Neema ya BWANA
Member
- Jun 25, 2023
- 45
- 32
Kwa takriban karne 21 sasa Bara la Afrika limekuwa likitegemea Teknolojia kutoka Nchi za Magharibi ikiwemo Marekani, Ujerumani, Uingereza na baadhi ya Mataifa ya Asia Magharibi. Kwa hili naomba niseme asante sana kwa Mataifa ya Magharibi kwani mmeweza kulisaidia Bara la Afrika katika nyanja mbalimbali ikiwemo Uchumi, Ulinzi na Usalama na Teknolojia yenyewe; asanteni sana.
Swali linarudi kwetu sisi Waafrika baada ya kushirikiana kindakindaki kwenye masuala ya Ki-Teknolojia na Mataifa ya Magharibi mpaka kufikia karne hii ya 21; je! Tunapojitathmini kwa sasa, tumeweza kufikia malengo ya kujitegemea Ki-Teknolojia na hata kupelekea kusimama wenyewe kwenye nyanja muhimu ambazo ni Elimu, Afya, Ulinzi na Usalama, Uchumi na Teknolojia yenyewe?
Jibu ni hapana, mpaka Karne hii ya 21 bado Bara la Afrika ni tegemezi KITEKNOLOJIA kwa Mataifa ya Magharibi na Asia Magharibi hata kupelekea kuendelea kuwa tegemezi kwenye nyanja muhimu za Elimu, Afya, Ulinzi na Usalama, Uchumi na Teknolojia yenyewe kwa Mataifa ya Magharibi na Asia Magharibi.
SABABU ZA BARA LA AFRIKA KUWA TEGEMEZI KWA NCHI ZA MAGHARIBI NA ASIA MAGHARIBI
Sababu zilizopelekea Bara la Afrika kuwa tegemezi kwa Mataifa ya Magharibi na Asia Magharibi ni UKOLONI NA UTUMWA uliofanyika barani Afrika miaka ya 1990 kurudi nyuma mpaka miaka ya 1960 na kurudi nyuma zaidi ya miaka ya 1960 ambapo waliofanya biashara hii ya Utumwa yalikuwa ni Mataifa ya Magharibi pamoja na Mataifa ya Asia Magharibi barani Afrika.
Sababu hii ya Ukoloni wa Mataifa ya Magharibi na Asia Magharibi kwa Bara la Afrika imepelekea Bara la Afrika kuyachukulia Mataifa ya Magharibi na Mataifa ya Asia Magharibi kama mzazi wake hivyo yamekuwa kama vile mtoto ambaye hawezi kutoka nyumbani kwa baba na mama yake kwenda kujitegemea na kutafuta maisha sehemu nyingine kwa hofu ya kushindwa.
Ili Bara la Afrika liweze kusimama na kujitegemea tunatakiwa kutoka kwenye mikono ya Mataifa ya Magharibi na Mataifa ya Asia Magharibi kisha KUACHA utegemezi wa kuyategemea Mataifa haya kuendesha mambo yetu binafsi, bali Afrika inatakiwa kuhama kwa baba na mama ambaye ni Mataifa ya Magharibi na Mataifa ya Asia Magharibi kwa amani kama ambavyo mtoto huondoka kwa amani kutoka nyumbani mwa wazazi wake na kwenda kuambatana na mkewe au mumewe kwa ajili ya kuanza ukurasa mpya wa maisha ili hatimaye aje kuwa tegemeo la wazazi wake yaani wazazi waanze kumtegemea mtoto.
Hatutakiwi kuachana na Mataifa ya Magharibi na Asia Magharibi kwa chuki, hasira, maneno ya kashfa na visasi kwani tukumbuke fadhila zao pale waliposimama kama wazazi sisi Bara la Afrika tulipokuwa watoto wadogo, hivyo tunatakiwa tuachane nao kwa AMANI NA KUTAKIANA KILA LA HERI ili tukaanze maisha mapya tukiwa kama mtoto mwema ambaye hakugombana na wazazi wake siku ya yeye kuondoka nyumbani mwa wazazi wake bali aliyeondoka kwa furaha na shangwe kwa matarajio ya kuwa msaada kwa wazazi wake baada ya mtoto huyu kufanikiwa huko aendako na kuwakumbuka wazazi wake.
