Niende moja kwa moja kwenye pointi
Kumeibuka na wimbi la wahandishi wa habari uchwara kutokana na kuongezeka kubwa la onlineTVs lakini ukiangalia utendaji kazi wao 98% wengi ni vilaza na hawana uelewa wowote kuhusu taaluma ya uhandishi wa habari ila unaweza kusema unawaone onlineTVs ila ukichunguza pia kwenye Mainstream Media hali ya ukosefu wa weledi ndo mbaya zaidi
Yani akipatikana tu mtu yeyote anaeweza kununua kamera na mic au anauwezo wa kuanzia radio na tv basi anamtafuta mtu yeyote anamuweka hapo na yeye tayari anakua muhandishi wa habari.
Sijajua kwa wengine ila kwa upande wangu sijajua kama uhandishi wa habari wa kisasa ili uonekane muhandishi mkali ni lazima uulize maswali ya kimbeya au maswali ya kutaka kuchonganisha watu pasipo sababu yani imekua ndo fasheni
Mfano juzi kuna muhandishi mmoja nimemsikia anamuuliza msanii DullySykes studio swali eti "chidbenz anatumia madawa ya aina gani"?!...ili iweje ndugu muhandishi
jana nimemsikia muhandishi mwigine anamuuliza mama mmoja kungwi ili atoe maoni yake "kwanini Rushyna anadai kua kwa hadhi ya Hamisa hakustahili kuolewa na Aziz Ki na hajui eti kampendea nini mwanume mwenye mdomo kama ule" unauliza maswali ili uchonganishe watu si ndio ndugu muhandishi?!..aya leo tena naamka tu asubuhi namsikia muhandishi mwingine anamuuliza mama zuchu kwanini zuchu wanamuita king'ang'a...ivi unauliza swali kama ili upate nini na hadhira yako umepanga kuhilisha nini ndugu muhandishi?!...yani daah fani ya uhandishi wa habari siku hizi inachezewa sana ni kinyaa kwa kweli na kuna mifano mingi sana siwezi kuimaliza yote
Naomba kuwauliza nyie wanahabari wa media za bongo ni nini hasa lengo la uhandishi wenu
1.Kuchonganisha na kugombanisha watu?
2.Kuijenga au kuibomoa jamii?
3.Kuforce content ili habari zenu zitrend?
5.Ukosefu wa weledi na profesionalism?
4. Au ni njaa tu na ukosefu wa ajira kwahiyo mmeamua kubeba vitonge kuingia mitahani kufanya vihoja?
Naiomba serikali iingilie kati kuhusu hii taaluma ya uanahabari ingefaa waandishi wote wachunguzwe elimu zao na wapewe leseni na ambao wana elimu ndogo na wasio na elimu kabisa wote warudi shuleni wakasome kwasababu 98% ya waandishi hawana weledi kabisa na fani ya uanahabri.. tasnia imejaa vilaza watupu
Waziri wa teknolojia na habari naomba lifanyie kazi hili swala na naomba kuliwasilisha hili mezani kwako kwa ajili ya utekelezaji
Tatizo wabongo wengi (kama wewe) wanapenda shortcuts na haya mapendekezo yenu yanaonesha tatizo lilipo.
Tatizo ni elimu ndogo ya jamii.
Suluhisho, ongeza elimu kwa jamii. Hao vilaza wote mpaka wabunge wasio na elimu wataondoka automatically bila sharti lolote la serikali.
Jamii iliyoelimika haitataka kusikiliza watangazaji wajinga. Kutoka hapo market forces zita dictate nani atangaze na nani asitangaze. Huhitaji sharti la serikali hapo.
Hata pendekezo lako haliwezi kusaidia kwenye jamii yenye elimu ndogo na isiyo na utashi wa kujielimisha.
Kwa sababu a stupid audience will want stupidity in their shows and market forces will dictate the shows to be stupid. This is a business, businesses cater to markets.
Na ninapoongelea elimu, siongelei vyeti, naongelea elimu.
Mgonjwa ana kifua kikuu cha UKIMWI, wewe unataka apone kwa kumpa Cofta inayotuliza kikohozi.
Huwezi kutatua tatizo.
Zaidi, utatengeneza tatizo lingine la censorship na ukiritimba.
Kwa hiyo tatizo la kwanza hutatatua, halafu utatengeneza matatizo mengine.