eliakeem
JF-Expert Member
- May 29, 2009
- 17,214
- 15,853
Miaka mingi iliyopita, watu wengi walifikiri kwamba MArekani anapigana vita ili kulinda amani, demokrasia au kuwaokoa watu/nchi fulani kutoka katika ukandamizaji. Ilijipambanua kwamba yenyewe haitangulizi masirahi yake, badala yake inapambania utu, ubinadamu, haki na mali za wale wote wanaoonewa.
Sasa kinachoendelea Ukraine ni tofauti kabisa. Ukweli ni kwamba iliingia kuisaidia Ukraine siyo kuilinda dhidi ya uvamizi wa Urusi, bali kama muwekezaji yeyote ambaye aliona fursa ilioko mbeleni. Kwamba vita inayoendelea katika taifa hilo, siku za usoni itakuwa ni neema kwa Marekani.
Imekuwa kweli. Sasa marekani kwa uwazi kabisa anamdai Ukraine kwamba waingie mkataba wa makubaliano ya kuwa Marekani itanufaika na madini muhimu yanayopatikana humo. Haya yote yalikuwa yanafanyika miaka mingi sana huko nyumba.
Lakini yalikuwa hayawi wazi kama ilivyo sasa. Ndiyo maana nasema na kurudia tena, TUNAKUSHUKURU SANA TRUMP KWA KUYAWEKA HAYA WAZI.
SASA TUNAJUA FIKA KABISA KWAMBA HAKUNA KITU CHA BURE HAPA CHINI YA JUA.
www.bbc.com

Kwanini Ukraine inajadili mkataba wa madini na Marekani? - BBC News Swahili
Waziri mmoja anasema kwamba "majadiliano yamekuwa yenye tija, huku karibu maelezo yote muhimu yakiwa yamekamilika."