na Mama yako mpenzi na Mkeo kama yupo.
 
MJ1 asante kwa mada yenye somo linalohitaji kutupiwa jicho mara tatu tatu. Kwa kweli kama mzazi, pamoja na mapenzi kulinganishwa na maua kuwa popote huchanua, nitamkalisha kitako tuelezane vizuri kuhusu huyo mwenza wake. Manake kwa sasa maisha yalivyokaa, tunatakiwa kupunguza ukali wake njia mojawapo kuwa angalau kila mmoja awe na uelekeo jamani khaa.. Tatizo la ndoa nyingi za sasa, wazazi tumejipotezea kabisa ule muda wa kuchunguza huo upande wa pili ambao wanetu wanaenda kuangukia. Zamani, lazima historia itatoka hadharani kuwa, huko nooooo....kuna ukoma, huo ukoo sahau kabisa wavivuuuuu.....Ila tatizo wa siku hizi nao ving'ang'aniziii, kisa kishakutana nae huko 'kapelekeshwa', basi haangalii kushoto wala kulia kwa kuangalia factor moja tu. Unabaki kujiuliza hasa huko wanakoenda watakuwa wanakula hayo hayo?

Nafikiri somo kubwa pia wazazi tunatakiwa tuanzie mbali kwa kuwajenga watoto wetu kwa maandalizi hayo ya baadaye, siyo wakaonekane hawana mwelekeo huko waendako.
 
Tasia I sijui kwa nini napata hisia kuwa thread hii imekuudhi!! Natanguliza samahani zangu.

Hata hivyo ninashukuru kwa kuweza kutupatia upande mwingine wa shilingi katika huu mjadala. Ni kweli kabisa na ninakubaliana nawe kuwa msingi wa ndoa unatakiwa kuwa ni mapenzi ya kweli. Na ndoa zote zilizojengwa kwenye mapenzi ya kweli hudumu sana.

Lakini kinachonikwaza mie hapa ni vitu viwili
1. Siku hizi kuna hicho kitu cha mapenzi ya kweli? Tuiangalie hii katika dhana nzima ya maisha tunayoishi sasa ambako maadili yamemomonyoka kama si kuisha kabisa, swala la ukweli, uaminifu n.k tunaona jinsi yalivyochakachuliwa najiuliza hili la mapenzi ya kweli kama limehimili hii tsunami ya mmomonyoko wa maadili.
2. Maisha ya sasa si kama ya enzi zetu au za wazazi wetu ambapo kina baba walikuwa wanafahamu wajibu wao kama walezi wakuu wa familia zao hivyo mume alikuwa radhi kuhangaika ipasavyo ilimradi tu atimize majukumu yake kama baba na kichwa cha familia. Sasa hivi ninaona hii imepungua sana na vijana wetu wengi wanakuwa na kijitabia cha uvivu hivi (sijui na malezi yetu mabovu) utakuta mkaka hayuko tayari kufanya kazi ngumu za kutoa jasho (sisemi kuwa hawapo) lakini kuna tabia ya kuchagua kazi na akiona kiwingu ah ataingia kwa madawa ya kulevya i.e. biashara ya madawa ya kulevya.

unawezasema kuwa ujenzi wa familia unatakiwa kushirikisha wote wawili mke na mume ninakubali kabisa lakini wewe mzazi unaona kabisa kuwa mwanao wa kike amefall in love na dreamer..... would you let her get married kweli?
 

Ndugu yangu huna haja ya kuwa mkali hakuna anayekubishia unayoyawaza kwani ni mtazamo wako (na wapo wengine wengi wanaowaza kama wewe) tuelimishe taratibu na kwa hakika tunawezakukubaliana na wewe. Swala ulilozungumzia hapa ni sahihi kabisa (Kasoro hapo uliposema nyie wanawake ni pungufu kwa asili) ninakubaliana na wewe kabisa lakini ninakukumbusha kuwa hata hii inabadilika siku hizi ingawa speed yake bado ni ndogo. Hii imejengeka kwa kuwa ilijengwa tangu enzi za wahenga kuwa Mume ndo mlezi wa familia na ndio maana hata malezi yetu sie wa kale watoto wa kike walikuwa hawaendelezwi kielimu na bila kuwa na elimu mtoto wa kike atakuwaje na uwezo kifedha au kazi nzuri? Lakini kama nisemavyo kuwa hii sasa inabadilika hasa baada ya watoto wa kike wanapewa elimu (ingawa bado kuna wazazi wenye uelewa tofauti juu ya hili).

Lakini pia bado kaka zetu mnapeana shauri mbalimbali ambazo zinapelekea muoe wanawake wasio na uwezo. Si huwa mnaambiana kuwa usilogwe kuoa mke alokuzidi elimu, kipato n.k mnasema watawanyanyasa sana. Kama vile haitoshi mkiona mwenzenu ana mpenzi alomzidi elimu mnamcheka na kumtahadharisha au kama ana mpenzi mwenye kipato zaidi mnamdharau na kumwona analelewa. Sasa haya yote yanapelekea nyie msioe wanawake wa aina hii ndugu yangu.

