Asante kwa msaada wenu madr wa JF(Feedback)

Asante kwa msaada wenu madr wa JF(Feedback)

MadamG

Senior Member
Joined
Feb 1, 2013
Posts
125
Reaction score
47
Nashukuru sana kwa madr wa jf Watu8, Bubu msemaovyo, Andate, Maubero, Mzizi mkavu na wengineo walionisaidia kunitajia siku za kupata mimba ushauri wenu niliufanyia kazi na sasa natoa shukrani kwa kufanikiwa kushika mimba mbarikiwe na mwendelee kutusaidia.

Nina ombi jingine kwasababu ni mimba ya kwanza utunzaji wake, pia nina kama wiki ikifika usiku nakuwa na njaa sana hadi nakosa usingizi chakula cha usiku napendelea sana chipsi mayai au inachangiwa na kutokuwa na hamu ya kula nikila kidogo tu nashiba je iyo hali itaisha baada ya muda gani?
 
MadamG hepuka kula sana hizo chips hongera pia jitahidi kuwa na vitu vidogovidogo vya kutafuna kama snack na matunda muda ambao hujisikii kula
 
Last edited by a moderator:
Mimba ina week harafu unapendelea kula
Mie najua ikiwa kubwa miezi sita na kuendelea ndo unakuwa na njaa sana
Hongera
 
Kazi kweli kweli..mwenye mbuzi kashindwa kujua mbuzi ale nini ili anenepe...
 
hahahahaha kweli jf burudani
ngoja tumsubiri mtoto wetu kwa hamu
ha haa, hiyo hali iliwahi nipata, siku siyo nyingi.....
fikiria hapo nilishajisemesha nimemaliza mahesabu long time ago, halafu mtu unakosema mahesabu...... akili yote inawaza mimba......
after siku kama 3 hivi nikaanza kuhisi dalili zoote za mimba..... bado kidogo nipate kichaa, basi nikawa najitengenezea kapicha kangu ka mimba jioni hii....... baada ya wiki 2, wajomba hao wamekuja kutembea, nilirukaje sasa kwa furaha.....
 
Ati watu8 !????? a a nakataaaaa.......
 
Last edited by a moderator:
Woow!! Hongera sana rafiki MadamG...nakumbuka namna ulivyokuwa na wasiwasi siku ile uliyoweka uzi wako hapa.

Kwenye hilo la Chakula ngoja niwapishe wenzangu waliobobea hapo labda wanaweza kuwa na maneno muafaka ya kukushauri.
 
Last edited by a moderator:
Munamsahau Mupirocin amewapa formula nzuri sana ya namna ya kupata mimba coz mzizimkavu nakumbuka alikuwa amekosea hata formula na mupirocin akamrekebisha, sijui labda ulitumia njia ipi.

Lakini tunashukuru kwa feedback coz wapo wanawake wengi hata wasomi hawajui siku za kupata mimba, wanagegedana tu bila mpangilio.
 
Uangalizi unapokuwa mja mzito

Hii ni kutunza afya yako wakati wa mimba ili kuongezea tokeo la kupata mtoto aliye na afya. Haya ni baadhi ya mambo yatakayo kuwezesha kuwa na mimba iliyo na afya na kujifungua vyema.

