Asanteni Simba SC kwa kumsikiliza Maoni yetu kwa Kuachana na Msaliti Inonga, sasa tunasubiria 'Thank You' ya Msaliti mwingine Chama

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Hawa Wachezaji Wasaliti Wawili wametuumiza pakubwa dhidi ya Washamba na Malofa fulani hivi wa Kariakoo 'Twiga Street' ndani ya hii miaka miwili mitatu.

GENTAMYCINE ambaye ni Mstaafu Tukuka wa Michezo Michafu ya Ligi Kuu ya Tanzania baada ya kuwepo katika Shughuli hiyo miaka ya 2011 hadi 2013 nilipiga mno Kelele hapa Jamiiforums kuwaonya Uongozi wa Simba SC na wana Simba SC juu ya Hujuma na Usaliti unaofanywa na Viongozi Virusi baadhi na Wachezaji Waandamizi wa Kigeni ( wakiongozwa na hawa Watajwa Wawili ) na Wazawa wakiongozwa hasa na Kipa Aishi Manula ila wengi kwa Makusudi au Dharau tu juu yangu Mwamba wa Soka la Bongo Jamiiforums nzima hawakutaka Kunielewa japo najua sasa Wananielewa na Watanielewa Mzanaki na Myao Mimi.

GENTAMYCINE nimefurahi sana kusikia Simba SC imeachana rasmi na Beki Henock Inonga na sasa nataka upesi mno Uongozi wa Simba SC uachane pia na Mchezaji Clatous Chama kwani Binafsi kama mwenye Uchungu na Simba SC yangu SIMTAKI na SIMPENDI kabisa kutokana na UNAFIKI na USALITI wake huku akiwa ndiyo Kinara wa Kuwagawa Wachezaji Kambini.

Na wala msiogope Yeye kwenda upande wa Pili kwa Rafiki yangu mkubwa hapa Jamiiforums Bila bila ila nawahakikishieni akienda huko naenda Kumpiga Pini ya maana ya ama apate Majeraha ya Kudumu au muda wote tu akivaa Jezi ya hiyo Timu awe anajambajamba tu au namvimbisha Kende ( Pumbu ) kama alivyofanyiwa Morisson au namtupia Jini Farakanisha na huko anakoenda Kutwa tu atakuwa Anafarakana na Wenzake hadi watamchoka na hatocheza kabisa.

Nilimuonya mno Kipa Manula kupitia Kiongozi mmoja Serikalini ambaye ni Mshabiki mkubwa wa Simba SC na Rafiki yake juu ya Usaliti na Hujuma kubwa aliyotufanyia Aishi katika zile Gongo Tano Moko Umiza za mwaka Jana zinazoniumiza hadi sasa akadhani Natania ila sasa Kinachompata sasa ( japo anahangaika mno kwa Waganga ili apone ) anakijua na mwambieni hiyo Pini imepigiwa Congo DR na Fundi Mmoja Hatari na akitaka itolewe akiri kwa wana Simba SC wote Duniani kuwa mwaka jana alishiriki 100% katika Hujuma ya zile Gongo Tano Moko Umiza kutoka kwa Washamba na Malofa fulani wa Kariakoo.

Uongozi wa Simba SC mkishamalizana na Chama na baadhi ya Wachezaji Wazawa wasio na Viwango ila Uchawi wao tu ndiyo Unawabakisha hapo Simba SC mniambie ili niwapeni muongozo wa kuifanyia Simba SC yetu Tambiko Kubwa kama ambalo alikuwa akilifanya miaka ya nyuma ya Mafanikio yetu Marehemu Mzee Bamchawi kisha mtawaita wale Wataalam Wawili yule Bibi wa Kikwajuni Zanzibar na yule Mtaalam wa Morogoro waunganishe Nguvu zao kwa Kuisafisha Klabu Kiutaalam kuanzia katika Viwanja vyetu vya Mazoezi na hasa kwa Wachezaji na hakikisheni kila Mchezaji mnayemsajili Simba SC awe anajua haya Masuala yetu ya Utamaduni wa Mwafrika ( Ndumba Ndumba ) na ambaye atasema hataki achaneni nae au Mrogeni upesi ili Akili yake ikubali. Soka la Afrika bila Ndumba halinogi na wala haliendi Kudadadeki.