Hiyo sentensi yako ya mwisho........kama tuko kwenye mipaso kaka yangu ah!! Haifai hivyo.
 
MJI malezi ya mtoto huanza toka mimba inapotungwa ,tunachofundisha watoto wetu mara nyingi huamini na kukua katika misingi hiyo lakini embu tujiulize
1.mapenzi ni nini,je ni pesa na mali ambazo kila mmoja anauwezo wa kusimama na kuzitafuta mwenyewe

nakumbuka wazazi wangu toka niko mdogo walinikatisha tamaa sana kuhusu wanaume wenye pesa,hilo jambo nimekuwa nalo mpaka leo nipo kwenye ndoa ukweli MJI nachohitaji kutoka kwa mwanaume ni mapenzi ya kweli basi pesa kama itakuwepo ni sawa na lazima tukimbizane kufanya majukumu yetu ,lakini kama imeshindikana deep inside my heart naweza kutake care kila kitu.huku nikipata upendo wa kweli basi.

na ndivo nitavomlea mwanangu wa kike ajifunze kusimama mwenyewe na kuhangaikia maisha yake,akibahatika kupata yule anayempenda nitamuuliza na kumwambia ukweli awe amempenda kutoka moyoni mwake,hayo ya maisha yao watafundishana na kuelekezana wakiwa ndani.

huwezi kuununua upendo wa kweli kwa pesa hata siku moja.mapenzi ya kweli yapo tatizo wenye mapenzi ya kweli wanakutana na wacheza sinema na wenye makovu ya mapenzi wanaishia kuumizwa kwaiyo game linaendelea ivo.
 

Aksante Tracy umesema vema mtazamo wako na nimekuelewa.......May be maelezo yangu yamekanganya ninaposema hana mbele wala nyuma sikumaanisha pesa au utajiri wa mtu..............maana yangu niliyotaka iweka ni ile hali ya mtu kutokuwa na malengo katika maisha mf. Yeye ni lifist................yaani hana future development plans si kwake binafsi wala watoto wake. Cha kuhimu ni msimamo au malengo ya maisha .
 

Dah, kama nakuona vile kwenye hiyo Keybord.
Nashukuru sana kwa huu ukweli uliousema hapa.

Ila kiukweli, sio mtoto wangu tu, hata mdogo angu, rafiki yangu jirani yangu, si mshauri aingie kwenye ndoa na mkaka/mwanaume ambaye hana mbele wala nyuma. Amelelewa kwenye taulo, hajui kuhangaika na maisha, hajui hili wa lile, hakhaaaaaaa ya nini kujitesa mwenzangu.
 

MJ1 umefafanua vizuri sana, si swala la pesa na utajiri linalozungumziwa hapa ila malengo ya kimaisha, Je huyu mtu anajitambua? Je ni mtu ambae anaishi kwa kutegemea marafiki, wapambe na ndugu? Kutwa kucha anazunguka na watu wenye shughuli zao kuwapigia hadithi na anaona sawa? Anatumiaje muda wake? Maana wapo , wao kazi kuulizia leo kijiwe kipo wapi mfukoni hana kitu na wala haoni kwa nini ajishughulishe...mara unamsikia anataka kuoa. Je huyu atajenga familia ya namna gani?
 

Dada Keren-Happuch, mchango wako ni mzuri kabisa. Ingawa si wakati wa kuwachagulia watoto wetu waume/wake, ni busara kuangalia sifa za mtarajiwa na kumshauri mhusika ipasavyo kwa kadiri tunavyoyaona sisi, bila ya kulazimisha. Kwani yakimwendea upande sisi tutakuwa wa kulaumiwa. Tuwaoneshe njia, mshauri, lakini uamuzi wa mwisho tuwawachie mwenyewe. Sisi kama wazazi, wajibu wetu ni kuwaunga mkono muda wote. Mtoto anaweza kuwa yuko sawa, inawezakana kuwa ameteleza, lakini likitokea hili la mwisho, tuwapokee waje kuanza upya. Wakiwa wana wa kufahamu, wataelewa kuwa kujikwaa si kuanguka.
 

As long as they love each other i will let her go, experience niliyoisema hapo ni ile tu niliyoipitia mimi tangu wakati wa mapenzi na ndoa sio wazazi wangu, understood?
 


Ukimpenda mtu haya yote utaona ni ya kawaida mamii, waliweka malengo wengi tukawashuhudia mwishoni waliangukia wasikotarajia na wakang'ang'ania hukohuko. ni uamuzi mzuri ukiusimamia bila kutetereka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…