Hivi what makes us think kwamba Mama Migiro anaweza kuwa kiongozi bora wa nchi ya ulimwengu wa tatu kama TANZANIA yetu? Lets get real jamani. Kama ingekuwa hivyo...hawa madiplomats wetu ndo wangekuwa wanarudi home na kuonyesha njia..kuanzia kwa akina Balali, Ndullu, Kagasheki (Veteran wa UN), Cheyo (UDP) nk. Mimi naamini yule mama ana leadership qualities. LAKINI sidhani kama ni mtu ambaye anaweza kuikabili system ya Tanzania ya leo. Kumbuka.....na yeye ni product ya kubebana hivyo hivyo hivyo (ingawa atleast alibebwa akiwa na vyeti na uwezo). Infact I would say Prof. Tibaijuka (with all her negatives) ni strong kuliko Rose...maana ni mama alithubutu kuikabili system (remember BAWATA)...Atleast. Kuongoza nchi kama TANZANIA inahitaji ujasiri wa hali ya juu kuuliza maswali ambayo hayauliziki...kitu ambacho mwalimu wangu Rose hawezi. Na wala hajawahi kufanya.
In all, Ban Ki-Moon anaweza kuamua kumdrop..kama atapata second term....Wala hilo halina tatizo ni uamuzi wake tuu...maana by all accounts Ban haja-command respect kama top notch diplomat especially in Washington and PARIS. Infact najua kabisa...kama atataka kuongezewa term ya pili..lazima atapewa masharti lukuki na akina Susan Rice na wenzake......
Infact kama ni ushauri wangu, mama Migiro akirudi bongo..asijiingize kwenye siasa tena. Aingie kwenye shughuli ambazo zina tija kwetu wananchi..mfano aje na idea mpya ya kuanzisha kitu kingine..kama policy Institute ya mambo ya Peace au mengineyo..anaweza kuwa na impact kubwa sana...Tufike pahala tujifunze mambo ya maana kutoka kwa wenzetu. TANZANIA sidhani kama tuna policy institute ya maana, sijui who makes our foreign policy, who advises Membe.....huko ndo watu kama akina Rose, Salim, Tibaijuka... wanafaa wakae..watengeneze sera za taifa letu for generations to come.
Imagine akina Halbroke etc..Clinton alivyotoka madarakani..walianzisha Centre for American Progress..kwa wanaojua ile ndo Think Tank ya Democrats.....ndo imeshape/inashape foreign policy ya democrats....akina Susan Rice leo wana unguruma UN..nk...Republicans wana ya kwao..wengi waliotoka kwenye utawala wa Bush ndo wako humo sasa...wakiangalia mikakati ya mbele...
Ingekuwa ni furaha iliyoje kuwa na mtu kama Mkapa..angekuwa Professor pale UD au chuo kingine..wa mambo ya International relations na globalization? au Sumaye, Msuya, SALIM, Malecela...etc...kibaya hatuna huo utamaduni...kwa kuingia kufundisha.... hawa wazee wange-admit makosa yao, wakaandika vitabu kuelezea sera walizozisimamia....wakaja kufundisha generation nyingine..kusudi vijana wakajua wazee walijikwaa wapi..Sadly..ndo akina mzee Malicela na uzee wao wako kwetu usukumani kukampaign kiti cha ubunge..yaani at times sijui Africa itasonga mbele vipi....Yaani unashindwa kuelewa mtu kakaa kwenye public service almost forty years..lakini ndo hivi mpaka leo wanakimbizana na watoto huko Nyarugusu....kutafuta kura. Imagine Mzee MALICELA ANGEKUWA ANAANDIKA VITABU NA KUTWAMBIA WHAT REALLY WAS HE DOING IN POLITICS AND POLICIES WHICH SHAPED OUR COUNTRY....FOR ALL THE YEARS HE WAS IN ACTIVE PUBLIC SERVICE. SAME APPLIES TO OTHERS...
YAANI HAPO NDO NAMPA HESHIMA Nyerere..aliandika mawazo yake..leo ukiongelea ujamaa..you have where to look for reference. Kifupi..mzee alituachia urithi wa kipi alikisimamia na kukiamini. Kuyakubali au kuyakaa mawazo yake, ni kitu kingine. Imagine.Mkapa anaongelea Globalization Geneva....lakini nyumbani kwake..hawezi kuwapa ideas...Jamani where do we get these leaders? Duh!