Asante Rais Samia kwa stendi mpya ya kisasa Mkoa wa Mbeya. Umejenga jina lako Mbeya badala ya Kizimkazi, tutasimulia Wajukuu zetu

Hiyo stand mpya unatosema ni ipi? Mabasi bado yapo stand ya zamani kama kachumba, au unazungumzia stand ya daladala ya NANENANE?
 
Tusaidie kujua barabara ya njia nne inaendelea. Maana tulio mbali na mkoa wetu tunatamani kuona yanayoendelea
 
Tusaidie kujua barabara ya njia nne inaendelea. Maana tulio mbali na mkoa wetu tunatamani kuona yanayoendelea
Nimepita hiyo barabara ujenzi umesimama, na inaoneka umesimama kwa muda mrefu Sasa....

Shughuli pekee niliona maroli ya watu binafsi yakipakia udongo uliochimbwa kwenye upanuzi wa barabara hiyo.
 
Nilipita kipande Cha Uyole - Kabwe hakuna hata kifaa kimoja cha Mkandarasi...
Watu wengine wanasema labda utaanza Tena kwenye mwaka huu mpya wa fedha(2024-2025).
 
Nilipita kipande Cha Uyole - Kabwe hakuna hata kifaa kimoja cha Mkandarasi...
Watu wengine wanasema labda utaanza Tena kwenye mwaka huu mpya wa fedha(2024-2025).
Uanze au unaendelea? Mkandarasi anaamua wapi aanze wapi asimamie au wapi afanye nini,mradi Ina km 35 Sasa unadhani Kuna kazi ambayo Kila section utaona grader?
 
Uanze au unaendelea? Mkandarasi anaamua wapi aanze wapi asimamie au wapi afanye nini,mradi Ina km 35 Sasa unadhani Kuna kazi ambayo Kila section utaona grader?
Kwa taarifa tu, Mkandarasi amekimbia kandarasi yake... Vifaa vyake vyote kavitekeleza hapo Iwambi.
 
Kazi ya ujenzi wa Stendi inaendelea Kwa Kasi 👇👇

View: https://youtu.be/Ks9p7bJDq-0?si=MAV85pQScF5_Csvl
 
Kwa taarifa tu, Mkandarasi amekimbia kandarasi yake... Vifaa vyake vyote kavitekeleza hapo Iwambi.
CHICO ni Mkandarasi mkubwa hawezi kukimbia na kapewa kazi ya Barabara ya Iringa-Ruaha NP.

Nimekwambia kazi inaendelea na juzi nilikuwa Mbeya.

Hujasikia TRA imevunja rekodi ya Mapato? Serikali imeanza kuwalipa wakandarasi madai Yao so Kaa Kwa. kutulia.
 
Hiyo ilikuwa September... saa hivi kazi imeresume....

Nawaona sasa mitaa ya Nane nane hadi Uyole....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…