pole sana dada unayejiita usiye na bahati (unlucky)!
mi naona hapo ndipo penye kosa kubwa. hivi ni bahati gani unayoamni kuwa huna na unafikiri ungekuwa nayo mambo yako yangeenda vizuri?
napenda kukuambia kwa uwazi kuwa duniani hakuna bahati, ila kuna BARAKA NA FURSA. baraka hutoka kwa Mungu na ni matokeo ya kumcha Mungu na neema na rehema zake kwetu wanadamu. fursa hutokana na circumstances au mazingiza. ikishindwa kusoma mazingira yako na kuzibaini fursa zilizomo na kuzifanyia kazi, hutafanikiwa katika jambo lolote na ndio matokeo ya kujiita usiye na bahati na kumbe ulishindwa kuzibaini fursa na kuzitumia. hapa huwa tunaomba uzima tu, manake hata mtu asiye mcha Mungu akituma vizuri fursa zinazojitokeza hufanikiwa pengine hata kuzidi baadhi ya wacha Mungu!
kwa case yako, nakuona humchi Mungu sawasawa (rejea maelezo yako mwenyewe jinsi ulivyoelewa na jinsi unavyoyakabili majaribu kwenye ndoa yako). lakini hata kama humchi Mungu lakini unazo fursa amabazo ukiamua kuzitumia zinaweza kukusaidia. unasema huna uhuru, lakini umeweza kupata access ya internet na kusajili ID hapa, umeleta mada na unafuatilia mjadala na kujibu hoja! je hapo huoni fursa? je fursa hii ya kuwa connected umeitumiaje?
umeshauriwa na wengi kujitafutia cha kufanya, unasema mumeo hakuruhusu kutoka, hivi unajua wanawake wengine wanapambanaje na maisha? mbona akina mama wana mbinu nyingi sana, we unabadilishana nao mawazo juu ya nini ufanye, au we kwa kuwa umeolewa, basi unataka maisha yakuendee vyema kupitia mume? ukiona hayako unavyotarajia unasema huna bahati na kila ukipata fursa unaitumia kulalamikia tabia ya mwenzio? nyanyuka sasa (hata kama ni wakati akiwa kazini) jichanganye na akina mama wenzio walio karibu mshauriane kuhusu namna ya kukabiliana na maisha. usiwafuate wanaoendesha ma-VX, ma Rav-4 nk, bali wafuate wajane, aliotalikiwa na wengine wanaojua kukabili maisha katika hali kama hizo,hao ndio watakaokupa msaada kwa sasa. waulize taratibu, wao wanawezaje kushinda na kuishi kwa amani?
pia nakushauri, ufute kabisa mawazo ya kutoka nje ya ndoa au kugawana naye watoto kwa namna yoyote ile. usiogope kuhusu kuwa atawachukua, hayo mambo huamriwa na vyombo vya sheria na si mwanaume. uamini kuwa huyo ndiye mumeo wa kufa na kuzikana na usiache hata siku moja kuiombea familia yako na ujitahidi kuongea naye kwa hekima kubwa na upole hasa ukimwomba mjadili na kupanga maisha pamoja. hata kama ana dharau na mkali anakupiga mara kwa mara, hakikisha moyoni mwake unaweka chapa ya neno la hekima na upendo ili siku akirudiwa na fahamu zake, ajue ubaya wa hayo anayokutenda. usipoacha alama ya wema, hekima na subira moyoni mwake, hata kesho akirudi kwenye hali ya kukuheshimu, hataona alipokosea. hiii ndiyo maana Bwana wetu Yesu akatuambia TUUSHINDE UBAYA KWA WEMA!
mwisho nakupa pole kwa hayo unayopitia, fahamu kuwa Mungu anakupenda sana na mbele yako amekuwekea baraka na fursa, ukizitumia kwa hekima na shukrani, yeye ni mwaminifu hatakuacha katika majaribu yako.
tulihimidi jina la Bwana kila wakati