Asante mke wangu kuniletea mapacha, wadau nisaidieni kuwapa majina (yawe ya members wa JF)

MSAGA SUMU

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2015
Posts
6,661
Reaction score
21,656
NIKO SERIOUS,TENA SANA.

Hatimaye yamekuwa baada ya miezi 9 na siku kama 3 hivi,wife kaniletea mapacha wawilim, wakike na wakiume, wenye afya nzuri.

Mara ya kwanza nilifikiria kuwapa majina ya vyama viwili vikubwa vya siasa nchini lkn nilipofikiria suala la hivi vyama viwili kukosa msimamo kwenye uchaguzi uliopita kuhusu Lowassa nimeamua kuachana na huo mpango kabisa (nataka wanangu wawe na msimamo thabiti)

Kutokana na mapenzi yangu ya dhati kwa JF nimeamua kutafuta ID mbili za kufa mtu kutoka humu ndani ili niwape hawa wanangu,

Mdau majina gani hasa yatawafaa hawa mapacha wangu,maoni yenu ni muhimu sana wadau

NB:Tafadhali jina hilo lisiwe mshana jr

 
Mtoto wa kiume muite Mteghanyi Kighobo mwingine chagua mwenyewe.......
 
Huyo wa kiume muite Otorong'ong'o
 
hongera
unataka yanayoanzia na herufi gani?
nikutafutie majina makali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…