Hii ni kwa sababu, hata kwenye familia kuna watoto ambao wakati wa wao kutoka nyumbani ulipofika walipuuzia, waliendelea kuwa tegemezi kwa wazazi wao na walishindwa kutoka nyumbani kwa AMANI wakajitafutie maisha badala yake waliendelea kuwa 'mammy this' 'daddy that' waliweza kujikatisha uhai au kuingia kwenye makundi mabaya na njia mbaya hata kuharibu maisha yao baada ya wazazi wao kuachishwa kazi au kupitia changamoto mbalimbali zilizowafanya wasiendelee kuwasaidia watoto wao.
Jiulize kwa mfano ikitokea leo Taifa la Marekani likasema basi kuanzia leo tunasitisha misaada na huduma Barani Afrika kwa sababu moja mbili tatu na miongoni mwa huduma hizo zikawa mitandao ya Kijamii kama vile YouTube, Instagram, WhatsApp, E-mails, Threads, Twitter na mingine mingi, platforms mbalimbali, Software Mbalimbali, Google, Microsoft, Maduka Mtandao na kadhalika ni kwa kiasi gani Waafrika tutapotezana na kuanza kutafutana kwenye ramani ya dunia kuanzia Viongozi, Wanasiasa, Wasomi, Wanahabari, Wanamuziki, Waigizaji, na Vipaji Vingi Vingine? Hivi pia ndivyo itakavyokuwa kwenye nyanja mbalimbali zikiwemo NYANJA MUHIMU za Elimu, Afya, Uchumi, Ulinzi na Usalama pamoja na Teknolojia Barani Afrika.
Tafsiri yake ni kuwa, ili Barani Afrika tuweze kutoboa na kusimama imara katika nafasi ya UTAWALA BORA NA UWAJIBIKAJI duniani kwenye nyanja zote ikiwemo NYANJA MUHIMU za Elimu, Afya, Uchumi, Ulinzi na Usalama na Teknolojia tunahitaji kuachana kwa AMANI na Mataifa ya Magharibi na Asia Magharibi, kisha kuunga urafiki na Mataifa ya Asia Mashariki; Japan, China na Korea ambayo hayakuwahi kututawala hivyo 'mentality' na roho ya kuwategemea wao kama wazazi kwetu haipo wala kwao 'mentality' na roho ya kututawala sisi kama watoto wadogo haipo hivyo hawatasimama kama wazazi kisha kuanza kutudekeza ili wafanye kila kitu chetu badala ya kutufundisha kujitegemea na kutuachia nafasi kama yalivyosimama Mataifa ya Magharibi na Asia ya Magharibi kwa Afrika bali watasimama kama marafiki na 'business partners' ambao watatufundisha kujitegemea na kutuachia nafasi ya kupambana pamoja nao mguu kwa mguu, mkono kwa mkono, bega kwa bega tukiwa pamoja nao 'HAPA KAZI TU NA KAZI IENDELEE' usiku kwa mchana iwe mvua, jua au mawingu mpaka tutoboe kwani hakuna mafanikio yanayokuja kwa kupewa misaada na kuwa tegemezi kwa mwanadamu au taifa fulani HAKUNA bali kwa kujituma na kwa kushirikiana na waliotutangulia tukiwaweka wazazi wetu pembeni lakini tusiwasahau.
