Asasi za kiraia zaiomba CCM ikubali, tume huru ya kuchunguza kupotea kwa raia

Asasi za kiraia zaiomba CCM ikubali, tume huru ya kuchunguza kupotea kwa raia

Bagamoyo

Platinum Member
Joined
Jan 14, 2010
Posts
32,522
Reaction score
37,398

Asasi Za Kiraia (AZAKI) zaidi ya 300 nchini zimewasilisha mapendekezo kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), zikitaka kuundwa kwa tume huru ya kiraia kuchunguza matukio ya utekaji na kupotea kwa watu, pamoja na serikali kusaini mikataba ya kimataifa ya kulinda watu dhidi ya kupotezwa kwa kulazimishwa.

Kupitia Mratibu Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Wakili Onesmo Olengurumwa, AZAKI hizo zimesema kuwa mapendekezo hayo yanahusisha pia hatua za haraka kabla na baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu, ikiwemo kukomesha vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu, kulinda uhuru wa vyombo vya habari na kuhakikisha mazungumzo ya kitaifa yanafanyika kwa ajili ya maridhiano na umoja wa kitaifa.

Mapendekezo hayo ambayo yamekabidhiwa Oktoba 22, 2025, katika makao madogo ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Lumumba, AZAKI zimeitaka serikali kuimarisha mazingira huru ya kisiasa na kijamii ili kuhakikisha Asasi Za Kiraia, vyombo vya habari, na vyama vya siasa vinafanya kazi bila hofu, sambamba na kurejesha imani ya wananchi kuelekea uchaguzi mkuu.

Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, John Mongella, amesema chama hicho kinatambua mchango mkubwa wa Asasi Za Kiraia katika kuimarisha demokrasia, haki za binadamu na utawala bora nchini.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara John Mongella ameahidi kuwa CCM itaendelea kushirikiana na wadau wote kuhakikisha hoja zinazowasilishwa na Asasi Za Kiraia zinachukuliwa kama fursa ya kujenga taifa lenye umoja, amani na haki sawa kwa wote
 
1761180101644.jpeg
 
Back
Top Bottom