  • Anza kujitunza mapema na kwa kawaida. Hii inaweza husisha uchunguzi na vipimo kuhakikisha kijusi/mimba ina afya na vipimo kuhakikisha mwili wako unafanya kazi ipasavyo.
  • Hakikisha unakula chakula kilicho na protein, matunda, mboga, nafaka na madini ya ‘calcium’ kijusi/mimba hupata chakula chote kutoka kwako, hivyo chagua chakula kitakachokupa afya. Jaribu kula mara tatu kwa siku na mara sita vipimo vidogo vidogo kama una matatizo ya uchefuchefu au kuhara.
  • Daktari wako anaweza kukushauri unywe vitamini zilizo na chuma (iron) na ‘folic acid’ ili kusaidia kukuzuia kupatwa na upungufu wa damu. Vitamini hizi pia hulinda kijusi kutokana na magonjwa ya ubongo na uti wa mgongo.
  • Jaribu kufanya kazi itakayokuhitajia nguvu zako kwa dakika 30 siku kadhaa kwa wiki. Mazoezi husaidia kupatia misuli yako nguvu itakayotumika wakati wa kujifungua na kuhufanya uwe na raha/rafaja wakati wa mimba. Kuogelea, kutembea na mazoezi mengine hukufaa sana wakati wa mimba. Hakikisha umeongea na daktari wako kabla hujaanza zoezi lolote.
  • Kunywa aghalabu bilauri 6-8 za maji kila siku; na bilauri nyingine kwa kila saa litumiwalo katika mazoezi. Hili hukuzuia kuishiwa na maji mwilini, ambalo unaweza kusababisha mkazo hivyo kujifungua kabla ya muda wake kuwadia.
  • Pata/ongeza uzito ufoao. Kwa wanawake wengi, hii uwa kilo 11-16. Daktari wako atakusaidia.
  • Pata pumziko. Wakati wa mimba unaweza kupata mabadiliko ya ‘hormon’, ambayo yanaweza kusababisha mabadiliko ya tabia yake (furaha na hasira) jichunge kimwili na kiakili.
  • Muambie daktari wako kama ‘unatumiwa’ vibaya (abuse). Hili linapoendelea wakati wa mimba hukuweka wewe na kijusi hatarini ya kuharibika kwa mimba au kujifungua mtoto aliye na uzito mdogo isivyotarajiwa.
  • Ongea na daktari wako kuhusu kazi uifanyayo na usalama wa kazi hiyo. Wanawake wengi walio na mimba iliyo na afya wanaweza kuendelea na kazi yao ya kawaida hata wiki za mwisho za mimba Madam G
 
Last edited by a moderator:
[h=1]Dalili za kukutahadharisha[/h]Kama utaona baadhi ya yafuatayo, mwone daktari haraka iwezekanavyo:

  • Damu au maji maji zikitoka ukeni
  • Unarudiwarudiwa na uchefuchefu na kutapika
  • Kufura kwa uso au vidole
  • Kuumwa na kichwa kusikoma
  • Kizunguzungu au kuona kusikodhahiri
  • Uchungu au kiharusi kwenye sehemu ya chini ya tumbo
  • Homa na kibaridi
  • Kubadilika kwa mwendo (mazunguko) ya mwanae tumboni.
  • Mkojo kidogo zaidi au kuwashwa wakati unapokojoa
Kumbuka, inakufaa ufanye kila kitu uwezacho kujiweka na mtoto wako na rai.

[h=1]Jinsi mtoto hukua akiwa tumboni[/h]Awamu ya kwanza

  • Moyo huanza kupiga
  • Kichwa, mikono, vidole vya miguu viungo vingine mishipa ya fahamu zinatengenezwa.
  • Nywele zinaanza kumea
  • Awamu hii ikiisha, kijusi huwa na urefu wa centimita 10 na gramu 28.
Awamu ya pili

  • Viungo vinaendele kukua na kijusi kwa wakati huu kinakua upesi
  • Nyushi na kucha zinaota
  • Kijusi kinaanza kusonga, kurusha mateke, kulala, kuamka, kumeza, kusikiza na kukojaa
  • Ngozi ya mwili kwa wakati huu imejikunja na huwa na nywele
  • Kujusi huwa na urefu wa centimita 30 na huwa na uzito wa kilo moja awamu/kipindi hiki kikikamilika

Awamu ya tatu

  • Nywele zilizo mwilini zinatoweka
  • Mifupa ya mwili inakuwa migumu lakini ya kichwa huendelea kuwa ya kunyumbuka/kukunjikana
  • Kijusi hukaa
  • Awamu hii ikikamilika, kijusi huwa cha centimita 50 na uzito wa kilo 3-4

Jihusishe na ujifunze jinsi unavyoweza kukaa kwa afya wakati wa mimba. Unaweza kumuuliza daktari wako maelezo ili kumpa mwanao msingi bora wa maisha.



 
Kumuona Daktari

Daktari wako atapanga miadi kwa muda wa miezi tisa ili kuhakikisha wewe na mwanao mna rai. Mimba hukaa kwa muda wa wiki 40 (kutoka wakati wa hedhi ya mwisho) na hugawanywa kwa awamu tatu. Awamu ya kwanza huwa ya wiki 12, ya pili wiki 15 na ya tatu wiki 13.

Miadi hii ili kuhakikisha mimba iliyo na afya huwa:

  • Siku moja kwa miezi katika miezi ya kwanza sita.
  • Siku moja kila wiki mbili kutoka mwezi wa saba hadi wa nane (7-8)
  • Mara moja kwa wiki hadi wakati wa kujifungua.

