Asha Baraka nakuchukia sana

Acha kuchafua Majina ya watu Ndugu , Unadhani huyo Asha kumiliki Bendi ndiyo kigezo cha Kujaa Mapesa ?? Hata yeye anashida zake anashindwa kuzitatua lol ....Wabongo kwa Kulalamika tupo nambari moko !:A S 13:
 
Unaweza kumsaidia mtu baki ukamuacha ndugu yako na maradhi? Ivi unajua Asha na Amigoras ni ndugu?

Ni kweli mkuu sokwe Asha na Amigo ni ndugu? Hebu fafanua kidogo?

Ni kweli Una uhakika Asha alikuwa na Pesa ya kumpeleka Amigo India?

Wewe ulifanya nini kuhakikisha Amigo anakwenda India?
 
Last edited by a moderator:
Unaweza kumsaidia mtu baki ukamuacha ndugu yako na maradhi? Ivi unajua Asha na Amigoras ni ndugu?

Sasa ugomvi wa ndugu we unakuhusu nini? Si uache wenye familia yao wasuluhishe? Mambo ya familia yana mengi ukute hata huyo marehemu alikataa msaada wa ndugu yake vile vile!
 

Wewe sokwe huyo jamaa kwa miaka yote hiyo aliyoajiriwa na ndugu yake alikua halipwi? Hilo la kuajiriwa tu na ndugu kwa miaka 18 unaliona dogo? Si alimpa hadi uongozi wa bendi yule? Hilo nalo dogo? Wewe ulimpa nini marehemu?
 

asha mtu wa visasi sana anaonekana
 


Sasa mbona umemkomalia Asha pekee si mgechangishana ndugu wengine?

Kwani hiyo miaka 18 alikuwa halipwi?

Huwezi kumpangia mtu amsaidie nani wakati ni hela zake.

Mtegemea cha nduguye hufa maskini,upo?
 
Kwani mtu gani hapa duniani ataishi milele? Kila mmoja anakifo chake. Mbona rais wa Zambia kapelekwa UK, na bado kafaa. Ikifika imefika jamani. Lawama hazina tija mleta mada.
 
Sasa hapa wamueleza Asha au sisi walimwengu!?


du nmecheka nusura nigongane na mtu. watu wengine bwana ndio yalee una chuki na mama/baba mkwe halafu unamtusi mtoto wako ulompa jina la babu/bibi yake matusu ambayo hayaendani na mtoto kumbe unampasha mkwe
 
Msaada ni hiari, sio shuruti.

Huwezi kumchagulia mtu wa kumsaidia.

Kutomsaidia mtu sio dhambi.

Ukimchukia hutafaidika na chochote.

Bahati mbaya sana kwako kuna wengine wanampenda

RIP Amigolas. sote tuko njia moja. Pamoja na Asha Baraka.

Na ni kweli watu waache uswahili kumsaidia mtu sio lazima na pia huwezi jua huyo Asha kama alikuwa anamsaidia marehemu,pia ikumbukwe hata Asha nae kuna wakati anaishiwa,wa kulaumiwa ni serikali yetu ambayo imezifanya hospitali zetu zisiwe na uwezo wa kutoa matibabu bora,na sisi wenyewe ndio kila kukicha tunaichagua hii serikali ya CCM,kulikuwa na Dr bingwa wa magonjwa ya moyo na alikuwa nahospitali yake hapa hapa Bongo ,jamaa wakamchanganya hadi kajifanyia akiwa masikini.Tuna madktari bingwa wa haya magonjwa hapa hapa TZ lakini hawana vifaa ila fedha ya BMK zinapatikana.
Kwa hiyo tusimlaumu dada Asha ,sote tu wapita njia,tupo kwenye foleni.
 
Hata kama angemsaidia matibabu unadhani yule angepona na kale kaugonjwa kake kale?
Siku zote unatakiwa utoe pesa/michango baada ya mtu kufa maana ye kasepa hana chake tena sio kwa mgonjwa,ndo maana waswazi wakasema"hujafa hujasifiwa"

Sio ugonjwa wa moyo tena ,mbona makubwa.
 
Watu mnapenda kulaumu, unauhakika gan kama Asha alikuwa anajua kwamba marehem alikuwa mgonjwa?Unauhakika gan kama alikuwa na hela ya kumpeleka India?
 
Kwani mtu gani hapa duniani ataishi milele? Kila mmoja anakifo chake. Mbona rais wa Zambia kapelekwa UK, na bado kafaa. Ikifika imefika jamani. Lawama hazina tija mleta mada.

UK wameenda wng, wakarudi ndn ya boksi!
 
Sasa ugomvi wa ndugu we unakuhusu nini? Si uache wenye familia yao wasuluhishe? Mambo ya familia yana mengi ukute hata huyo marehemu alikataa msaada wa ndugu yake vile vile!

Kasema hivi: Mtoa uzi, Asha na Marehemu wote ni ndugu! Yaan mtoa mada na Asha na Amigo ni ndugu!
 
Hapa Sokwe hujafikiria kama binaadamu....malalamiko yako hayana msingi wowote.

Na unaposema Asha alimsaidia mtu baki akamuacha ndugu yake...hiki ni kioja, huyo Mungu unayemshtakia kwake yeye hajui kama kuna ndugu baki na ndugu ndani...kwake ndugu ni ndugu, hebu ujifanyie tathmini kama kweli unamjua Mwenyezi Mungu.

Kesho Misanya Bingi mambo yake yasipoenda sawa utambwatukia Mzee Mengi kwa kuwa tu Misanya alifanya kazi IPP ? je ni Amigo peke yake ndiye aliyekwishafanya kazi kwa Asha ?....na wengine je hawana stahili hizo ? huyo Asha atayaweza wapi ? badala kuilaumu serikali yako kukosa hizo huduma bora unahamishia hasira kwa Asha.

Unavyosema Asha ni mbaya wewe tunakujua wapi tuone kuwa ni mwema unayepaswa kumuona Asha ni mwema ? nijuavyo mbaya pia humuona mwema mbaya kwa maslahi na tafsiri zake binafsi...kama wewe ni Singa singa na Asha ni Kafulila basi Asha atakuwa mbaya tu kwako, hatuna msaada kwa hilo ewe Sokwe.

Kama unasema Asha ni ndugu wa Marehemu ni dhahiri kuwa wewe usiye ndugu hujui Marehemu alikuwa anaugua nini, hujui daktari aliongea nini na ndugu wa marehemu kuhusu ugonjwa wa Marehemu...sasa hebu kafanye homework zako vizuri uje tena ueleweke unataka kusema nini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…