Pdidy
JF-Expert Member
- Nov 22, 2007
- 57,951
- 32,619
Asha Baraka ajitosa ubunge Kinondoni
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC), Asha Baraka, ameingia matatani kwa kudaiwa kuanza kufanya mikutano ya siri na wajumbe wa Tawi la Minazini, kwa lengo la kujitafutia uungwaji mkono wa kugombea ubunge wa Jimbo la Kinondoni, katika uchaguzi mkuu ujao.
Taarifa zilizoifikia Tanzania Daima Jumatano, zinadai kuwa mjumbe huyo ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya ASET, ambao ni wamiliki wa bendi ya muziki ya Twanga Pepeta, amedhamiria kukutana na viongozi wa matawi yote na kutoa posho kwa baadhi yao ili kufanikisha azima yake.
Katika kikao kilichoketi juzi, inadaiwa kwamba Asha alifanya mkutano na viongozi wa CCM Tawi la Mnazini, kwa lengo la kuwapongeza kwa ushindi uliopatikana katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika hivi karibuni, sambamba na kujipigia debe la kuwania kiti hicho kinachoshikiliwa na Mbunge wa Jimbo hilo la Kinondoni, Idd Azzan.
Tanzania Daima Jumatano iliwasiliana na mmoja wa wajumbe aliyekuwapo katika mkutano huo, ambaye hakutaka jina lake liandikwe, alisema kuwa ni kweli alihudhuria kikao hicho na kupewa posho, lakini hakufahamu kama ilikuwa ni kwa ajili ya kikao au ilitolewa na mjumbe huyo.
Hata hivyo, mjumbe huyo hakusita kubainisha kuwa hatua ya Asha kukutana na viongozi hao, inaonyesha wazi dhamira yake ya kuwania kiti hicho kinachotarajiwa kuwa na upinzani mkali ndani na nje ya CCM.
Mikutano hiyo ni endelevu kwa Asha Baraka katika matawi yote ya Kinondoni, amepanga kuonana na wajumbe katika kujadili mustakabali wa CCM kwa Jimbo la Kinondoni, katika kuweza kuchota wajumbe watakaofanikisha mpango wake, alisema mmoja wa wajumbe waliohudhuria kikao hicho.
Aidha, chanzo kingine kimeidokeza Tanzania Daima Jumatano kuwa Asha hajaanza hivi karibuni mikutano yake hiyo, bali mingine amekuwa akiifanya kinyemela.
Asha anatumia kila njia ya kuwafikia wajumbe kujiweka imara, ili atakapotamka hadharani nia yake hiyo awe na uungwaji mkono wa watu wengi zaidi, kilisema chanzo cha habari.
Akizungumzia suala la posho na vikao, Asha Baraka alikiri kukutana na wajumbe hao na kukanusha kwamba hafanyi kampeni ya kugombea ubunge mwakani, bali ni kukijenga chama na kupongezana kwa ushindi walioupata.
Aidha, alisema kukutana kunasaidia kujua matatizo ya tawi hilo, kwa kuwa hakuwapo kwenye kipindi cha uchaguzi wa serikali za mitaa.
Hata hivyo alisema sababu ya kufanya mkutano katika tawi hilo ni kutokana na historia yake ya kukulia katika eneo hilo, sambamba na kuanza harakati za siasa akiwa Minazini, hivyo si rahisi kwake kusahau nyumbani.