Asante Mungu kwa kutuletea Messi duniani

yitzhak

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2019
Posts
616
Reaction score
853
Huwa najiona MTU mwenye bahati kumtazama mchezaji bora zaidi kuwahi kutokea duniani

Toka anakaribishwa uwanjani na Gaucho miaka zaidi ya kumi imepita ila sijawahi kuona hata siku moja yeye akicheza vibaya,sijawahi kuona akimpa adui pasi,sijawahi kuona apige golini maratatu na akose goli

Kabla ya messi tulikuwa na Pele kama mchezaji bora wa muda wote ila messi amekuja kuharibu kila kitu

Ewe mfalme wa soka duniani nakuhusudu sana

Kwa kumuenzi messi nitamtaja mtoto wangu jina la messi amefanya makubwa

Hakuna mchezaji hata mmoja anayeweza kumsogelea messi katika kizazi hiki tulichonacho

Messi hata ukistaafu mpira kesho hakuna ninachokudai

Messi The GOAT
 
Ushabiki maandazi ameisaidia vipi nchi yake?Bora ungewaweka level Moja na Cr7 na akina zizzou
 
Mungu hawezi kuleta mtu ambaye akiwa nje ya barca hana makali, ungekua na akili timamu ungemshukuru Mungu kwa kumleta CR7 kwenye hii dunia maana CR7 tokea akiwa man united, madrid Juve mpaka kwenye timu ya taifa tunaona mafanikio yake!!
 
Ile mechi Brazil kabebwa mno
Nusu fainail UNL:Ronaldo goli 3
Result Port 3 - 0 Swiz

Nusu fainal CopaAmerica:Messi:244 dribbling,455 ndizi,chance created 56446,touches 453257,pass accuracy 45536%
Result Braz 2 - Arg 0
 
Unataka aisaidie Mara ngapi_? Huoni kafika nusu fainali? Pamoja na Brazilian kubebwa jana
Yani uzi wa kindezi huu....mess ndiyo umemshushia paragraph hivyo kashindwa hata kuisaidia timu yake ya taifa,
 
Huwezi kumweka Messi level mmoja na huyo mchezaji wa kuvizia magoli

Messi undisputed
Ushabiki maandazi ameisaidia vipi nchi yake?Bora ungewaweka level Moja na Cr7 na akina zizzou
 
Hana makali vipi? Umeangalia takwimu za timu ya taifa ya Argentina au mmekaririshwa na wachambuzi uchwara

Unajua kua messi ni mfungaji bora wa muda wote Argentina?
Mungu hawezi kuleta mtu ambaye akiwa nje ya barca hana makali, ungekua na akili timamu ungemshukuru Mungu kwa kumleta CR7 kwenye hii dunia maana CR7 tokea akiwa man united, madrid Juve mpaka kwenye timu ya taifa tunaona mafanikio yake!!
 
Reactions: Qwy
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…