MTAJI WA KUWA BUSINESS PARTNERS NA MATAIFA YA ASIA MASHARIKI
Tofauti na tulivyokuwa kwa Mataifa ya Magharibi na Mataifa ya Asia Magharibi ambapo tulikuwa hatuchangii chochote kile kwao zaidi ya kungoja wao ndio watuletee kila kitu, kwa Mataifa ya Mashariki inatupasa tuwe na share ya 50 kwa 50 ili kweli wawe 'Business Partners' kwetu na wasiwe wazazi wala wakoloni kwetu. (Wagalatia 4:1-8)
Mataifa ya Mashariki ni Mafundi au 'Manufacturers' wazuri (VITENDO) lakini wamekuwa nyuma kwa muda mrefu duniani kutokana na udhaifu wa kukosekana kwa kiwango kizuri cha MAWAZO YA UBUNIFU (MANENO) hata kupelekea kufunikwa na Mataifa ya Magharibi, hivyo hapa jina 'Bongo' la Tanzania ndipo linatakiwa litumike ili KWA NEEMA YA MUNGU tutumie Akili Alizotubariki nazo MUNGU kuibua UBUNIFU MPYA NA WA HADHI YA JUU (MANENO) tayari kwa ajili ya Marafiki zetu Mataifa ya Asia Mashariki kuchakata BUNIFU HIZI (VITENDO); kwani Tanzania na Watanzania tumebarikiwa mawazo mazuri ya UBUNIFU (MANENO) lakini tumefunikwa na Mataifa ya Magharibi kutokana na udhaifu wetu katika kuyachakata (VITENDO) mawazo au maneno haya ili yawe. Ushirikiano huu katika UBUNIFU ndio unaitwa MNYORORO WA THAMANI WA UBUNIFU kwani hata hapo Mwanzo wakati MUNGU Anaumba Ulimwengu hakuwa PEKE YAKE bali YEYE MUNGU BABA Alikuwa Anatoa WAZO LA UBUNIFU (MANENO) KWA UWEZA WA ROHO MTAKATIFU ALIYETULIA JUU YA MAJI (Mwanzo 1:2) halafu MUNGU MWANA BWANA YESU KRISTO YEYE Alikuwa Anayachakata Kiufundi mawazo haya (VITENDO) mpaka ulimwengu wa kupendeza ukatokea. (Mwanzo 1:3) (Mithali 8:23-31) (Yohana 1:1-5); ndiyo maana MUNGU Akasema na Tumfanye mtu KWA MFANO WETU KWA SURA YETU... tafsiri yake ikiwa kwamba katika Uumbaji Hakuwa MUNGU BABA PEKE YAKE. (Mwanzo 1:26)
MTAJI PEKEE ILI TUWEZE KUWA 'BUSINESS PARTNERS' kati ya Tanzania na Mataifa ya Mashariki; Japan, Korea na China ni AKILI YA ROHONI yaani HEKIMA YA MUNGU, kwani huu ndio MTAJI PEKEE AMBAO MUNGU MWENYEWE PIA Aliutumia KUUMBA Mbingu na Dunia (Mithali 3:19-20); kama Andiko langu liitwalo MADINI YA THAMANI YALIYOFICHWA DUNIANI AMBALO KWA NEEMA YA MUNGU NIMETANGULIA KULIANDIKA HAPA JAMII FORUMS KIPENGELE CHA STORIES OF CHANGE LINAVYOSEMA.
(SoC03 - Madini ya thamani yaliyofichwa duniani)
UMUHIMU WA MNYORORO WA THAMANI WA UBUNIFU
Ubunifu ni nini?
Ubunifu ni MANENO (Innovation) na VITENDO (Crafting or Manufacturing); yaani ni kazi ya pande mbili; wanadamu au mataifa ambapo kazi ya upande mmoja ni kuchakata mawazo yaliyo ndani ya akili ya upande wa pili yatolewayo kupitia njia ya maneno mpaka mawazo haya yawe katika umbo halisi 'physically'. (Mwanzo 1:3) (Mithali 8:23-31)
Ubunifu unahitaji Pande Mbili Imara ambapo upande mmoja unatakiwa kuwa wa kutoa MAWAZO MAZURI NA MAPYA YA UBUNIFU YENYE KUTATUA CHANGAMOTO ZINAZOUKABILI ULIMWENGU (INNOVATING = MANENO) huku upande wa pili ukiwa ni kwa ajili ya KUCHAKATA NA KUYATENGENEZA mawazo haya ili yawe na kuushangaza ulimwengu (CRAFTING OR MANUFACTURING = VITENDO); hivyo Mataifa ya Asia Mashariki yanatufaa ipasavyo nasi tunawafaa ipasavyo ili KUUNGANISHA MNYORORO WA THAMANI WA UBUNIFU uliokatika duniani na kuzikabili changamoto zote barani Afrika na duniani kwa ujumla kwa kuleta suluhu za changamoto hizi.
