Asha Mkwizu Hauli-Na kesi ya kumuua hawara wa mumewe

Asha Mkwizu Hauli-Na kesi ya kumuua hawara wa mumewe

Mzee Mtambuzi, heshima mbele mkuu.

Nina swali moja. Hivi unajikita tu katika kutuletea kesi zilizotokea Tanzania na zinazowahusu Watanzania au hata za kwingine ili mradi ziwe ziliwahi kukamata nadhari ya watu?

Nimeuliza kwa sababu kuna kesi kama zile za O.J. Simpson na Clara Harris ambazo zote zilihusu mambo ya mapenzi na ambazo simulizi zake zinasisimua sana.
 
Mchambuzi, je unaonaje ukiandaa pia vipindi vya TV kama wafanyavyo kwenye discovery channels. Au Tanzania hatuna wataalamu wa kuandaa vipindi kama hivyo? (reconstruction/dramatisation of what happened). Hivi watangazaji wa zamani kama akina Kipozi si wanaweza kutuandalia vipindi kama hivyo wakauza kwenye local channels zetu?
 
Mchambuzi, je unaonaje ukiandaa pia vipindi vya TV kama wafanyavyo kwenye discovery channels. Au Tanzania hatuna wataalamu wa kuandaa vipindi kama hivyo? (reconstruction/dramatisation of what happened). Hivi watangazaji wa zamani kama akina Kipozi si wanaweza kutuandalia vipindi kama hivyo wakauza kwenye local channels zetu?

Wazo lako ni zuri sana, lakini tatizo ambalo mimi naliona ambalo linaweza kutukwamisha ni kupata ushirikiano wa Polisi. Nakumbuka nilikuwa na wazo la kutaka kuandika habari za kiuhalifu wakati fulani na nilikwenda pale makao makuu ya Polisi jijini Dar ili kupata takwimu za uhalifu ki-mkoa na kitaifa.........Nilipigwa dana dana mpaka nikaishiwa na nguvu, ilikuwa kila nikienda idara hii naambiwa sio nenda idara ile, na nikienda idara hiyo naambiwa nirudi idara ile............. Mpaka nikachoka nikaamua kuachana na wazo hilo.

Hata hivyo bado najaribu kutafuta ushirikiano na wadau wengine ili kama ikiwezekana tushirikiane kutengeneza kitu kama Documentary kama ya majaribio ili kuangalia kama jamii itapokeaje.

Naamini kwa kupitia makala hizi za kesi ninazoziweka humu kila Ijumaa, kuna uwezekano wa kupata maoni zaidi ambayo yatatimiza ndoto hiyo.

Pamoja Daima
 
Mzee Mtambuzi, heshima mbele mkuu. Nina swali moja. Hivi unajikita tu katika kutuletea kesi zilizotokea Tanzania na zinazowahusu Watanzania au hata za kwingine ili mradi ziwe ziliwahi kukamata nadhari ya watu?

Nimeuliza kwa sababu kuna kesi kama zile za O.J. Simpson na Clara Harris ambazo zote zilihusu mambo ya mapenzi na ambazo simulizi zake zinasisimua sana.

Salaam kwako mkuu.
Ni kweli naandika kesi ambazo zimejikita kwenye nadharia mbalimbali kulingana na kile nilichokipata mtandaoni au katika Maktaba ya Mahakama Kuu. Kwa kesi za hapa nchini si rahisi kuzipata mtandaoni na hata zile ninazozipata katika maktaba ya Mahakama Kuu zinakuwa ni katika mfumo wa kesi kama ilivyo hii ya Asha Mkwizu........... Huwezi kupata back ground ya acuused na yale yaliyojiri nje ya mahakama wakati wa tukio hilo au wakati kesi ikiendelea kama ilivyo kwa wenzetu huko Ughaibuni.

Kuna kitu nimejifunza kwa Wamarekani kwa mfano, kuna kitu wanaita Accused Profile. Hii inakuwa ni taarifa ya mhalifu au mhanga ambapo inakuwa inaeleza historia yote ya mhusika tangu utotoni na hata majirani waliowahi kumuona katika makuzi yake watatafutwa walipo ili kupata taarifa sahihi za muhusika......... kwani hiyo kuwasaidia sana katika upelelezi wao. Sina uhakika kama sisi tunao utaratibu huo.

Ninatarajia kuanza kuandika makala za Crime Investigation nikiwa nimejikita zaidi kwa Wamarekani maana wao ni rahisi kupata habari zao mtandaoni na hata vitabu vinavyozungumzia namna wanavyofanya upelelezi wa matukio mbalimbali.
Hii itasaidia sana kuielimisha jamii yetu kuhusiana na swala zima la uhalifu na consequences zake.
 
Mzee Mtambuzi, heshima mbele mkuu. Nina swali moja. Hivi unajikita tu katika kutuletea kesi zilizotokea Tanzania na zinazowahusu Watanzania au hata za kwingine ili mradi ziwe ziliwahi kukamata nadhari ya watu?