Baada ya Kunifurahisha kwa Kuachana rasmi na Msaliti na Mnafiki Beki Henock Inonga sasa GENTAMYCINE nawaahidi wana Simba SC kuwa narejea Kunipigania na Kuishauri Simba SC yangu ila hakikisheni Mkutano Mkuu wa Dharula unafanyika kabla ya Ligi Kuu kuanza ili tumfukuze Msaliti mkubwa Mwenyekiti Murtaza Mangungu.

Hunipendi na hunikubali kabisa GENTAMYCINE kwa CHUKI BINAFSI zako, USHAMBA wako, WIVU wako kwa UMAARUFU wangu mkubwa hapa Jamiiforums, kwa ROHO MBAYA yako ya KURITHI na ya KISHETANI na kwa KUTESWA na NYOTA YANGU KALI kutoka kwake MWENYEZI MUNGU ALIYONIBARIKI / ALIYONITUNUKU nayo tokea ANANIUMBA acha Kusoma Mada zangu kwani Sijakulazimisha na wala sijakushikia Mtutu wa Bunduki Usome au uwe Unanisoma hapa Jamiiforums.

Mimi ndiyo GENTAMYCINE "Purely Talented, Charismatic Fella, Game Changer and Entertainer" na hakutotokea mwingine wa kufanana nami.

Nimemaliza.
 
Simba inazidi kuteketea pasi na kujua shida hasa ni viongozi ama wachezaji au ni Yanga Bora kuliko wao
Msimu mpya unazidi kusogea kwa Kasi huku team ikifanya usajili konki wa Kailima Ramso ili kukabiliana na changamoto za msimu ujao
Mshindani wa Yanga atakuwa SBB na Azam
 
Katika vitu simba itajutia mwaka ni CCC km silaha kuiacha iende yanga kila akiwa uwanjani atawaumiza na hii itafanya simba kupoteana sana ligi ya mwaka huu. Kusajili mchezaji ni kingine na mchezaji kufanikiwa ni kuingia kwenye mfumo ni lingine kbs. CCC alikuwa sehemu ya mafanikio yote ya simba kwa miaka hii ya karibuni.

Na uhakika simba na MO watafarakana sana MO ameingia kwenye mfumo atajua alichemka kumwacha baada ya kuharibu na no way back to remedy.
 
Chama huyu mpira umeshaisha hata hao viongozi wa Yanga waliomsajili kwa hela ndefu ni siasa chafu za kufikiri wanaikomoa Simba,kabla hiyo miezi sita kwisha mtaanza kumtupia chupa za maji uwanjani.
 
"Mimi kama kocha wa makipa sikutaka Manula acheze, lakini Kocha Mkuu akasema ni lazima acheze, lakini pia nilimfuata Manula nikamwambia unajua afya yako ilivyo hairusu kucheza".- 2023/2024 Goal Keep Coach

Sasa sijui Ni Mangungu au Jaribu tena ndo aliforce kama Jogoo ili Manula acheze hiyo siku! Huyo ndo Msaliti namba moja wa Timu!
 
Nikipata uwezo wa kuishawishi Simba kumfukuza mwanachama, wewe GENTAMYCINE utakuwa wa Kwanza. Atafuatia Kigwangalla namalizia na Mwina Kaduguda. Hamna cha maana Simba!
 
XS§ABkA¿SOCATbhrT¿bTrrF¡VoCAZSW§a§AtCSISÑ@ÆIkOkAZiKUCY¡?SMkekgQSAFQCW§AFQCARÑiCÑKiSAVSÄKWoSgQCC¡?SEkAD2Ø'E¡VoKÑsKA&
 
Kijana tuliza wenge
 
😂😂😂😂😂💦💦💦💦
Nimecheka mpaka machozi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…