Asali ya nyuki wadogo na ndimu/limao

Asali ya nyuki wadogo na ndimu/limao

Mparee Halisi

Senior Member
Joined
Jan 4, 2014
Posts
104
Reaction score
8
Naombeni ufafanuzi wana JF,nimesikia asali na ndimu/limao ni Dawa nzuri sana ya Mafua na kikohozi,vipi kuhusu asali ya nyuki wadogo ukichanganya na ndimu/limao?
 
Naombeni ufafanuzi wana JF,nimesikia asali na ndimu/limao ni Dawa nzuri sana ya Mafua na kikohozi,vipi kuhusu asali ya nyuki wadogo?


...ASALI NA MDALASINI


ASALI: KIBOKO YA UNENE:

Yahusu kupunguza unene;

Endelea... Baada ya hapo unaweza kuchuja na kupata kinywaji kisicho na vipande wala ungaunga. Kunywa nusu kikombe kabla ya kula kitu chochote asubuhi. Nusu kikombe kinachobaki, kihifadhi kwenye friji au sehemu safi na salama na uimalizie kunywa usiku wakati ukienda kulala. Jambo la kuzingatia hapa ni kuepuka kuchanganya asali kwenye maji ya moto kabla hayajapoa, kwa kufanya hivyo utaua virubisho muhimu vilivyomo kwenye asali. Tengeneza na kutumia mchanganyiko huo kila siku na uangalie matokeo yake. Baadhi ya watumiaji wameweza kupunguza hadi kilo 3 kwa wiki moja. Tahadhari inatolewa kwamba hakikisha unatumia mdalasini halisi kama ilivyo kwa asali. Aidha, mchanganyiko huo uutumie kwa kipindi ambacho utatimiza lengo lako la kupunguza uzito, lakini usitumie kwa muda mrefu sana na isizidi miezi minne mfululizo.

ASALI NA MDALASINI HUTIBU MAGONJWA MENGI

Imedhihirika kuwa asali na mdalasini vina uwezo wa kutibu magonjwa mengi. Nchi nyingi duniani zinazalisha asali na zimekuwa zikiitumia katika aina mbalimbali za madawa. Hata wanasayansi wa sasa wamekubali kwamba asali inasaidia katika kutibu magonjwa mengi. Aidha, wanasayansi wamethibitisha ubora na maajabu ya asali kwa kusema kuwa ingawa asali ni tamu kama sukari, lakini ikitumiwa kwa kiwango kinachotakiwa kama dawa, haiwezi kumdhuru hata mgonjwa wa kisukari.

Katika jarida moja la nchini Canada liitwalo Weekly World News, lilichapisha orodha ifuatayo ya magonjwa yanayoweza kutibiwa na asali, kama ilivyothibitishwa na Wanasayansi wa Magharibi: MAGONJWA YA MOYO: Tengeneza ‘pesti’ ya asali na mdalasini (kama tulivyokwisha eleza), kisha tumia kama jamu kulia mkate, chapati, n.k na uwe unakula mara kwa mara wakati wa kufungua kinywa asubuhi. Mchangayiko huu huondoa lehemu kwenye mishipa ya damu na hivyo kumuepushia mtu uwezekano wa kupatwa na mshituko wa moyo au kiharusi. Na kwa wale ambao wameshapatwa na kiharusi kwa mara ya kwanza, watajiepusha na kupatwa kwa mara ya pili. Utumiaji wa mara kwa mara wa mchanganyiko huu wa asali na mdalasini, huondoa tatizo la kupumua kwa shida na kuimarisha mapigo ya moyo. Nchini Marekani na Kanada, wakunga wa majumbani wamegundua kwamba kadri mtu anavyozeeka , njia ya kupitishia damu nayo hudhoofika, lakini kwa kutumia asali na mdalasini mishipa huendelea kuimarika.

KUUMWA NA MDUDU:

Mbali ya kukinga magonjwa ya moyo, asali na mdalasini pia ni dawa ya vidonda vitokanavyo na kuumwa na wadudu wa aina mbalimbali. Ili kupata dawa hiyo, chukua kiasi kidogo cha asali na maji ya uvuguvugu (kijiko kimoja cha asali na vijiko viwili vya maji) kisha changanya na kijiko kimoja kidogo cha unga wa mdalasini na uwe kama ‘pesti’. Upakae mchanganyiko huo katika sehemu inayouma kwa kuchua. Imeelezwa kuwa mara baada ya kupakaa mchanganyiko huo , nafuu huweza kuanza kuonekana ndani ya dakika moja hadi mbili, ikimaanisha utendaji kazi wake ni wa mara moja.

