Asante Erasto Nyoni, Karibu Ibrahim Ame

Asante Erasto Nyoni, Karibu Ibrahim Ame

MTAZAMO

JF-Expert Member
Joined
Feb 8, 2011
Posts
19,675
Reaction score
33,583
Wakuu,

Mimi nimekuwa mshabiki sana wa mabeki ambao wana uwezo mkubwa wa kumiliki mpira. Nilikuwa kichaa wa George Masatu na baadae Victor Costa. Baada ya Victor Costa niliamini kizazi cha mabeki wenye akili kimeisha then akaibuka Erasto Nyoni! Huyu mpira unamtii yeye, anaweza kufanya anachotaka akiwa na mpira.

Wakati wengi tukihisi Erasto Nyoni inakuwa jioni kwake tumepata igizo jipya ambalo sihitaji kumuona mechi nyingi kuamini uwezo wake, Ibrahim Ame!

Pale tumesajili mtu na nusu na bora tulivyomkosa Mwamnyeto. Ukimuangalia Ame unamuona Victor Costa na Erasto Nyoni! Kwa Utulivu, ball control na nguvu. Inawezekana akawa mkali wa kupiga penati pia, Tusisahau, Masatu, Costa na Nyoni hawajawahi kukosa penati.

Sasa kwa amani sina wasiwasi Erasto akiamua kupumzika, tumepata mbadala wake Simba na timu ya taifa. Nafikiri kocha wa Taifa Stars atambue sasa kuwa hili Taifa lina vipaji vingi ila hatuna njia ya kuviibua na kuishia kuteua kwa mazoea, imagine Ally Mtoni amewahi kuitwa Taifa Stars na si Ibrahim Ame.

Ibrahim Ame kaza mdogo wangu, wewe ni hazina ya nchi na tegemeo la muda mrefu sababu ya umri wako.
 
Watu wa tanga wenyewe wanakwambia AME alikuwa staa kabla ya mwamnyeto hapo coastal ..
Akapata majeraha ya muda mrefu ndipo Jamal akajenga jina zaid na AME ariporeje a uwanjani akaanza upya
Wamekudanganya
Ame alicheza ndondo cup akaonekana akaenda piga majaribia coast ndo wakamsajili sasa ustaaa kitambo unatoka wapi?
 
Sijasemea AME ameanzia kuchezea wapi
Bali kati yake yeye na mwamnyeto yupi aliwahi kushine kabla ya mwenzake

Elewa
Msimu wa kwanza Ame anacheza coast ulikua hata unamjua? Hakuna hata aliyemwongelea.
Msimu huu wa pili baada ya combination yake na mwamnyeto kuiva ndo kapata jina.
 
Msimu wa kwanza Ame anacheza coast ulikua hata unamjua? Hakuna hata aliyemwongelea.
Msimu huu wa pili baada ya combination yake na mwamnyeto kuiva ndo kapata jina.
Nadhani hujaelewa kabisa point yangu .

Kwaheri
 
Back
Top Bottom