Asanteni wote kwa ushauri wenu, Nimefanikiwa kupata ujauzito

Asanteni wote kwa ushauri wenu, Nimefanikiwa kupata ujauzito

Xian

Senior Member
Joined
Mar 24, 2014
Posts
127
Reaction score
42
Habari wapendwa,

Nakumbuka ilikuwa tarehe 14 ya Julai mwaka huu nilivyofanya vipimo baada ya kukaa muda mrefu bila kupata ujauzito, nilienda hospitali kubwa kama tano hapa Dar na nilionana na madaktari bingwa wa magonjwa ya wanawake tofauti tofauti ila wote majibu yao yalikuwa sawa kuwa sitaweza kupata ujauzito kwa njia ya kawaida, labda nijaribu kupandikiza.

Kiukweli niliumia sana na nilikuja kuomba msaada wa mawazo hapa, nawashukuru wote waliovaa uhusika na kuumia pamoja nami pia nawashukuru hata wale walionitolea maneno mabovu.

Basi, baada ya kuleta hapa nilitajiwa dawa mbalimbali ila niliona nianze na dawa ya dada mmoja ambaye yuko Singida kwa kuwa ilikuwa ni chakula tuu huyo dada nakumbuka jina lake ni Hornet, toka mwezi wa saba nilivyotumia ikawa kimya nikakata tamaa. Mwezi huu wa Novemba ndiyo nimegundua kama mimi ni mjamzito.

Julai nilitoka machozi ya uchungu na Mungu amenifuta machozi hayo na kunitoa yenye furaha, nawashukuruni wote kiukweli mlikuwa wengi siwezi kutaja majina ila yaani nimekuwa kama sijielewi kwa furaha, naomba muendelee kuniombea nifike salama safari hii yaa kuelekea kuwa mama.

Mungu awabariki sana dada Hornet ,NITAKUAFUTA KESHO KWENYE SIMU.
 
Last edited by a moderator:
Sijakuelewa! Mimba kakupa mtu au dawa? Mi naona mshukuru mungu na huyo aliyekushughulikia. Otherwise kama nawe upo kibiashara maana naona kama promo. Mtu akusaidie tatizo kama hilo halafu mbio unakuja kuandika hapa halafu kesho ndio umpigie? Hopeless!
 
Shosti niinbox mwenzako bado nina msiba huu ndg yangu bado sijafanikiea pliz tuwasiliane kwa inbox unisaidie na mie pliz

Usiseme ivo huo sio msiba. Maneno huumba ujue jamiif
 
Last edited by a moderator:
Hongera sana mdada Mungu ni mwema, achana na hao wanaokubeza, hawajuai mauchungu ya kukosa mtoto
 
Hongera sana mdada Mungu ni mwema, achana na hao wanaokubeza, hawajuai mauchungu ya kukosa mtoto
yaani hawajui hiki kitu ukisikie kwa jirani tuu hata hivyo itauma, hili jambo linaumiza sana
 
Sasa kama kilichokusaidia ni siri, unakuja kusema ili wewe ufuatwe inbox ama yeye ndo afuatwe? Hebu ondoa promo zako hapa na wewe!
 
Hongera sana, anza na kumshukuru sana Mungu, mpende na kumheshimu sana mumeo, yapuuze kabisa mawazo hasi ili uilee mimba yako ukiwa na peace of mind, tazama na kusonga mbele.
 
siko hapa kwa promo na yeye alinitajia inbox na kama hukusoma hicho kitu huna haja ya kuchangia nadhani walio nisaidia wanajielewa, tafadhani nimekuja kushukuru sikuja kuharibiwa furaha yangu

Ok mumie hongera sana na kama ni chakula ulitajiwa tuambie na sie au masharti yake hautakiwa kusema kwa mtu?
 
Sasa kama kilichokusaidia ni siri, unakuja kusema ili wewe ufuatwe inbox ama yeye ndo afuatwe? Hebu ondoa promo zako hapa na wewe!

nina imani wau kama nyie pia nimeshawashukuru hapo juu
 
Ok mumie hongera sana na kama ni chakula ulitajiwa tuambie na sie au masharti yake hautakiwa kusema kwa mtu?

hakunipa masharti ni kitu ambacho alivyoniambia hata mimi ni dharau ila nilijipa moyo tuu ni maini robo na nyama ya ng'ombe sehemu ya nundu iliyojaa mafuta unapika pamoja bila maji coz maini yatatoa maji nundu itatoa mafua itaiva then kuna dawa ya kimasai jina niliandika kwenye diary nikiisoma nitakuandikia unachananya unakula baada ya siku 15 unarudia tena na inakuwa basi
 
Hongera sana, anza na kumshukuru sana Mungu, mpende na kumheshimu sana mumeo, yapuuze kabisa mawazo hasi ili uilee mimba yako ukiwa na peace of mind, tazama na kusonga mbele.

asante sana kwa kuendelea kunitia moyo
 
hakunipa masharti ni kitu ambacho alivyoniambia hata mimi ni dharau ila nilijipa moyo tuu ni maini robo na nyama ya ng'ombe sehemu ya nundu iliyojaa mafuta unapika pamoja bila maji coz maini yatatoa maji nundu itatoa mafua itaiva then kuna dawa ya kimasai jina niliandika kwenye diary nikiisoma nitakuandikia unachananya unakula baada ya siku 15 unarudia tena na inakuwa basi

Asante sana ngoja niifadhi haya maandishi yako yanaweza kunisaidia au kuwasaidia wenzangu siku za usoni
 
Back
Top Bottom