Kufuata miadi hii huwa muhimu sana, hata kama wajihisi mzima, Hivyo, daktari wako anaweza kuchukua hatua kama wewe na mwanao mna matatizo.

Katika miadi ya kwanza na daktari wako, daktari atakuuliza kuhusu afya yako na historia ya familia yako na atakupima damu na mkojo pia. Kama una ugonjwa wowote kama, kupandwa na damu, shida za moyo na mishipa ama ugonjwa mwingine wowote, usisahau kumwambia daktati wako kama ni za kununua dukani). Haya ni mambo unayofaa kujulisha daktari wako kwani yanaweza kuadhiri mtoto wako, hivyo jaribu kumweleza wasiwasi.

Daktari wako atakufanyia uchunguzi kama wa urefu, uzito na viungo vilivyo karibu na nyonga. Baada ya miadi hii, unafaa kuwa na wazo la lini utajifungua.

Miada mingine huchukua muda mfupi lakini daktari atachunguza mwendo wa damu yako, mkojo na uzito. Uchunguzi mwingine ni kama wa kasoro za kuridhi au kasoro zinginezo. Ili kujua jinsi mwanao anakua, unaweza kufanyiwa uchunguzi awa ultrasound: Kumbuka kumwambia daktaari mabadiliki ambayo umapata/umeona kutoka wakati wa miadi ya awali. Pigia daktari wako simu kama umepata matatizo yoyote katikati ya miadi.


Unayafaa kujiepusha nayo


Usijiweke hatarini wakati wa mimba. Tumia wakati huu kufanya mabadiliko fulani maishani yako:

  • Acha kuvuta sigara* - uvutaji wa sigara wakati wa mimba huongezea hatari ya kuharibu mimba, kujifungua kabla ya wakati ufaao, kuzaa mtoto aliye na uzito mdogo isivyotarajiwa, SIDS na matatizo mengine.
  • Usinywe pombe – unywaji pombe wakati wa mimba huweza kusababisha kasoro ambazo haziwezi kuzuilika kama kupungukiwa na akili.
  • Usitumie dawa za kulevya – Bangi, Cocaine, Heroin, Speed, PCP na dawa zingine za kulevya zaweza kusababisha kuharibika kwa mimba, kuzaa kabla ya wakati ufaao na kasoro zingine. Mtoto anaweza pia kupata matatizo ya kusoma (kuelewa) na anaweza kuzaliwa akiwa mzoevu* kwa dawa hizi ongea na daktari wako kama wataka kuacha kutumia dawa hizi.
  • Punguza au acha kutumia kafeini ipatikanayo katika kahawa, chai, vinywaji ‘chocolate' na dawa ziuzwazo dukani.
  • Usikule samaki, kuku au nyama nyingine ya mnyama kama haijaiva vizuri.
  • Jiepushe na kemikeli zenye sumu kama kuua za wadudu, rangi, vyuma kama lead na mercury.(Bidhaa nyingi za nyumbani zilo na tahadhari kwa walio na mimba) Bidhaa hizi kama hauna uhakika.
  • Jiepushe na ‘bafu ya pipa' (tub) na ‘Saunas' za maji moto. Hizi huongezea hatari ya kuharibika kwa mimba na kasoro zingine za uzazi.
  • Usioshe au kushika kisanduku cha paka wako. Hili linaweza kuambukiza maradhi yanayoweza kusababisha kasoro za uzazi. Pia valia vifuko vya mikono (gloves) unapofanya kazi shambani au mahali paka wako huwa Madam G
Ninakutakia kila la kheri mimba yako ikuwe kwa salama akuwe mtoto mwema mwenye kukusikiliza wewe mama yake inshallah.

 
Watu8 na wewe ni Dr? anyway hongera kwa ushauri hadi madam amepata ujauzito. mimba ina wiki...... siwezi kutoa ushauri wowote atleast ifikishe mwezi lol! hukawii kusema una mimba mara wageni wakaja lol!
Woow!! Hongera sana rafiki
MadamG...nakumbuka namna ulivyokuwa na
wasiwasi siku ile uliyoweka uzi wako hapa.

Kwenye hilo la Chakula ngoja niwapishe wenzangu waliobobea hapo labda
wanaweza kuwa na maneno muafaka ya kukushauri.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom