Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 16,419
- 26,594
Mama Samia kaingia na staili nzuri ya kuweka mambo wazi na si kuficha ficha kama ilivyokuwa kawaida ya mtangulizi wake.
From word go mwaka 2016, uchumi wa Tanzania ulianza kutikiswa kwa matumizi mabaya ya maguvu ya kisheria ya serikali.
Takwimu sa UONGO zilianza kutolewa na ikawa chini ya sheria , ikawa kosa la jinai kuzipinga. Na mtanzania huru au taasisi huru zikawa haziruhusisiwi chini ya sheria kutoa takwimu mbadala ambazo zimefanyiwa utafiti.
Ndio maana hadi leo hatujui wagonjwa walioambukizwa au kufariki kwa ugonjwa wa COVID19, maana Magufuli alikataza kwa sheria alizotunga.
COVID ilituathiri miaka miwili iliyopita lakini kuporomoka kwa uchumi kulianza zaidi ya miaka minne iliyopita. Maduka kufungwa, kampuni kufungwa, wawekezaji kutimka, hata maslahi ya wafanyakazi kuporomoka, hayo yameingia na Magufuli.
Business confidence kwa wazawa na wawekezaji pia kukaporomoka, mitaji ikakimbizwa nje ya nchi, mashahidi benki zetu, deposits zilipungua sana. Tuwe wakweli.
Hivyo kuporomoka uchumi si vema kudai kuwa ni kutokana na COVID peke yake maana Awamu ya Tano iliukaba ukuaji wa uchumi.
Najua Mama Samia kaanza vizuri kwa kusahihisha mambo muhimu kibiashara, lakini sheria kandamizi zilizotungwa wakati wa Magufuli ni lazima zibadilishwe ili mitaji iliyokimbizwa iweze kurudi.
Kinachonitia shaka ni viongozi wale wale kina Philipo Mpango, Mwigulu Nchemba na wengine waliokuwa wanaimba kuwa uchumi unakua kwa over 7%, leo wameumbuliwa kuwa ukuaji wa uchumi umeporomoka toka 6.9% hadi 4.7% kama alivyo tangaza Mama Samia.
Watu (viongozi) wa Awamu iliyopita inabidi WATUBU ili kurudisha heshima yao mbele ya umma kwa uongo waliokuwa wanatulisha.