Asante John Rafael Bocco kwa kuwaziba midomo Ayub Fc waliokuwa wanakupinga vikali kubaki Simba sc.

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2016
Posts
10,587
Reaction score
13,425
Mashabiki wa Ayubu FC kuanzia jukwaa pendwa la Jamii forum waliandika nyuzi nyingi na kupiga kelele nyingi kuwa Bocco umezeeka hufai kuichezea Ayubu Fc.

Ikafikia hatua mashabiki wakaanza kumpangia kocha ampange Moses Phiri badala ya John Bocco.

Kwa ushangiliaji ule wa John Bocco kwa wenye akili kubwa Kama NALIA NGWENA tumeshaelewa kuwa mashabiki wa Ayubu FC wapunguze mdomo na John Bocco yupo sana ndani ya kikosi Cha Ayubu FC.

Na jinsi mashabiki walivyo mbumbumbu Kama alivyowaita Rage walizani The captain fantastic John Bocco anawanyamazisha mashabiki wa Yanga.

PIGA KAZI JOHN BOCCO
NO BOCCO NO SIMBA.
 
Aaahaaaa ajiandae na Al Ahyl
 
Kwa mujibu wa kocha mkuu wa Simba Sc, Robertinho amesema mshambuliaji John Bocco pekee amekuwa akifanikiwa kucheza kwa maelekezo yake kwa kutumia muda mwingi kukaa ndani ya eneo la wapinzani faida ambayo imewapa nafasi ya timu hiyo kufunga mabao.

Kocha huyo amesema “Sikiliza, ni kweli naiona hiyo hali, mashabiki waje uwanjani kuangalia Simba inacheza mpira vizuri, Kwangu Bocco bado ni mshambuliaji mzuri kwani anakwenda kufanya kile ninachokitaka afanye,” amesema Robertinho na kuongeza;

“Hata katika mechi dhidi ya Power Dynamos aliingia akafanya nilichotaka tukapata bao lililosaidia kutuvusha makundi na juzi nimempa nafasi ya kuanza amefunga tena, lakini akawafanya mabeki wa Prisons kwa muda mwingi kubaki nyuma, nataka mshambuliaji wa aina hii anayekaa muda mrefu eneo la hatari la wapinzani na hili ndicho anafanya Bocco huyu bado ni bora kwangu.”

Kocha huyo amesema anayo washambuliaji wengine kama Jean Baleke na Moses Phiri ambao nao ni wazuri kwa kukimbia pembeni lakini wamekuwa hawajaweza kucheza kwa nidhamu kama anavyofanya Bocco.
.
“Simba tunajivunia kuwa na washambuliaji wengi wazuri, kwa Baleke na Phiri angalieni tu, muda mwingi wanataka kukimbia pembeni hili linatufanya kushindwa kutumia vizuri nafasi tunazotengeneza tunaendelea kuwaongezea ubora huo na wao ili wacheze kama Bocco.
.
“Nimezungumza na Bocco nimemwambia aachane na mambo ya mashabiki anisikilize mimi kama kocha wake, mashabiki wanataka ushindi hesabu zetu ndio zitakazowapa furaha, unaona amefunga wamenyamaza nataka aendelee kufanya hivyo hivyo kila mara kwani nitaendelea kumtumia,” amesisitiza Robertinho aliyefikisha jumla ya mechi 15 bila kupoteza katika ligi kuu ya Tanzania.
 
JOHN BOCCO YEYE YUPO BIZE NA MASHABIKI WANAOMSEMA VIBAYA.
 
Hahahaha 🤣🤣🤣🤣 hahahaha hahaaaaaaaaaaaa.
 

Nipo pamoja na kocha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…