Mkungunero
JF-Expert Member
- Aug 13, 2023
- 401
- 569
ASALI MUBASHARA-Jumatatu 16/10/2023
Karibuni ndugu zangu wapendwa kwa adhimisho la misa Takatifu asubuhi hii.
Bwana Yesu anasikitishwa na kizazi kisichokuwa na imani; kila wakati kinatafuta ishara. Hakioneshi kuridhika na ishara zilizopo. Bwana Yesu anasema kwamba hakitapewa ishara zaidi ya ile ya Yona kwa watu wa Ninawi. Watu wa Ninawi walimpokea Yona na mafundisho yake kama yalivyo bila kudai mahubiri mengine.
Malkia wa Sheba aliyafurahia mafundisho ya mfalme Sulemani. Lakini kizazi hiki hakiridhiki na kile kinachotendwa na Yesu. Siku zote watu wasio na imani, hawaridhiki. Watu wa kizazi hiki walishindwa kumwona Yesu kuwa ishara tosha. Hakuna ishara kubwa zaidi ya Yesu. Yesu ni mkuu kuliko Suleimani. Ikiwa walimkataa Yesu, wasingaliweza kupatiwa ishara nyingine ambayo ingewasaidia.
Basi tujiombee tuige unyenyekevu kama wa watu wa Ninawi. Tusiwekeze kwenye miujiza na ishara. Tukiwekeza kwenye miujiza tutaishia kudanganywa na manabii wa uongo.
Mt. Paulo anamtangaza Yesu kama mtoaji na mgawaji wa huduma zote. Yeye hakujituma mwenyewe; na hatendi kazi ya utume kwa ajili ya kujitangaza yeye bali ni kwa ajili ya Yesu. Kazi ya Mt. Paulo ni kuihubiri injili kwa watu wa mataifa. Tujiombee ili nasi tukubali kutumwa kwa ajili ya kazi ya Bwana.
Sala: Bwana, ninakuomba nikugeukie wewe ishara ambayo ninahitaji kila siku, Amina.
©️Pd. Prosper Kessy OFMCap.