Mfano kwa Tanzania tunaye kaka yetu Masoud Kipanya hongera sana kwake Mbunifu Huyu aliyethubutu kuchukua hatua. Mbunifu huyu, MNYORORO WA THAMANI WA UBUNIFU unamsaidia kumwongoza mwanzo hadi mwisho wa mipaka yake ya UBUNIFU, ili asije akavuka mpaka akaharibu wazo lake la UBUNIFU.
Kwa kutumia kipaji chake cha uchoraji, Masoud Kipanya anao uwezo wa kubuni gari kali kichwani mwake ambalo halijawahi kutokea duniani na kisha akalichora kama lilivyo kuanzia 'interior design' mpaka 'exterior design'. Baada ya kulichora, MNYORORO WA THAMANI WA UBUNIFU unamzuia Masoud Kipanya asiendelee na ufundi wa gari hili wala kulitengeneza kwani kazi yake ya kuandaa wazo la UBUNIFU (INNOVATION) tayari ni la THAMANI kwenye MNYORORO WA THAMANI WA UBUNIFU; na hapo ndipo mipaka ya KIPAWA chake katika MNYORORO WA UBUNIFU hivyo kazi ya kulichakata gari hili ili litoke kama lilivyo inatakiwa ifanywe na Kaka Suzuki kutoka Japan. Gari litakalotoka hapa ni lazima liwe la hadhi ya juu tofauti na Kaka Masoud Kipanya alivyoamua kumaliza vyote mwenyewe hatimaye gari limebaki kuwa maonyesho badala ya kuwa bidhaa ya THAMANI KUBWA; tatizo ni kutofuata wala kuutambua MNYORORO WA THAMANI WA UBUNIFU, kwani huenda gari lile tunaloliona na lililo kwenye kichwa cha Masoud Kipanya ni vitu viwili tofauti.
Kufanya Ubunifu Pweke ndiyo sababu iliyopelekea MNYORORO WA THAMANI WA UBUNIFU kukatika duniani kutokana na kila mwanadamu na kila taifa kutofahamu MNYORORO WA THAMANI WA UBUNIFU hivyo kutaka kila kitu upande mmoja ufanye peke yake wakati UBUNIFU hauhitaji UBINAFSI bali unahitaji ushirikiano wa pande mbili nao ndio MNYORORO WA THAMANI WA UBUNIFU. Ubinafsi katika UBUNIFU umepelekea kukatika kwa MNYORORO WA THAMANI WA UBUNIFU duniani hivyo ulimwengu kushindwa kukabiliana na changamoto zilizopo nchini Tanzania, Afrika lakini pia dunia nzima hata kupelekea mpaka leo hii ulimwengu umekosa UBUNIFU wa kupambana na changamoto zinazoukabili hivyo kubaki umeelemewa na kila aina ya matatizo na changamoto zisizo na majibu kabisa au zisizo na majibu sahihi.
Ili Watanzania, Taifa la Tanzania, Waafrika na Bara la Afrika tuweze kuwa HURU, KUWA NA UTAWALA BORA NA UWAJIBIKAJI; Njia ya MNYORORO WA THAMANI WA UBUNIFU ndiyo inayotakiwa kutumika kwenye nyanja zote kati ya Tanzania (Afrika) na Mataifa ya Mashariki yaani Japan, China na Korea zikiwemo NYANJA MUHIMU ZA ULINZI NA USALAMA, ELIMU, AFYA, UCHUMI na TEKNOLOJIA yenyewe.
UKWELI KUHUSU UPANDE WA MASHARIKI
Mashariki ni Upande ambao MUNGU Alipanda BUSTANI kisha Kumweka humo mwanadamu wa kwanza.
