Asante sana kunguru, kisicho rizki hakiliki

Miss Natafuta

JF-Expert Member
Joined
Sep 16, 2015
Posts
27,031
Reaction score
49,928
kweli nimeamini ,kisicho riziki hakiliki. niliotesha mipapai yangu miwili hapa nilipopangisha maana kuna uwanja mkubwa.yote ikaota tu vizuri .mpapai mmoja niliuotesha kwa nyuma mwenye nyumba akasema ukatwe maana wba za kuanikia nguo na hapo mpapai ulikuwa ushakuwa tu mkubwa.

Ukabaki mmoja nimeutunza wee nakumbuka ulipata ugonjwa nikaja hadi jf kuomba ushauri.nikatumia tsh 50 kuutibu na kumleta mtaalamu.kweli Mungu ni mwema mpapai ukakaa vizuri ukatoa matunda sio ya sport sport mara paap mwenye nyumba kila mara anafata mapapai,au anamuagiza kijana wa usafi kuja kuchukua.yaani nimekula hapo papai moja tu . Mi wala sikumind kiivo japo niliona sio sawa.

mara paap kunguru wakaingilia papai likiiva kidogo tu wanalila.wakaona kwa vile kunguru wanayala basi wayatoe mapema yakikomaa. wakawa wanayatoa mabichi flani.kunguru nao wajanja sasa hivi wanayala mabichi wametoboa papai zote hazifai .nasikia watakata tu huo mpapai.sijui nitanunua lini kwangu jamni Mungu saidia japo naogopa bomoa bomoa
 
Sijaelewa ngoja nikojoe nikalale mambo mengine yawakubwa haya
 
Pole sana, uoteshe sebuleni, kwani we utajenga sehemu ambayo haijapimwa na hauna hatimiliki???
Pole aisee.....
 
Umezunguka sana ila tuu tumekusoma
 
Pole rafiki yangu!
Ipo siku na wewe utamiliki nyumba yako na kupanda mime ya kila aina unayoitaka na hata kufuga mifugo yako
 
kumbe mpenzi wa papai ehe safi sana ila unamaana yako kupenda kula papai.
 
Popo ndo wanakula sana mapapai...njoo kwangu uwe mama mwenye nyumba
 
Ahhh nitayapanda ili uwe unakuja kuyala kwangu, hata hivyo kwakuwa ulisema unakuja basi ntakuandalia yakutosha sawa, ukitaka ya kubeba unambie mapema nitakuandalia ya kufungasha.
 
Siku ukijenga na kuwa na kwako, usisahau kumpa YULE Kura ya NDIO....
 
Hapa sijaelewa kitu kwa kweli

Mkuu mtoa uzi una maanisha mpapai huu huu naoujua mimi au umetumia tafsida?

Kunguru hawa hawa naowajua mimi au wapi mkuu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…