Asante Rais Samia kwa kuelekeza kero ya namna ya ukusanyaji kodi, Lakini sijasikia kero ya Bodi ya Mikopo wa Elimu ya Juu

Asante Rais Samia kwa kuelekeza kero ya namna ya ukusanyaji kodi, Lakini sijasikia kero ya Bodi ya Mikopo wa Elimu ya Juu

APA CHICAGO

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2019
Posts
259
Reaction score
292
Huwa sipendi kuwachosha wanajukwaa naenda moja kwa moja kwenye maada.Kama kichwa cha habari kinavyojieleza kuwa " kuna kero ya board ya mikopo ya elimu ya juu hususni sheria mpya ya mwaka 2016.

Sheria hii mhe Rais ni kandamizi kwa sababu ya mambo mawili,mosi sheria hii inatumika kuwakata wanufaika asilimia 15% hata wale waliokopa kabla ya sheria hii kupitishwa ambapo mkataba ulikuwa unatamka asilimia 8%.

Pili sheria hii imeweka retention fee kwa wanufaika wa board vilevile walionufaika 2015 kurudi nyuma retention fee haikuwepo hii pia ni uonevu kwa mtu ambaye hakuingia mkataba na board pasi kuwepo na mashariti haya.

Tatu kwanini board hawataki kuonyesha deni lote kwenye salary slip badala yake deni wanalificha hii inaweza pelekea watu kupigwa cha juu.

Kwa maoni yangu hakuna haja ya kuweka retention fee kwa fedha ambayo serikali inajua kabisa haiendi kuzalisha bali ni for consumption.

Sielewi kwanini watu waliosoma bure enzi za Baba wa taifa hayati mwalimu Nyerere wao waliamua kupitisha sheria kandamizi kiasi hiki.
Nategemea kuona loan board wakitoka hadhalani na kusema nani aliforce hii kitu kama walivyofanya wale wengine.

Mwisho kwa Unyenyekevu mkubwa kabisa nikuombe Mhe Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa awamu ya sita Samia Suluhu Hassan, itazame sheria ya Bodi ya Mkopo wa elimu ya juu ya 2016, sheria hii ni kandamizi katika taifa huru.
 
Kwani watumishi wote ndo wanadaiwa na bodi bhana.. Kwanza wengi wao waajiriwa na Diploma/certificate hayo mambo ya mikopo wala hawayajui, kama umespend pesa za watu na ajira umepata lipa pesa ya watu ili wengine nao wapate kusoma pia acha kulialia.
 
Back
Top Bottom