Nimeuliza kwa sababu kuna kesi kama zile za O.J. Simpson na Clara Harris ambazo zote zilihusu mambo ya mapenzi na ambazo simulizi zake zinasisimua sana.

Tuanzie za Nyumbani hizi za nje tulizisikia sana daily kwenye tv na redio. tunataka hizi ambazo huwa hazitoki ovyo kwa sie wananchi kwa undani woteeeeeeee.

Bado tunasubiri zingine Mtambuzi.
 
Tuanzie za Nyumbani hizi za nje tulizisikia sana daily kwenye tv na redio. tunataka hizi ambazo huwa hazitoki ovyo kwa sie wananchi kwa undani woteeeeeeee.

Bado tunasubiri zingine Mtambuzi.

Nafanyia kazi maoni yenu..............Kikubwa ni kupata ushirikiano wa Mahakama Kuu.....................
 
.......Hii story ndio kwanza nasikia leo, ila Asha alifanya kosa kubwa la kumuua Happyness.
Angeamua kudeal na mumewe na sio kumfupishia maisha mwezie. Ukisikia mwanamke ana roho mbaya/mkatili ndio kama huyo Asha.
 
Huu mkasa unatisha!!! Yan mtu anaua then anauchoma moto mwili wa mwenzie. Sijui alipataje hyo courage maana mie na roho yangu nyepesi hata kujeruhi siwezi. Ila nimependa Asha alivyokuwa muwazi zaidi bila kupinga na kuelezea mkasa mzima kwa upana bila kuficha ficha hivyo kutupa funzo sie wengine.
 
Mkuu kuna kesi moja miaka ya 80 ilivuma sana nchini hasa kule Dodoma kuhusu Mzee Hobe Ngandu, je nini ilikuwa hatima yake
 
Eh mtambuzi umenikumbusha mbaaali sana, mama huyo alikuwa rafiki sana na mamangu na nilikuwa namfahamu kiasi kwamba siku mama alivyotuambia mambo yaliyomkuta hatukuamini kabisaa, ingawa nilikuwa bado mdogomdogo lakini I still rembmer issue yake ilikuwa ni ya aina yake kwa wakati ule kwa kweli aliwashangaza na kuwasikitisha wengi, najiuliza leo ilikuwa ni 'nguvu ya mapenzi' iliyomfanya kuuvaa ujasiri wa kufanya hayo yote au ni nini hasa! oh pole kwa ile family nzima aliwabadilishia maisha kwa siku moja tu.
 
daaah ee Mungu niondolee tamaa nije kuwa mume bora
 
Hivi mpaka leo kesi ya mauaji kuna kuwa na jury wawili tu?

Inashangaza sana kuwa Happiness amekubali kwenda kwa Asha, licha ya kuwa alikuwa akimchukulia mume wake ....
hili hata mini limenishangaza kwa kweli alikuwa na guts gani?
(thread ya siku nyingi lakini imenivuta )
 
muhanga

I will never forget maana nilisoma na mtoto wake khushe forodhani darasa la pili Nafikiri duh yaani Khushe alitia huruma jamani,natalia na umbea wangu tukamsindikiza Khushe walikuwa wanakaa upanga karibia na salenda bridge.Ee ilikuwa sheshe sio mchezo.kushe is very successful men na alikuwa na akili he was extremely handsome little boy.

Huyu Asha mkwizu kaka ake Balozi Mkwizu (huyu balozi nae drama) .Duh umenikumbusha mbali mno kushe anakaa Zambia yupo juuuuuu
 
Last edited by a moderator:
Shukrani sana, hii kesi imenifunza mengi, inabidi nikae mbali na mahawala wa mume wangu, wasije wakanitia majaribuni nikatenda nisiyowahifikiria kuyafanya.

mimi mwenyewe ndo ninayopitia kutukanwa na kukashfiwa na mahala wa mume wangu.mwingine kanipa wiki mbili nimpishe ndani. jamaani wanaume mnatutengenezea mengi ukiwa na moyo mwepesiyjatakukuta ya huyo mama .

wamama Mungu awape nguvu na hekima Dhambi ya mume isitufanye tutende dhambi wataoumia ni watoto wetu na wazazi wetu yeye anaoa mwingine. yule kafa wewe umefungwa yeye anaendelea namaisha na wanawake wengine.

mbaya sana
 
This case to me sounds kama ya simbaulanga? Ndo najishangaa hapa like inakuwaje naikumbuka.
...nadhani mama Haule alifungwa "maisha"....30yrs? ...yupo uraiani sasa, au...sina uhakika,
nyumba ikachukuliwa na jeshi..na watoto wakahama nchi kama sikosei...
mama Liundi no comment....inauma sana aiseee....

.....kesi hizi zimenikumbusha Sarah Martin Simbaulanga pia na ule wizi wa ' vijisenti'
Miaka hiyo Sokoine, Nyerere, na Kawawa wakiendesha inji hii...
 
Back
Top Bottom