Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Stand mpya ni ipi ndg? Nane nane?Wewe punguani unaishi Mbeya ya wapi ambako haijaanza kujengwa? Au unasimuliwa tuu? Nikuoneshe progress?
Nani amesema stendi Mpya imejengwa? Mada umesoma na kuelewa?Stand mpya ni ipi ndg? Nane nane?
Soma mada na ulewe sio kukurupuka tuu👇👇Hiyo stand mpya unatosema ni ipi? Mabasi bado yapo stand ya zamani kama kachumba, au unazungumzia stand ya daladala ya NANENANE?
Nimepita hiyo barabara ujenzi umesimama, na inaoneka umesimama kwa muda mrefu Sasa....Tusaidie kujua barabara ya njia nne inaendelea. Maana tulio mbali na mkoa wetu tunatamani kuona yanayoendelea
Tusaidie kujua barabara ya njia nne inaendelea. Maana tulio mbali na mkoa wetu tunatamani kuona yanayoendelea
Ujenzi hauwezi kusimama sema unaenda taratibu sana ,sababu ni zile zile miradi ya kujenga Kwa pesa za ndani ndio Huwa hivi tofauti na Mkopo.👇👇Nimepita hiyo barabara ujenzi umesimama, na inaoneka umesimama kwa muda mrefu Sasa....
Shughuli pekee niliona maroli ya watu binafsi yakipakia udongo uliochimbwa kwenye upanuzi wa barabara hiyo.
Uanze au unaendelea? Mkandarasi anaamua wapi aanze wapi asimamie au wapi afanye nini,mradi Ina km 35 Sasa unadhani Kuna kazi ambayo Kila section utaona grader?Nilipita kipande Cha Uyole - Kabwe hakuna hata kifaa kimoja cha Mkandarasi...
Watu wengine wanasema labda utaanza Tena kwenye mwaka huu mpya wa fedha(2024-2025).
Kwa taarifa tu, Mkandarasi amekimbia kandarasi yake... Vifaa vyake vyote kavitekeleza hapo Iwambi.Uanze au unaendelea? Mkandarasi anaamua wapi aanze wapi asimamie au wapi afanye nini,mradi Ina km 35 Sasa unadhani Kuna kazi ambayo Kila section utaona grader?
Wamepita Marais wengi hapa Tanzania lakini ni Rais Samia mtoto wa Ardhi ya Kizimkazi ndio ameutendea Haki Mkoa wa Mbeya kulingana na hadhi yake.
Ilikuwa ni Kilio Cha mda mrefu Kwa Wana Mbeya ambacho hakuna aliyekisikia isipokuwa huyu mwanamke Rais Samia.
Umefanya mambo mengi sana ya kuacha alama Mkoani Mbeya,miongoni mwayo ni
1. Ujenzi wa Barabara ya Tanzam njia 4
2. Ujenzi wa Mradi mkubwa wa Maji mto Kiwira
3. Ujenzi wa Barabara za lami za Mitaa km 15
4. Ukamilishaji wa uwanja wa ndege wa Songwe na kuanza kujenzi wa cold room
5. Kuanza ujenzi wa uwanja wa Maonesho ya Kilimo 8/8 kuwa wa Kimataifa
6. Pamoja na miradi hiyo mikubwa ila kubwa kuliko ni hili la Stendi kuu ya Mkoa
My Take
Mungu azidi kukupa hekima na maisha marefu uje utujengee na uwanja mkubwa wa mpira maana watu wa Mbeya ni wanamichezo mahiri.
Tutasimulia Wajukuu alikuwepo Samia aliipa heshima Mbeya 🙏🙏
Pia soma Idadi ya miradi mikubwa inayotekelezwa na Rais Samia mkoani Mbeya
View attachment 3053755View attachment 3053756
View attachment 3057257
=====
MBEYA -Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mohamed Mchengerwa amesema ujenzi wa Stendi Kuu ya Mabasi na Soko katika jiji la Mbeya vitakwenda kuongeza thamani ya Jiji hilo kwani itaboresha upatikanaji wa huduma kwa wananchi.
Ameongeza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan imetoa fedha zaidi ya Sh bilioni 30 kwa ajili ya uboreshaji wa miundombinu katika jiji la Mbeya.
Mhe. Mchengerwa ameyasema hayo wakati wa hafla ya utiaji saini Mikataba ya miradi ya ujenzi wa barabara, Kituo Kikuu cha Mabasi na Soko Kuu la Jiji hilo kupitia Mradi wa TACTIC iliyofanyika katika Viwanja vya Ndege vya zamani jijini Mbeya leo Julai 27, 2024.
Amesema ujenzi wa Kituo Kikuu cha Mabasi eneo la “Old Airport” na Soko Kuu eneo la “Sokomatola” utagharimu Jumla ya Sh bilioni 30.12 na ni imani yetu sote pasina shaka kuwa miradi hii italeta mabadiliko chanya kwa wananchi wa Jiji la Mbeya na wageni mbalimbali ambao watanufaika huduma za usafiri na usafirishaji na ufanyaji wa biashara kwani nidhahiri kuwa thamani ya maeneo husika itapanda na hivyo kusababisha ongezeko la mapato kwenye Halmashauri.
Imeandaliwa na Mwandishi Wetu
View: https://youtu.be/m1oo21ZfKI0?si=2zRCHlTtVnd3wSDh
CHICO ni Mkandarasi mkubwa hawezi kukimbia na kapewa kazi ya Barabara ya Iringa-Ruaha NP.Kwa taarifa tu, Mkandarasi amekimbia kandarasi yake... Vifaa vyake vyote kavitekeleza hapo Iwambi.
Hiyo ilikuwa September... saa hivi kazi imeresume....CHICO ni Mkandarasi mkubwa hawezi kukimbia na kapewa kazi ya Barabara ya Iringa-Ruaha NP.
Nimekwambia kazi inaendelea na juzi nilikuwa Mbeya.
Hujasikia TRA imevunja rekodi ya Mapato? Serikali imeanza kuwalipa wakandarasi madai Yao so Kaa Kwa. kutulia.
Ndio maana nimekwambia huyo Jamaa wamelipwa Sasa wako siteHiyo ilikuwa September... saa hivi kazi imeresume....
Nawaona sasa mitaa ya Nane nane hadi Uyole....
Kazi ya ujenzi wa Stendi inaendelea Kwa Kasi 👇👇
View: https://youtu.be/Ks9p7bJDq-0?si=MAV85pQScF5_Csvl
Hawa sio CHICO ,Hawa ni Wakandarasi wazawa wanajenga Stendi na Soko Kuu.Niliwaona wakati wa Wasafi Festival....