UGONJWA WA BARIDI YABISI:

Mtu anayesumbuliwa na ugonjwa wa baridi yabisi (Arthritis) huweza kupata nafuu iwapo atatutumia mchanganyiko wa asali vijiko viwili na kuchanganya na glasi moja ya maji ya uvuguvugu pamoja na unga wa mdalasini. Mchanganyiko huu utumiwe kila siku asubuhi na jioni. Katika utafiti mmoja wa hivi karibuni, uliofanywa na Chuo Kikuu cha Copenhagen nchini Denmark, uligundua kwamba wagonjwa 200 wa baridi yabisi au viungo vya mwili (arthritis) waliotibiwa kwa kupewa vijiko viwili vidogo vya asali na mdalasini kabla ya kufungua kinywa asubuhi, 73 waliacha kusikia maumivu ndani ya wiki moja.


KUTOOTA NYWELE/UPARA:

Ni habari njema pia kwa watu wenye matatizo ya kutoota nywele utosini au kuwa na kipara. Changanya ‘Olive Oil’ ya moto na kijiko kimoja kikubwa cha asali na kijiko kidogo cha unga wa mdalasini. Kisha pakaa sehemu isiyoota nywele na uache kwa dakika 15 kabla ya kwenda kuoga. Dawa hii imeonekana kusaidia sana hata kwa kuweka kwa dakika 5 tu.


KUSAFISHA KIBOFU CHA MKOJO:

Chukua vijiko viwili vikubwa vya unga wa mdalasini, changanya na kijiko kimoja kidogo cha asali, tia ndani ya maji ya uvuguvugu kisha kunywa , mchanganyiko huo huua wadudu wote na kuacha kibofu cha mkojo safi.


ASALI DAWA YA JINO:

Ili kutengeneza mdalasini na asali kama dawa ya jino, chukua kijiko kimoja kidogo cha mdalasini na vijiko vitano vidogo vya asali. Changanya asali na mdalasini ili kupata mnato maalumu (paste). Pakaa mnato huo katika sehemu ya jino inayouma, mara tatu kwa siku hadi maumivu yatakapoondoka.

ASALI DAWA YA KUONDOA LEHEMU (CHOLESTROL)


Changanya vijiko vikubwa viwili vya asali na vijiko vitatu vidogo vya mdalasini kisha weka kwenye kikombe cha maji yenye moto kiasi kama ya chai na changanya. mchangaynyiko huo anapopewa mgonjwa wa lehemu, utafiti umeonesha kuwa kiwango cha lehemu katika damu hupungua kwa asilimia 10 ndani ya saa mbili tu. Aidha, utafiti zaidi umeonesha kama mchanganyiko huo ukitumiwa mara tatu kwa siku kwa muda fulani, tatizo la lehemu huweza kutibiwa kabisa. Kwa mtu ambaye hana tatizo hilo kwa sasa, akiwa na mazoea ya kulamba asali kila siku vijiko viwili au kimoja baada ya mlo usiku, hatapatwa na tatizo la lehemu katika maisha yake. kama mnavyojua , lehemu ndiyo chanzo cha magonjwa ya moyo pia.


MATATIZO YA MAFUA:

Kwa wale wenye matatizo ya mafua sugu au ya muda mrefu, wanaweza kupata nafuu au kupona kabisa kwa kutengeneza na kutumia mchanayiko wa asali na mdalasini . Changanya asali kijiko kimoja cha chakula na robo kijiko cha unga wa mdalasini, tumia mara tatu kwa siku.


ASALI HUWEZA KUTIBU TATIZO LA UZAZI:

Kuna utafiti umeonesha kuwa asali huweza kuimarisha mbegu za uzazi kwa akina baba na kuondoa tatizo la kutoshika mimba kwa akinamama. Akina baba wenye tatizo la upungufu wa mbegu za kiume, walipoanza kutumia asali kwa kulamba vijiko vikubwa viwili vya asali kila siku kabla ya kulala, waliondokewa na tatizo hilo baada ya kipindi kifupi. Wanawake wa China na Japani wenye matatizo ya kutoshika mimba wamekuwa wakitumia mdalasini kuondoa tatizo hilo. Kuondoa tatizo hilo, wanawake hao huwa wanaweka mchanganyiko wa nusu kijiko kidogo cha asali na kiasi kidogo cha unga wa mdalasini na kuupaka mara kwa mara kwenye fisi mchana kutwa. Utaratibu huo huwezesha mchangayiko huo kuingia mwilini taratibu kwa njia ya mate kwa siku nzima. Kuna ushuhuda uliwahi kutolewa wa mama mmoja nchini Marekani ambaye alikuwa na tatizo la kutokuzaa kwa muda mrefu, lakini baada ya kutumia asali na mdalasini waliweza kupata watoto mapacha. Orodha ya matatizo ya kiafya yanayotibiwa na asali na mdalasini ni ndefu. Baadhi ya matizo hayo ni pamoja na kujaa gesi tumboni, upungufu wa kinga ya mwili, ukosefu wa choo, vipele, magonjwa ya ngozi, saratani ya tumbo na mifupa, uchovu, harufu mbaya mdomoni na kutosikia vizuri. Kwa ujumla, asali na mdalasini inafaa kutumiwa katika milo yetu ya kila siku, kwani faida zake kiafya ni nyingi na ni kinga ya mataizo mengi ya kiafya , makubwa na madogo.
 
Back
Top Bottom