"BWANA MUNGU Akapanda BUSTANI upande wa Mashariki wa Edeni, Akamweka ndani yake huyo mtu Aliyemfanya." (Mwanzo 2:8)
Mashariki ni upande wenye NGUVU ZA MUNGU kwa UWEZA WA ROHO MTAKATIFU Ambazo zina UWEZO KAMA UPEPO wenye kusukuma kila bahari na kuigawanya ili wana wa Israeli (Tanzania (Afrika)) tuweze kupita.
"Musa; akanyosha mkono wake juu ya bahari; BWANA Akaifanya bahari irudi nyuma kwa UPEPO WA NGUVU utokao Mashariki, usiku kucha, akaifanya bahari kuwa nchi kavu, maji yakagawanyika. Wana wa Israeli wakaenda ndani kati ya bahari katika nchi kavu; nayo maji yalikuwa ukuta kwao mkono wa kuume, na mkono wa kushoto. (Kutoka 14:21-22)
Mashariki ndipo ilipoonekana na kung'aa; NYOTA YA BWANA YESU KRISTO Alipozaliwa hapa duniani.
"YESU Alipozaliwa katika Bethlehemu ya Uyahudi zamani za mfalme Herode, tazama, mamajusi wa Mashariki walifika Yerusalemu, wakisema, YUKO wapi YEYE Aliyezaliwa MFALME wa Wayahudi? Kwa maana tuliiona NYOTA YAKE Mashariki, nasi tumekuja kumsujudia... Nao waliposikia maneno ya mfalme, walishika njia; na tazama, ile NYOTA waliyoiona Mashariki ikawatangulia, hata ikaenda ikasimama juu ya mahali Alipokuwapo MTOTO. Nao walipoiona ile NYOTA, walifurahi furaha kubwa mno. Wakaingia nyumbani, wakamwona MTOTO pamoja na Mariamu mamaye, wakaanguka wakamsujudia; nao walipokwisha kufungua hazina zao, wakamtolea tunu; dhahabu na uvumba na manemane." (Mathayo Mtakatifu 2:1-2) (Mathayo Mtakatifu 2:9-11)
Mashariki ndipo kwenye NURU YA ULIMWENGU inayoangaza mpaka magharibi; UMEME ulioumbwa na MUNGU hapo mwanzo yaani NURU ya Mwanzo 1:3.
Tafsiri yake ni kuwa Upande wa Mashariki ndipo jua huchomoza kwanza kabla ya Magharibi, Kaskazini na Kusini.
"Kwa maana kama vile UMEME utokavyo Mashariki ukaonekana hata magharibi, hivyo ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu." (Mathayo Mtakatifu 24:27)
Mashariki mwa dunia yaani Japan, Korea na China ndipo Kampuni Kubwa kabisa duniani za KI-TEKNOLOJIA zilipo; Sony, Samsung, Tecno, Lenovo, Hyundai, Honda, Toyota, Canon, Hitachi, Nissan, LG, Panasonic, Nikon, Casio, Toshiba, Mazda, Suzuki, Isuzu, Subaru, Lexus, na nyingine nyingi.
Mashariki mwa Afrika yaani Tanzania 'Bongo' ndipo kwa NEEMA YA MUNGU Ametumiminia ROHO YAKE hata kutupa Akili ya Rohoni; yaani HEKIMA YAKE, NA MAWAZO MAZURI YA UBUNIFU (Kutoka 31:1-6) (Kutoka 35:30-35); yenye kupelekea Taifa la Tanzania kuwa msaada kwa Mataifa ya Kusini mwa Bara la Afrika kupata UHURU wa Bendera tangu enzi za Mwalimu Nyerere na sasa KWA NEEMA YAKE MUNGU TENA ni wakati mwingine wa Taifa la Tanzania kuupigania UHURU WA FIKRA, UHURU WA ROHONI NA UHURU WA MWILINI hata kuwa msaada tena kwa Bara zima la Afrika kuupata UHURU HUU.

Upvote
1